Jumba la Ushirika 1964

Jumba la Ushirika 1964

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
JUMBA LA USHIRIKA UKILITAZAMA KUTOKA MTAA WA LIVINGSTONE 1960s

Nikiangalia hii picha inanikumbusha mbali mwaka wa 1964.

Nyumba hiyo iliyoko Mtaa wa Livingstone na aina ya nyumba hizo hazipo tena Dar-es-Salaam.

Nilikuwa na miaka 12.

Moja ya michezo tuliyopenda kucheza ilikuwa kupanda ngazi za nje ya jumba hili hadi juu kabisa na kuiangalia Dar es Salaam yote.

Nawakumbuka rafiki zangu na wengine wameshanitangulia mbele ya haki.

Namkumbuka Mohamed Kitunguu na nduguye Ali "Nakioze," Hussein.

Ali alikuwa mdogo kwangu kwa umri lakini ndiye aliyenifunza kuvua samaki kwa mshipi.

Hamza Msangamapesa, Ebby Sykes, Sindbad Bomu na wengine sura zinanijia majina siyakumbuki.

Nakumbuka siku hizo nyimbo nilizokuwa nazipenda na zikipigwa radioni.

Na nikiziimba.

"It is a Young World," ya Rick Nelson, "Thank You Girl," The Beatles na "Roses Are Red," ya Jim Reeves.

Angalia hizo ngazi kulia la hilo jumba.

Tukizipanda bila kupumzika njiani hadi tufike.juu.

Jumba la Ushirika lipo Mtaa wa Lumumba likiangalia Mnazi Mmoja.

Hili jumba limekarabatiwa na muonekano wake wa sasa ni mwingine kabisa.

Hapo lilipojengwa jumba hilo kulikuwa na nyumba kadhaa ambazo ilibidi zivunjwe kupisha ujenzi wa jumba hilo.

Katika nyumba hizo zilizovunjwa moja ilikuwa nyumba ya Bi. Mruguru bint Mussa mama yake Abdul Sykes.

Mwalimu Nyerere alimwandikia barua Bi. Mruguru akimuomba ruhusa akubali hiyo nyumba ivunjwe na serikali ili pajengwe jumba la Ushirika na yeye atalipwa fidia.

Kwa nini Mwalimu aliona lazima yeye binafsi aandike barua ile na si Waziri wa Ardhi?

Huyu Bi. Mruguru bint Mussa ni nani khasa?

Sababu ni kuwepo na ikhsani kubwa kati yake na Bi. Mruguru.

Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Julius Nyerere alikuwa akienda sana nyumbani kwa Bi. Mruguru Kirk Street (sasa Mtaa wa Lindi)akiongozana na Abdul Sykes.

Fidia aliyolipwa Bi. Mruguru kwa ajili ya nyumba hii alinunua nyumba nzuri sana Mtaa wa Uhuru.

Nyumba hii ilikuwa imegusana na nyumba ya Zuberi Mtemvu.

Siku zote hujiuliza ingekuwaje kama Bi. Mruguru angekataa kuuza nyumba yake?

Siku zile za kupigania uhuru Bi. Mruguru aliweza kutoka nyumbani kwake Kirk Street akaja New Street kwenye nyumba yake hii akatandikiwa mkeka barazani akamsikiliza mwanae Nyerere akihutubia mkutano wa TANU.

Kulia ni Bi. Mruguru bint Mussa mama yao Abdulwahid, Ally na Abbas Sykes.

Screenshot_20220207-163526.jpg
 
Mzee wa kulia Lia na mfumo Kristo.
Wa kupuliza

Sikulaumu kwa kunikejeli.

Sababu inawezekana hili somo unalojadili hulijui.

Inawezekana pia wewe hunifahamu kwani asiyekujua hakuthamini ukadhani unaweza kunikejeli, kunidhihaki na kunitusi.

Mimi ninapokutana na mtu mfano wako wajibu wangu ni kwanza kujaribu kukufunza heshima ya majadiliano kisha kukusomesha somo lenyewe.

Hapana faida katika kukosa adabu nadhani hili kwenu umefunzwa.

Hapa mimi nakukumbusha tu kuwa ikiwa mtovu wa adabu unamtukanisha mama yako.

Hivi ndivyo mimi ninavyowafunza wanangu kuwa mkiwakosea adabu watu watakuchukulieni nyinyi ni watoto mliozaliwa vichochoroni.

