Shamba kubwa la Neverland linalomilikiwa na marehemu Michael Jackson limeuzwa kwa mwekezaji bilionea kwa robo ya thamani.
Ron Burkle, rafiki wa zamani wa Jackson, hivi majuzi alinunua nyumba iliopo katika shamba hilo huko Los Olivos, California, msemaji wake alisema .
Alilipa $22m (£16.2m) kwa jumba hilo la kifahari, limesema jarida la Wall Street Journal, akiweka wazi rekodi zake na kuwataja watu watatu waliohusika katika makubaliano hayo. Jumbe hilo lililojengwa katika ekari 2,700 (1,100 hectare) kwa mara ya kwanza lilinadiwa kwa $100m in 2015.
Tangu wakati huo jumba hilo la Neverland, lililopo kaskazini mwa mji wa Santa Barbara limekuwa likiuzwa hivi karibuni kwa $31m.
Jackson alinunua jumba hilo kwa $19m, ambalo baadaye alililitaja baada ya kisiwa kisichojulikana katika kitabu kilichoandikwa na Peter Pan .
Mwanamuziki huyo alilinunua jumba hilo mwaka 1987 , na kulifanya kuwa nyumbani kwake wakati wa umaarufu wake..
Alibadilisha jumba hilo na kuwa eneo la burudani , akijenga eneo la kufuga wanyama mbali na ukumbi wa chini ya ardhi ambapo aliwafurahisha watoto na familia zao.
Miaka 1990 na 2000 , Jumba hilo lilichunguzwa sana kutokana na madai ya udhalilishaji watoto kingono dhidi ya msanii huyo.
Jackson alilibadilisha jumba hilo na kuwa eneo la watoto kuchezea
Bwana Burkle mwenye umri wa miaka 68 , ni mwanzilishi na msimamizi mwenza wa Yucaipa Companies, LLC, kampuni ya uwekezaji wa kibinafsi .
Thamani ya Burkle kufikia tarehe 24 mwezi Disemba 2020 ilikuwa $1.4bn, kulingana na jarida la Forbes.
BBC