jumatatu nasimama mahakamani nipeni nondo wadau

jumatatu nasimama mahakamani nipeni nondo wadau

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,293
jambo wakuu.
Kama wiki mbili zimepita walivunja nyumbani kwangu mchana na kuiba hela, nguo, walet yenye vitambulisho vyangu na kubeba vitu kwenye dressing table.
Nilienda polisi kuripot na kupata RB.
Baada kama ya siku tatu kuna jirani angu kasahau mlango wazi ile anarudi anakuta simu mezani haipo ikabidi aite vijana wa mtaani wazunguke pande zote kufatilia ndipo wakamkuta jamaa walipomuhoji na kumsachi wakamkuta na hiyo simu na walet yenye driving licence yangu na atm card wakaniita manake wananifaham tukampeleka polisi baada ya kumgonga kidogo.
Mwizi kakiri mbele ya polisi na kachukuliwa maelezo yote.
Ijumaa kapelekwa mahakamani cha ajabu kakana kuwa hajawahi kuiba na hanijui ila wallet yangu bado iko polisi.
Jumatatu kesi inasomwa tena hebu nipeni uzoefu hapa nafanyeje
 
Hata mimi namuwaza lowasa tu
Ila maadamu mashahidi wapo na police waliona utashinda kwa mwizi kwenda jela

Au wewe unatakeje kwani
 
duh kweli sa ivi siasa ndo kila kitu haina noma ntapambana kiume hiyo jumatatu

Pole sana kwa madhila yaliyokukuta sina uzoefu na mambo ya mahakamani ila huko nako kuna fitna nyingi sana vyema ukae vizuri na mpelelezi wa hilo tukio ndio atakupa picha itakavyoenda.
 
Pole sana muathirika wa uhalifu.Jiandae kwa maswali magumu na yakutumia akili.Epuka kuutegemea ushaidi ulioupata polisi kuwa mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo mara baada ya kupigwa maana ushaidi wa namna hiyo haupokelewi mahakamani isipokuwa kama kupigwa kule kulisababisha kupatikana vitu vilivyoibiwa, kutumika kukamilisha tukio.Mahakamani utapaona kama sebuleni kwenu kama utaongea ukweli tupu.
 
jambo wakuu.
Kama wiki mbili zimepita walivunja nyumbani kwangu mchana na kuiba hela, nguo, walet yenye vitambulisho vyangu na kubeba vitu kwenye dressing table.
Nilienda polisi kuripot na kupata RB.
Baada kama ya siku tatu kuna jirani angu kasahau mlango wazi ile anarudi anakuta simu mezani haipo ikabidi aite vijana wa mtaani wazunguke pande zote kufatilia ndipo wakamkuta jamaa walipomuhoji na kumsachi wakamkuta na hiyo simu na walet yenye driving licence yangu na atm card wakaniita manake wananifaham tukampeleka polisi baada ya kumgonga kidogo.
Mwizi kakiri mbele ya polisi na kachukuliwa maelezo yote.
Ijumaa kapelekwa mahakamani cha ajabu kakana kuwa hajawahi kuiba na hanijui ila wallet yangu bado iko polisi.
Jumatatu kesi inasomwa tena hebu nipeni uzoefu hapa nafanyeje

Tatizo letu Wabongo tunapenda kurahisisha sana mambo. Dunia hii ya utandawazi wa sasa itatufundisha mengi.

Ni vema upatapo tukio la kuibiwa utoe ripoti kwa mamlaka husika hii ni kwa usalama wako na mali ilyoibiwa ikiwa itapatikana. Vinginevyo usivofanya hivyo una ji-risk kwa mengi,

Kwa msaada tu, tafuta watu au officials credible waliojua kuibiwa kwako wakakujengee hoja tetezi, Maana hivi sasa mzigo uko kwako!
 
Acha kuwa muoga,mahakama ipo kwa ajili yako,cha msingi simamia maneno aliyochukuliwa kituo cha polisi,maana lile jarada la kesi ndilo linatumika mahakamani kumsomea mashtaka mtuhumiwa,
 
Fanya uchunguzi kwanza kuona endapo kuna uwezekano wa kuvipata vitu vyako vilivyoibiwa kutoka kwa huyo jamaa, kama tayari hakuna uwezekano au pengine tayari vimeuzwa, angalia kama huyo mtu anaweza kulipa fidia ya upotevu wa mali zako, kama hana sikushauri usumbukie kitu ambacho mwishoni utakuwa sawa na mwanzoni.

Cha msingi ni kuhakikisha unaziba mianya yote inayoweza kupelekea ukaibiwa tena, kama tatizo ni sehemu uliyopanga, fanya mipango ya kuhama, huyo aliyekuibia ipo siku dunia itamfunza tu, hakuna haki mkuu usihangaike kama huna uhakika wa kurejeshewa mali zako.
 
shukrani kwa mawazo kesho ndo mahakamani ngoja tuone. Manake anaweza kana kuwa kaiba? Na je vitambulisho vyangu ambavyo kakutwa navyo atavikanaje? Kama akishindwa kurejesha garama zangu hata akienda segerea poa tu manake nimepata taarifa hapa kuwa huyu mwizi wangu taarifa zake mahakamani zipo na alishawahi kuhukumiwa kwa kesi ya wizi katoka anaendelea
 
Mrejesho wa mahakamani????
 
Back
Top Bottom