Sasa tuje kwenye somo lenyewe.

Soma hapo chini kisha rejea kwenye mjadala tujadili kwa heshima na adabu:

"Professor mmoja wa UDOM aliyekua VC alipata malalamiko kuhusu baadhi ya watu kutotendewa haki kwenye ''admission.''

Wakati huo TCU ilikua haijaundwa.

Alipoamua kuitisha ''applications'' zote akakutana na maajabu.

Kuna zaidi ya ''applicants'' 350 walikua wameachwa huku wakiwa wame ''qualify'' huku kukiwa na idadi ya kutosha kabisa wakiwa wamepata ''admission'' wengine wakiwa ''below cut-off point'' ya chuo.

Kwa “sudfa” au ''coincidence'' wote waliokua wameachwa kwa dhulma walikua na majina ya Kiislamu na wote walioku ''admitted'' walikua na majina ya Kikristo.

VC akatoa ''order'' mchakato urudiwe tena japo jambo hilo lilikua ''down played.''

Miaka ya karibuni kulikua na zoezi la kuwaondoa waalimu wa masomo ya arts sekondari waajiriwa wa serikali kuwarudisha shule za msingi. Zoezi husika halikuwahusu waalimu wa masomo ya sayansi na hesabu

Nilikua mkoa fulani kipindi zoezi hili linaendelea.

Kukatokea malalamiko kua zoezi hilo lina sura ya ubaguzi na waathirika ni Waislamu.

Ofisa mmoja Muislamu katika idara ya elimu ambaye hapo awali alikua amejaribu kuomba uhamisho kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya miaka miwili bila mafanikio alipokea malalamiko hayo na baada ya kujiridhisha ni ''genuine'' akayapeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.

Kikaitwa kikao kati ya Mkurugenzi, Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma, Ofisa Utumishi na yule ofisa aliyeipeleka ''issue'' kwa Mkurugenzi.

Wahusika wote kasoro yule aliyepeleka malalamiko walikua Wakristo na ilivyoonekana baada ya kikao kuanza ni kutaka kum ''pin'' huyo ofisa kwa nini analeta udini kwenye utendaji wa kazi za Halmashauri na hususan hilo zoezi la kitaifa.

Walianza kumpa maneno makali kabda hata hawajamuuliza kuhusu ushahidi.

Walipomuuliza atoe ushahidi wa madai yake akaoonyesha majina wa wahusika waliohamishwa.

Shule ina waalimu 68 kati yao Waislamu 18.

Waalimu wanaotakiwa kupelekwa primary schools ni 21.

Basi wakaondolewa wale wote 18 wenye majina ya Kiislamu na hao wengine 3 wasiokua Waislamu.

Kikao bado kikasema huo sio ushahidi maana Mkuu wa Kituo (Headmaster) ana ''discretion'' ya kuchagua mradi anafata ''secular'' iliyotolewa na Wizara (TAMISEMI).

Ndipo akaangusha bomu la''Atomic'' ambalo alikua hajawaambia ''before.

Kwamba katika wale waalimu Waislamu 18 watatu ni wa Mathematics na sita ni wa masomo mengine ya sayansi na akawaonyesha.

Kikao hakikuendelea.

Mkurugenzi akamwambia Afisa Elimu akarekebishe hilo tatizo."
 
Mzee wetu Mohamed Said, je umetafakari kuandika historia ya Dar es Salaam, kutokana na kumbukumbu zako? Yaweza kuwa hazina kwa wengi.
Suel...
Nimechoka nakimbilia miaka 70.
Kukaa kitako kuandika kunanitisha.

Jamaa zangu wengi wananiwekea shinikizo kuhusu hili.

Nawaambia mkitaka niandike nitafutieni mahali Ulaya au Marekani kwenye chuo.
 
JUMBA LA USHIRIKA UKILITAZAMA KUTOKA MTAA WA LIVINGSTONE 1960s

Nikiangalia hii picha inanikumbusha mbali mwaka wa 1964
Simulizi nzuri sana, ila nime zoom picha, sijaziona ngazi.

Je, jengo halikuwa na uzio hadi nyie watoto wa Uswahilini mlifanye playing ground?

