Jumba la Kifahari la Askofu Kakobe

Kanisa Kwake ni marufuku kuvaa mikufu,na vidani vya dhahabu,shaba nk,lakini yeye ni ruhusa kuishi kwenye ukwasi wa namna hii?!!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo nyumba ni ya kifahali sana...ukijaribu kupita usiku utaona hadi madhari ya kifahali ya ndani. Ipo pale mbezi chini raibow junction ya kupandisha kuja tangi bovu kulia...imesimama hatari
 
Vipi ndugu, kwa hiyo wewe unafanya ibada peke yako?
 
Hahahahahaha ewe tomaso fungua macho
Hakika mimi ni Tomaso! Bwana Mwokozi alisema "ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbinguni"!! Sasa unataka kusema Bwana wetu mwokozi alitupiga changa la macho, au ni hawa mitume wetu ndio hawalifuati neno la Mwokozi?!
 
Yesu mbona alishamaliza, wala hashangai! alisema anawajua walio wake

Yohane 10:14-15 BHN​

Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi, kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.

Na tena akasema si kila aitaye bwana bwana

Mathayo 7:21 BHN

“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.

Mathayo 7:23 SRUV

Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


 
Mkuu unasali kwa Kakobe??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…