Jumba la Ushirika 1964


Nadhani hapa umechaganya mambo!! Hilo jumba la ghorofa la ushirika sio mahala Faculty of Law ya UDSM ilipoanzia!! Jengo lilpoanzia Faculty of Law ni hilo jengo ambapo baadae lilikuja kutumiwa na SUKITA mtaa huo huo wa Lumumba!!
Sio Sahihi Kuwa Prof. Shivji alisoma pale; cohort ya shivji ni wakina Prof. Fimbo , marehemu Majaji Mwalusanya , Nsekela.etc wao walianzia masomo yao main campus! Walionza pale Lumumba ni Julie Manning, Kileo Arnold, Marehemu Bakilana na wengine.
 
Ninyi si mko bize na Elimu ya Ahera Shekhe?. Mtoto wa shule ya msingi unamkalilisha Kuluhani na wakati huohuo unataka awe na msingi mzuri wa Elimu dunia, haiwezekani maana mshika mawili moja humponyoka.Asalam aleikhum Shekhe [emoji41][emoji41]
 
Hapo mzee mwenzangu! UDOM ilianzishwa na Kikwete! Kikwete aliikuta TCU
 
Haya mzee wetu......
Lakini nashukuru kuwa you got my mesaage though unajitahidi kuwa evasive
Lib,
Swali lako ni hili:
''mzee wetu kwa nini unapenda Marekani au Ulaya badala ya Saudi Arabia au Iran, Oman?''

Jibu langu ni hili:
''Nimesoma Uingereza.
Nimekuwa Visiting Scholar Marekani na Ujerumani.

Kwa ajili hii nakufahamu zaidi Ulaya kuliko ninavyokujua Arabuni.

Zaidi kwa kutafiti na kuandika chuo kama SOAS au Northwestern University kuna Maktaba kubwa sana kuhusu Afrika.''

Chuo gani utakwenda Arabuni ambacho kinaweza kushindana na SOAS au Northwestern University katika utafiti wa Afrika?

Hata American University, Cairo au popote pale Arabuni haiwezi kufikia vyuo hivyo hapo juu.
Kwa kawaida wanafunzi huenda kwenye vyuo vinavyosomesha yale wanayotaka kusoma.

Ikiwa unauliza swali na jibu lako unalo mwenyewe na hili jibu lisipotolewa bila shaka hutaridhika.

Hii ndiyo hali kwa bahati mbaya iliyokufika.
 
Uwe na siku njema mzee wetu.....
Baniani mbaya kiatu chake dawa
 
Ninyi si mko bize na Elimu ya Ahera Shekhe?. Mtoto wa shule ya msingi unamkalilisha Kuluhani na wakati huohuo unataka awe na msingi mzuri wa Elimu dunia, haiwezekani maana mshika mawili moja humponyoka.Asalam aleikhum Shekhe [emoji41][emoji41]
Fall...
''Qur'an.''
''Karirisha.''
''Aleikum.''
''Sheikh.''

Mimi si ''sheikh.''
Ningependa kuwa lakini sikujaaliwa elimu hiyo.

Hapa JF nimepata kuwa na mjadala na watu waliokuwa wanashkilia kuniita ''Ustadh,'' ''Mufti,'' nk.

Nimepata tabu sana kuwafahamisha.

Naomba ruhusa yako nitumie neno, ''ujinga.''

Kuna ujinga mkubwa sana nchi petu kuhusu chochote kile kinachogusa Uislam na Waislam.

Bahati mbaya wengi hamjui na hamjui kuwa hamjui na hata mnapo elezwa ukweli wa jambo lenyewe hamtaki kusikiliza na kujifunza.

Kuhifadhi Qur'an yaani ''tahfidh,'' haijakuwa kushika mawili wala haijakuwa kikwazo cha mtoto kufanya vyema shule.

Kinyume chake ni kuwa huo ni msingi mkubwa sana wa watoto kuelewa masomo yao na katika upande wa kujifunza lugha inawapa nguvu sana.

Nakueleza haya kwa kuwa ninao katika nyumba yangu mahafidh Qur'an wengine wameshahitimu na wengine ni wanafunzi bado.

Hawa watoto hawajaniangusha.
Tatizo katika elimu ya Waislam ni kitu kingine kabisa.

Nisingependa tuanze upya mjadala huu lakini ikiwa wewe ni mwenyeji hapa utakuwa umenisoma.
 
Uwe na siku njema mzee wetu.....
Baniani mbaya kiatu chake dawa
Lib...
Ikiwa unakusudia kuwa mimi naiona Ulaya na Marekani ni wabaya wangu utakuwa umekosea sana.

Nimekuwa na uhusiano mwema na nchi hizo toka ujana wangu nikiingia na kutoka bila shida yeyote.

Napenda kukufahamisha kuwa kitabu changu cha kwanza kuandika, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' kilichapwa London mwaka wa 1998.

Review ya kitabu kimefanywa na wasomi watatu wawili kutoka Marekani na mmoja Uingereza na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History.

Nimepata pia kualikwa na hawa Wazungu kwenye vyuo vyao kuzungumza na pia kufanya utafiti.