Halafu watoto wa Kiswahili lazi.a wachafue jengo ndio waone raha. Huku kaka na dada zao wakiligeuza sehemu ya kukutana kimwili
 
Simulizi nzuri sana, ila nime zoom picha, sijaziona ngazi.
Je jengo halikuwa na uzio hadi nyie watoto wa Uswahilini mlifanye playing ground?
Halafu watoto wa Kiswahili lazi.a wachafue jengo ndio waone raha. Huku kaka na dada zao wakiligeuza sehemu ya kukutana kimwili
Jem...
Angalia kulia pembeni kuna ngazi.

Nakupa pole mama yangu kwa akili yako kukufikisha huko ulikofika.

Sisi tulilelewa.
Allah awalipe kila la kheri wazee wetu.

Kulikuwa na lango kuu na askari katika jengo.

Hili jengo lilikuwa kama "show piece,'' watu wakiruhusiwa kupanda ngazi hizi kutazama uzuri wa jengo hili.

Kwa wakati ule hapakuwa na mfanowe labda Kilimanjaro Hotel.
 
Nawaambia mkitaka niandike nitafutieni mahali Ulaya au Marekani kwenye chuo.
Kwanini siyo Arabuni sheikh?

Anyway, ilikuwaje Nyerere akaandika barua kwa unyenyekevu kwenda kwa Bi. Mruguru kumwomba nyumba yake ibomolewe na kumlipa fidia wakati angekubomoa tena kwa ukali nyumba ya huyu Ustaadhat bila fidia yoyote.

Huyu mchonga siku hiyo alipatwa na Nini sheikh 😀
 
JUMBA LA USHIRIKA UKILITAZAMA KUTOKA MTAA WA LIVINGSTONE 1960s

Nikiangalia hii picha inanikumbusha mbali mwaka wa 1964...
Ni kweli kabisa jumba hilo lilikuwa la benki ya Ushirika. Vile vile tuongezee kwamba hapo ndipo Chuo Kikuu cha DSM kilipoanzia mwaka 1961 kikiwa na Kitivo kimoja tu cha Sheria.

Watu kama Prof. Shivji na Prof. Kanywanyi ndipo walipoanzia kusomea. Ujenzi wa Chuo ulipokamilika huko Ubungo (Mlimani) ndipo Chuo Kikuu kikahamia huko.

Baada ya Chuo Kikuu kuhama, jumba hilo lilitumika pia kwa elimu ya watu wazima. Nawafahamu watu kadhaa ambao hawakufika Darasa la 12 katika shule za kawaida. Watu kama hao walikuwa wakienda kujiendeleza hapo hadi kufanya mtihani wa Darasa la 12.
 
Jem...
Angalia kulia pembeni kuna ngazi.

Nakupa pole mama yangu kwa akili yako kukufikisha huko ulikofika.
...
Kwenye picha hii ngazi zimeonekana kwa uzuri sana.
1644244728663.png

Sasa hiki kizazi cha kunajisi majengo ya watu kwa haja kubwa na ndogo kilitokea wapi?
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Maneno meeeeeeeeeeeeeeeengi
Wa kupuliza,
Vipi kuhusu hayo hapo chini?

Professor mmoja wa UDOM aliyekua VC alipata malalamiko kuhusu baadhi ya watu kutotendewa haki kwenye ''admission.''

Wakati huo TCU ilikua haijaundwa.

Alipoamua kuitisha ''applications'' zote akakutana na maajabu.

Kuna zaidi ya ''applicants'' 350 walikua wameachwa huku wakiwa wame ''qualify'' huku kukiwa na idadi ya kutosha kabisa wakiwa wamepata ''admission'' wengine wakiwa ''below cut-off point'' ya chuo.

Kwa “sudfa” au ''coincidence'' wote waliokua wameachwa kwa dhulma walikua na majina ya Kiislamu na wote walioku ''admitted'' walikua na majina ya Kikristo.

VC akatoa ''order'' mchakato urudiwe tena japo jambo hilo lilikua ''down played.''

Miaka ya karibuni kulikua na zoezi la kuwaondoa waalimu wa masomo ya arts sekondari waajiriwa wa serikali kuwarudisha shule za msingi. Zoezi husika halikuwahusu waalimu wa masomo ya sayansi na hesabu

Nilikua mkoa fulani kipindi zoezi hili linaendelea.

Kukatokea malalamiko kua zoezi hilo lina sura ya ubaguzi na waathirika ni Waislamu.

Ofisa mmoja Muislamu katika idara ya elimu ambaye hapo awali alikua amejaribu kuomba uhamisho kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya miaka miwili bila mafanikio alipokea malalamiko hayo na baada ya kujiridhisha ni ''genuine'' akayapeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.

