Jumba la Kifahari la Askofu Kakobe

Jumba la Kifahari la Askofu Kakobe

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
19,629
Reaction score
34,199
Sema chochote.


1615050364361.png


1615050361190.png
 
Yesu akirudi kuwaona hawa wanaojiita manabii maisha wanayoishi, sambamba na yeye maisha alivyoishi. Atajikuta anacheka mwenyewe tu.

Maana atakutana na huyu Nabii anaishi kama mfalme, mara yule Nabii kamlaza kondooo kifo cha mende, sijui nani nani Nabii kafumaniwa na mke wa mtu, Nabii Rashidi kaiba kura (Nabii Mwizi). Hatari na nusu.
 
Kiukweli mi naamin Mungu yupo Ila hawa wanaojiita manabii na mitume / wachungaji wa makanisa na maaskofu wengi wanamuwakilisha Mungu isivyo , ...wamebase Sana kwenye kutoa Mali uwape , na kujilimbikizia huku waumini wakibaki stressed na ufukara wa kutupwa ..... Aiseee mi Kwa vile naifahamu biblia so najua uhusiano wangu na Mungu anataka nini , hawa watu sio wazur sana ..... Madam Mungu ashatupa vitabu vya dini is better tukatafta uhusiano wetu na yeye privately , ...... Hawa watu wengi wao sio wazur
 
Kumtumikia Mungu unatakiwa uende wapi ?
Isaya 55
6 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,Mwiteni, maadamu yu karibu;
7 Mtu mbaya na aache njia yake,Na mtu asiye haki aache mawazo yake;Na amrudie BWANA,Naye atamrehemu;Na arejee kwa Mungu wetu,Naye atamsamehe kabisa.
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
12 Maana mtatoka kwa furaha,Mtaongozwa kwa amani;Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
13 Badala ya michongoma utamea msunobari,Na badala ya mibigili, mhadesi;Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina,Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
 
Kama na kanisa wanaloabudu ni la kifahari kama hii nyumba au zaidi basi hakuna tatizo, lakini kama kwa kanisa lile linalopigwa na vumbi pale big no.
Hawa wachungaji wanajua yapasayo kufanya na ni mahodari sana kufundisha haki ila kutenda ni zero.
 
Ndiyo maana nashangaa eti ninunue CD za akina Diamond, niendelee kuwatajilisha
 
Back
Top Bottom