Jumapili njema ya mwisho wa mwaka

Jumapili njema ya mwisho wa mwaka

Daudi Kempu

Member
Joined
Dec 6, 2024
Posts
26
Reaction score
56
Pole kwa kila gumu lililokusumbua mwaka huu; kama uliumwa, uliumia, uliumizwa, uliteseka, au ulitikiswa kivyovyote hisia zako na ukadhani usingetoboa kuiona leo...POLE MNO.

Hongera kwa kutojikatia tamaa. Mbali na maumivu na changamoto zote, hujakufuru.

Hujajisusa, hujajinyonga, hujajitosa baharini, hujafanya japo jaribio tu; la kujiua HONGERA SANA.

Haukuwa mwaka mwepesi kwa baadhi yetu. Lakini, pamoja na ugumu wake, hatujaruhusu tabasamu liondoke katika taswira zetu. Hivyo ndivyo tulivyo wakomavu.

Nguvu ndani yetu ni kubwa kuliko kila jabali linalopiga maisha yetu. Ujasiri tulionao, ni zaidi ya neno lenyewe. Tuna nguvu.

Zaidi ya MUNGU pengine hakuna kabisa mwingine aliyesimama upande wetu mwaka huu. Mimi na wewe tunashuhudia kuwa; kama si REHEMA zake, ujasiri wetu, ungeyeyuka kama barafu juani.

Tutafute nafasi ya kumshukuru. Tutenge muda wa kumuelekezea mioyo yetu. Tunyenyekee tu, halafu tuishie na "ASANTE KWA YOTE MUNGU"

Kama si yeye, sisi wengine, sijui ingekuwaje!

Hata kama bado unapita katika changamoto. Mwisho huu wa mwaka, mshukuru. Mshukuru.
Mshukuru tu.

Kuna namna moyo wa sukrani hufungua vifungo vinavyozidi kukazwa na moyo wa malalamiko.

MSHUKURU MUNGU KWA YOTE.

Naelewa sio vyepesi, najua si rahisi. Onyesha ukomavu, mshukuru MUNGU kwa mwaka unaoelekea ukingoni, halafu andaa moyo wako kuukabili mwaka mpya kwa ujasiri zaidi.
MUNGU AKUVUSHE SALAMA MPENDWA WANGU.
 
Back
Top Bottom