Jumapili tunasherekea miaka 51 ya Muungano, tujiulize haya ya Serikali tatu, Warioba aliyatoa wapi?

Haya ni maneno mnayoyapewaga kwenye semina elekezi eti "UZANDIKI" uzandiki ndio limnyama gani? Uzito wa serikali tatu wananchi wako tayari kuubeba (after all kama upo huo mzigo)

Mizigo wanayobebeshwa sasa huioni kuwa imewalemea sana, wananchi wa Tanzania wanatunza marais WATANO!!!! Nyie hamuoni limzigo hili.

Nakwambia mara hii UKOME KUNIAMBUKIZA UJINGA.

Wananchi wako tayari kubeba mzigo wa serikali 3 wawapi hao? Na umekutana nao saa ngapi ukawauliza! Kama huwezi kuchangia ni heri ukakaa kimya kuliko kutunga uongo,Serikali 3 ni mzigo kuanzia utawala na uendeshaji wake fikiri sawasawa na uniambie kama moja ikigoma kuchangia itakuaje?serikali gani isiyokuwa na ardhi?vyanzo vyake vya mapato n.k? Acheni kusindikiza ujinga tumeshatoka huko!!!
 
"Tanganyika imevaa koti la muungano"
Zanzibar nchi ina wimbo,bendera nk na sasa wanataka fedha zao.

Hilo koti nani kalishona?acha kejeli kwa wananchi?nenda kasome vizuri Muungano wetu ni wa nchi ngapi?afu ndo utajua Zanzibar ni nchi au sio nchi?kama sio nchi itaunganaje na nchi nyingine?Pia fuatilia kwa makini kwenye katiba inayopendekezwa utaona masuala ya Muungano yamewekwa wazi na kuna mambo mengi yanayotuunganisha na ndio maana tunaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!kama hujaelewa hapo naomba uulize!
 
Kama hao laki 3 hawana haki ya kushawishi aina ya muungano mbona hao million 40 walikaa kimya sababu hawajali aina ya muungano hata usipokuwepo kwao ni sawa basi tupitishe serikali 3

Acha kutengeneZa sylogism zisizokuwepo na zisizo na maana,umamshawishi nani na serikali 3 hiyo ya tatu inamuongoza nani?unataka kuruka kbla hujaota mabawa?
 
Kwani wakati tunaunga ni wananchi wangapi waliulizwa, wangapi waliridhia serikali mbili.

Weka data hapa.

Kama waliamua Nyerere na karume peke yao, basi this time (kwa maana ya tume ya warioba) watanzania wengi sana wamependekeza aina ya muungano wetu.

Ha ha ha ha unauliza swali?Muungano huujui kaa kimya we dotcom!ungekuwa umezaliwa time hizo ungekua na adabu ha ha ha hujui unachangia nini!
 
Kama hao laki 3 hawana haki ya kushawishi aina ya muungano mbona hao million 40 walikaa kimya sababu hawajali aina ya muungano hata usipokuwepo kwao ni sawa basi tupitishe serikali 3
Kama hujui hayo mambo ya muungano kakak bora uwe kimya tuu maana dah basi tuuu
 
Kwakweli kusema ni kazi rahisi. “Serikali mbili ni kiini macho” Mimi hujanishawishi bado hata kidogo. Huwezi kusema ni kiini macho wakati watu wengine wanatamani maisha ya Watanzania na kuomba kupata uraia wakijua hapo ndipo maisha yao yatakuwa na maana na manufaa, leo hii wewe unakaaa na kuafanya mambo yako hata kuweza kusema hayo. Anyway, maisha yako na jamii ni ya muhimu. Tuungane tujenge nchi yetu Tanzania.

Usitamani usichokijua na wala usitamani vitu vya watu wengine hata maandiko yanasema “Usitamani mali ya mtu mwingine”. Tanzania tumeamua rasmi dhati kujenga nchi yetu yenye jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu. Huo ni mwanga na msingi mwema wa nchi yetu.

Mkuu naona kuna ugumu wa kuelewana hapa, kusema serikali mbili ni kiini macho sikuwa na maana kuwa Tanzania ni nchi mbaya. Sina hakina kama kweli watu wanataka kuwa raia wa tanzania kutokana na kuwa na serikali mbili au kutokana na utulivu. By the way kuna watu wanataka kuishi kwenye nchi zenye serikali moja kama Japan, au kwenye serikali 51 kama Marekani, au serikali nne kama UK, wengine hata kwenye madola ya kifalme. Tutajenga Tanzania ikiwa nchi ya serikali moja, serikali mbili au hata tatu na kuendelea.

Lakini ukiini macho uliopo kwenye mfumo wa serikali unaendelea kuwepo, na watanzania sio kama tutakaa kusibiri kuondoa kiini macho hicho ndio tufanye kazi.

Inabidi kuangalia mambo kwa laser, ni bora kuliko kuangalia kwa ujumla jumla.
 
Serikali tegemezi hatuitaki!Serikali isiyo na ardhi yake peleka huko,vargue case study ndo unataka kuzileta Tz ziwe applicable never look the kind of union we have ndo utagundua ni tofauti na hiyo ya kimagumashi unayoitaja wewe isiyojitambua na utitiri wa viserikali kila kimoja kina mandate yake,kazi kutunishiana misuli tu, Serikali mbili zetu zinatosha sana miaka 51 sasa unataka nini tena?
 
Kwa mantiki yako naoana unakubalaiana na mimi ni kuwa serikali moja inafaa kuliko ya sasa. kama unazungumzia suala la kutunishiana misuli tunaweza kukumbuka sana Salmin alivyokuwa akifanya....

