Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JUMBA LA USHIRIKA UKILITAZAMA KUTOKA MTAA WA LIVINGSTONE 1960s
Nikiangalia hii picha inanikumbusha mbali mwaka wa 1964.
Nyumba hiyo iliyoko Mtaa wa Livingstone na aina ya nyumba hizo hazipo tena Dar-es-Salaam.
Nilikuwa na miaka 12.
Moja ya michezo tuliyopenda kucheza ilikuwa kupanda ngazi za nje ya jumba hili hadi juu kabisa na kuiangalia Dar es Salaam yote.
Nawakumbuka rafiki zangu na wengine wameshanitangulia mbele ya haki.
Namkumbuka Mohamed Kitunguu na nduguye Ali "Nakioze," Hussein.
Ali alikuwa mdogo kwangu kwa umri lakini ndiye aliyenifunza kuvua samaki kwa mshipi.
Hamza Msangamapesa, Ebby Sykes, Sindbad Bomu na wengine sura zinanijia majina siyakumbuki.
Nakumbuka siku hizo nyimbo nilizokuwa nazipenda na zikipigwa radioni.
Na nikiziimba.
"It is a Young World," ya Rick Nelson, "Thank You Girl," The Beatles na "Roses Are Red," ya Jim Reeves.
Angalia hizo ngazi kulia la hilo jumba.
Tukizipanda bila kupumzika njiani hadi tufike.juu.
Jumba la Ushirika lipo Mtaa wa Lumumba likiangalia Mnazi Mmoja.
Hili jumba limekarabatiwa na muonekano wake wa sasa ni mwingine kabisa.
Hapo lilipojengwa jumba hilo kulikuwa na nyumba kadhaa ambazo ilibidi zivunjwe kupisha ujenzi wa jumba hilo.
Katika nyumba hizo zilizovunjwa moja ilikuwa nyumba ya Bi. Mruguru bint Mussa mama yake Abdul Sykes.
Mwalimu Nyerere alimwandikia barua Bi. Mruguru akimuomba ruhusa akubali hiyo nyumba ivunjwe na serikali ili pajengwe jumba la Ushirika na yeye atalipwa fidia.
Kwa nini Mwalimu aliona lazima yeye binafsi aandike barua ile na si Waziri wa Ardhi?
Huyu Bi. Mruguru bint Mussa ni nani khasa?
Sababu ni kuwepo na ikhsani kubwa kati yake na Bi. Mruguru.
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Julius Nyerere alikuwa akienda sana nyumbani kwa Bi. Mruguru Kirk Street (sasa Mtaa wa Lindi)akiongozana na Abdul Sykes.
Fidia aliyolipwa Bi. Mruguru kwa ajili ya nyumba hii alinunua nyumba nzuri sana Mtaa wa Uhuru.
Nyumba hii ilikuwa imegusana na nyumba ya Zuberi Mtemvu.
Siku zote hujiuliza ingekuwaje kama Bi. Mruguru angekataa kuuza nyumba yake?
Siku zile za kupigania uhuru Bi. Mruguru aliweza kutoka nyumbani kwake Kirk Street akaja New Street kwenye nyumba yake hii akatandikiwa mkeka barazani akamsikiliza mwanae Nyerere akihutubia mkutano wa TANU.
Kulia ni Bi. Mruguru bint Mussa mama yao Abdulwahid, Ally na Abbas Sykes.