Kikaitwa kikao kati ya Mkurugenzi, Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma, Ofisa Utumishi na yule ofisa aliyeipeleka ''issue'' kwa Mkurugenzi.

Wahusika wote kasoro yule aliyepeleka malalamiko walikua Wakristo na ilivyoonekana baada ya kikao kuanza ni kutaka kum ''pin'' huyo ofisa kwa nini analeta udini kwenye utendaji wa kazi za Halmashauri na hususan hilo zoezi la kitaifa.

Walianza kumpa maneno makali kabda hata hawajamuuliza kuhusu ushahidi.

Walipomuuliza atoe ushahidi wa madai yake akaoonyesha majina wa wahusika waliohamishwa.

Shule ina waalimu 68 kati yao Waislamu 18.

Waalimu wanaotakiwa kupelekwa primary schools ni 21.

Basi wakaondolewa wale wote 18 wenye majina ya Kiislamu na hao wengine 3 wasiokua Waislamu.

Kikao bado kikasema huo sio ushahidi maana Mkuu wa Kituo (Headmaster) ana ''discretion'' ya kuchagua mradi anafata ''secular'' iliyotolewa na Wizara (TAMISEMI).

Ndipo akaangusha bomu la ''Atomic'' ambalo alikua hajawaambia ''before.

Kwamba katika wale waalimu Waislamu 18 watatu ni wa Mathematics na sita ni wa masomo mengine ya sayansi na akawaonyesha.

Kikao hakikuendelea.

Mkurugenzi akamwambia Afisa Elimu akarekebishe hilo tatizo.
 
Kwanini siyo Arabuni sheikh?

Anyway, ilikuwaje Nyerere akaandika barua kwa unyenyekevu kwenda kwa Bi. Mruguru kumwomba nyumba yake ibomolewe na kumlipa fidia wakati angekubomoa tena kwa ukali nyumba ya huyu Ustaadhat bila fidia yoyote.

Huyu mchonga siku hiyo alipatwa na Nini sheikh [emoji3]
Mkaruka,
Nimesoma Uingereza.

Nimekuwa Visiting Scholar Marekani na Ujerumani.

Kwa ajili hii nakufahamu zaidi kuliko ninavyokujua Arabuni.

Zaidi kwa kutafiti na kuandika chuo kama SOAS au Northwestern University kuna Maktaba kubwa sana kuhusu Afrika.

Mwalimu alifanya hivi kwa ajili ya hisani iliyokuwapo baina yake na Bi. Mruguru.

Abdul Sykes ndiye aliyempokea Nyerere alipofikia Dar es Salaam 1952 na ndiye aliyemtia katika siasa za Dar es Salaam.

Kupita Abdul mama yake Mwalimu Bi. Mugaya akafahamiana na Bi. Mruguru na wakawa mashoga wakubwa.

Nyerere akimchukulia Bi. Mruguru kama mama yake.
View attachment 2111499
 
Tuweke ushahidi khs Hilo ulilolisema maana mtu yoyote anaweza kuandika hayo uliyo yaandika.
Wa kupuliza,
Unakuja ukiwa na adabu kamili na kuuliza swali kama itakiwavyo.

Nini kimekubadili ghafla?
 
Ni kweli kabisa jumba hilo lilikuwa la benki ya Ushirika. Vile vile tuongezee kwamba hapo ndipo Chuo Kikuu cha DSM kilipoanzia mwaka 1961 kikiwa na Kitivo kimoja tu cha Sheria. Watu kama Prof. Shivji na Prof. Kanywanyi ndipo walipoanzia kusomea. Ujenzi wa Chuo ulipokamilika huko Ubungo (Mlimani) ndipo Chuo Kikuu kikahamia huko. Baada ya Chuo Kikuu kuhama, jumba hilo lilitumika pia kwa elimu ya watu wazima. Nawafahamu watu kadhaa ambao hawakufika Darasa la 12 katika shule za kawaida. Watu kama hao walikuwa wakienda kujiendeleza hapo hadi kufanya mtihani wa Darasa la 12.
Ng'w...
Unachanganya Jengo la Ushirika na Jengo la Chuo Cha Watu Wazima

Chuo Kikuu kilianza Chuo Cha Watu Wazima.

Haya majengo yako jirani.
 
Back
Top Bottom