Kwanini tunakuwa waoga kutaka serikali moja, na tunakuwa na sauti kubwa kukataa mbili? au kutaka tatu?
 
Mimi hiyo ya Serikali moja siijui na hiyo ya serikali 3 siijui! Ninachoweza kusema Serikali 2 nazijua na nimeishi kwa hizo kipindi kirefu na sioni taitizo kubwa la kuziondoa, palipo na changamoto zirekebishwe mambo yaense mbele naaamini itakua hivyo maana sasa tuna miaka 51 ni miaka mingi tunapaswa kumshukuru Mungu na kujivunia Tunu hii iliyotukuka!
 
Mkuu ni sawa na kusema mimi nimekula sana mchicha, naujua vizuri kwa hiyo nataka kuendelea nao, sikubaliani na samaki na maharage. Kutojua kitu au kutokizoea haina maana kuwa ni kibaya. Unaposema tumshukuru mungu pia unakosea, sidhani kama huu muugano uliletwa na Mungu, nina hakika kuna wanaosema mungu tusaidie ubadilike.
 
BONGOLANDER Usifananishe muungano na vyakula, au mavazi unayoweza kulala tu na ukiamka ukanunua mengine au chakula ukanunua kingine! Muungano ni Tunu, Muungano ni heshima sio nguo wala chakula! Angalia Afrika ni nchi ngapi zimeungana then utaona upekee wa Tanzania afu unaanza kushabikia, lipo kundi la watu wachache sana wanatumika wanataka uvunjike hata leo kwa masilahi yao binafsi ya madaraka, hawa hawajui wanalofanya tuwasamehe tu wakikua wataacha na wakiendelea wameshalaniwa! Mungu Ibariki
Tanzania,Mungu Ubariki Muungano!
 
Kwani huo muungano umevunjika? sasa kwanini mnaujadili as if umekufa wakati hata kwenye katiba hii inayopendekezwa katka Sura ya Kwanza Ibara ya 5 imezitaja tunu za taifa letu ambapo muungano umetajwa, na lengo la kuwa na serikali mbili ni kuhakikisha kuwa Muungano wetu pia unazidi kuimarika siku hadi siku, nyie mnaotaka uvunjike Mungu atawalaani, Warioba na mambo yake ya Srrikali 3 yalishapitwa na wakati kwa mujibu wa sheria kwa sasa tunachokijua ni Katiba Inyaopendekezwa na sio Rasimu tena hiyo ya babu Warioba.
 
BONGOLANDER Usifananishe muungano na vyakula, au mavazi unayoweza kulala tu na ukiamka ukanunua mengine au chakula ukanunua kingine! Muungano ni Tunu, Muungano ni heshima sio nguo wala chakula! Angalia Afrika ni nchi ngapi zimeungana then utaona upekee wa Tanzania afu unaanza kushabikia, lipo kundi la watu wachache sana wanatumika wanataka uvunjike hata leo kwa masilahi yao binafsi ya madaraka, hawa hawajui wanalofanya tuwasamehe tu wakikua wataacha na wakiendelea wameshalaniwa! Mungu Ibariki
Tanzania,Mungu Ubariki Muungano!

Mkuu unatakiwa kujua kuwa muungano si tunu, ni kazi ya Julius Nyerere na Abedi Karume, na sababu kubwa ilikuwa maslahi yao ya kisiasa. Wakati wanaungana wao walikuwa wanajua wanafanya nini.

Unajua mimi sipingi muungano, napinga muungano wa serikali mbili napenda tuwe na serikali moja tuwe na Tanzania tu, sio Tanzania na zanzibar.

Kama unafuatilia mjadala kuhusu katiba mpya unaweza kuona kuwa kuna watu wanapigana kwa nguvu muungano uendelee kuwepo, hasa kwa sababu ya madaraka..uroho wa madaraka na sio kwa sababu wanaona muungano unafaa. Kwa hiyo kuna wale wanaopigania muungano kwa sura ya sasa ili wakiwa marais madaraka yao yasipungue, na unguja kuna wanaotaka uvunjike kwa sababu hiyohiyo.
 
Nenda kalale we dotcom usijifanye kizazi cha nyoka,Muungano huujui!!mbaguzi mkubwa na mpinga Muungano,na kwa taarifa yako hauvunjiki!!kwa maneno yako ya kwenye kanga!
 
Mkuu unatakiwa kujua kuwa muungano si tunu, ni kazi ya Julius Nyerere na Abedi Karume, na sababu kubwa ilikuwa maslahi yao ya kisiasa. Wakati wanaungana wao walikuwa wanajua wanafanya nini.

Unajua mimi sipingi muungano, napinga muungano wa serikali mbili napenda tuwe na serikali moja tuwe na Tanzania tu, sio Tanzania na zanzibar.

Kama unafuatilia mjadala kuhusu katiba mpya unaweza kuona kuwa kuna watu wanapigana kwa nguvu muungano uendelee kuwepo, hasa kwa sababu ya madaraka..uroho wa madaraka na sio kwa sababu wanaona muungano unafaa. Kwa hiyo kuna wale wanaopigania muungano kwa sura ya sasa ili wakiwa marais madaraka yao yasipungue, na unguja kuna wanaotaka uvunjike kwa sababu hiyohiyo.
Kwako wewe sio tunu kwetu sisi watanzania halali katiba inayopendekezwa imeitaja kama moja ya tunu, kama huupendi huu muungano basi bora ukajinyonge uondoe balaa humu ndani.
 
Back
Top Bottom