singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Katika mambo ambayo yamekuwa yakinikanganya nia haya ya warioba na tume yake ambapo mpaka sasa wamekuwa wakitumia majukwaa mbali mbali kusema kuwa yale waliyoyakusanya ni maoni ya wananchi, miongoni mwa wanaosema hivyo ni rafiki yangu Polepole , hivi majuzi nimemsikia naye mzee wetu Butiku akiitaka tume ya uchaguzi utumie fursa hii ya kusogezwa mbele kura ya maoni kwa kuyarudisha mapendekezo ya tume ya warioba ambayo yaliondolewa na bunge maalum la katiba.
Lakini pia hata Jaji Warioba amekuwa akisisitiza kuwa wao wamechukua maoni ya wananchi na kuwa kilichomo katika rasimu yao ya katiba ni matakwa ya wananchi walio wengi, hasa lile suala la mfumo wa serikali tatu.
Tukirudia katika Tume ya Warioba, kwa Tanzania Bara, waliozungumzia Muungano walikuwa 39,000. Kati yao, ni watu 27,000 tu ndio waliozungumzia Muundo. Na kati ya hao, watu 16,470 (61%) walitaka serikali tatu. Kwa Tanzania Visiwani, waliozungumzia Muungano walikuwa 38,000 na ni nusu yao tu (19,000) waliozungumzia muundo. Kati ya hao, watu 11,400 (60%) walitaka serikali ya mkataba.
Ukijumlisha idadi ya watu ambao hawakugusia muundo wa Muungano, Bara na Visiwani, ni 27,000. Hawa ni wengi kuliko watu 16,470 waliotaka serikali tatu.
Ukikokotoa jumla ya waliotaka mkataba na serikali tatu ni watu 27,870, na hawa ni 36% ya jumla ya watu waliozungumzia Muungano. Jumla hii ni tone ya maji baharini ikilinganishwa na watu wapatao 333,537 waliotoa maoni katika Tume ya Katiba.
Kwa maneno mengine, waliotaka mkataba au serikali tatu walikuwa asilimia nane tu ya waliotoa maoni. Pia, watoa maoni 287,537 sawa na asilimia 86% hawakugusia kabisa Muungano au muundo wake. Sasa iweje watu 16,000 wawakilishe maoni ya Watanzania milioni 45? Je, uwingi aliousema Jaji Warioba kautoa wapi?.