Jumapili iliyopita mke wangu ameniadhirisha mno kanisani

Jumapili iliyopita mke wangu ameniadhirisha mno kanisani

Kanisani unaskiza earphone!???Bora hata usingeenda tu mkuu
 
Nina muda mrefu sijaonekana jamvini, majukumu ni mengi sana. Kwa sasa mimi ni baba Gebbie, nastahili pongezi. Jumapili iliyopita baada ya ibada nilikuwa nasikiliza earphone.

Mke wangu alinifanyia hujuma, kati kati ya waumini wengine alichomoa waya kwa siri na hivyo kufanya wengine wasikie wimbo wangu. Nilikuwa nasikilza wimbo wa J Moe, 'pesa ya madafu', wote wa pembeni akiwemo mke wangu walikuwa wanacheka mno, baadaye nikagundua walikuwa wakinicheka.

Nimehisi kumchukia mpaka leo hii, na niliondoka muda ule ule. Amenibembeleza lakini wapiii! Nina hasira naye sana. Amenidhalilisha, ameishusha heshima yangu. Na hivi kulikuwa na watu wachache, je wangekuwa wengi?

Hovyo kabisa!
Hahahaha umenichekesha sana aisee
 
Tafuta pesa br,huna hela ndio maana unadhalilishwa
 
Ukitoa earphones simu huwa ina pause media inayoplay kwa muda huo
 
Back
Top Bottom