Je, hawa Wazungu waliochapa kitabu changu na kunialika katika vyuo vyao na wao pia unaweza kuwaambia kuwa Baniani mbaya...?
 
Mzee wetu licha ya kwamba kuna mambo huwa natofautiana nawe (naamini haya ndiyo maumbile ya kibinadamu, kutokubaliana katik kila kitu).
Naomba unisaidie machapisho/ vitabu gani nivisome nipate unbiased narrations of Zanzibar Revolution?
 
Kolola,
Yawezekana kuwa ilikuwa haijaundwa.
Vipi kuhusu hizo taarifa nyingine?
The Tanzania Commission for Universities succeeded the former Higher Education Accreditation Council (HEAC) which was established in 1995 under the Education Act 1995 with a legal mandate to regulate the establishment and subsequent accreditation of private university institutions in the country. Being limited only to private universities, such mandate was considered unfavourable for the promotion of a viable public-private partnership in higher education as stipulated in the National Higher Education Policy of 1999.
Nimeitoa: https://www.tcu.go.tz/?q=node/2

The University of Dodoma was formally established in March 2007 following the signing of the Charter by the President of the United Republic of Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. The first academic programmes commenced September 2007.

Imepatikana: University of Dodoma - Wikipedia

Hivyo haiwezekani usajili Wanafunzi wa UDOM uwe Kabona ya TCU. Hizi ni stori mnazopata vijiweni wakati mnakunywa Ghahawa pale Saigoni. Zipuuze
 
Mzee wetu licha ya kwamba kuna mambo huwa natofautiana nawe (naamini haya ndiyo maumbile ya kibinadamu, kutokubaliana katik kila kitu).
Naomba unisaidie machapisho/ vitabu gani nivisome nipate unbiased narrations of Zanzibar Revolution?
Lib...
''Un biased.''

Hili nitakuachia wewe mwenyewe usome hiki kitabu na utaamua ukweli wake ukifananisha na vitabu vya waandishi wengine.

Nilikuwa ''Research Assistant,'' yaani Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' (2010).

Soma kitabu hiki na kinapatika mtandaoni.
Nimekuwekea na picha yangu iliyo kitabuni nikiwa Kipumbwi wakati wa utafiti.

View attachment 2112189
 
Kolola,
Umenifahamisha kuhusu TCU na mimi nimekujibu kiungwana.

Siku zote binadamu tutafanya makosa ya hiki na kile na unapoelezwa ukweli unaukubali ule kweli.

Umeleta taarifa nzuri na huyo aliyetoa taarifa hizi yuko hapa ataona jibu lako.
Bahati mbaya umehitimisha kwa matusi.

Saigon Club haihusiani hata kwa mbali na haya tunayojadili hapa.
Ama kupuuza ni kitu kingine.

Ndipo nilipokuuliza vipi kuhusu hizo taarifa nyingine?
 
Asante sana
 
Asante kwa ufafanuzi.
 
Kitendo cha wewe na heshima zako kuamini stori za vijiweni kama hizi, kinasikitisha sana. Baadaye unatumia stories hizi hizi kama rejea yako katika maandiko yako ya kichochezi huku ukisingizia kuwa unaandika kurekebisha historia. Unanisikitisha kwa kweli.
 
Acha uongo. Maelezo yote uliyosema si sahihi.
Crdb ilianzishwa baadaye. Baada ya jengo hilo kujengwa. Hakukuwa na uhusiano wa moja kwa moja kati ya Coperative and Rural Development Bank (cedb baadaye) na Ushirika waliokuwa wamiliki wa jengo.
Chuo Kikuu kilianzishwa kwenye jengo la TANU lililopo pembeni ya jengo la Ushirika.
 
Nan...
Hizi hazijapata kuwa stori za kijiweni hata siku moja.

Ni taarifa zenye ushahidi kamili.

Lakini ikiwa wewe utataka kuamini kuwa huu ni uongo hakuna ukweli hiyo ni juu yako sikulazimishi kuamini.

Viongozi wetu ambao taarifa hizi wanakusudiwa wao wanazisoma na kubakia kimya wanajua ukweli wa kila kitu.

Hakuna kiongozi asiyejua historia ya Waislam kuwa walitaka kujenga Chuo Kikuu mradi ukahujumiwa.

Kisa chote kinafahamika.

Hakuna kiongozi asiyejua yaliyokuwa yanatendeka Wizara ya Elimu nk.nk.

Hili si jambo jepesi kwao kulizungumza hadharani.

Na hii hulka ya ghadhabu na matusi ni njia mojawapo ya kushindwa kuwa na majibu.

Wala husikitishwi na kalamu yangu.

Maana ungekuwa unasikitika ungekuwa muungwana katika kauli zako.

Kalamu yangu inashtua.

Kalamu yangu inakusomesha yale ambayo hukupatapo hata siku moja kuyasikia.

Hii ndiyo sababu hukosekani ninapokuwapo kwani hupendi kupitwa na darsa zangu.

Mjadala mzito kama huu una njia mbili.
Kutoa majibu au kubakia kimya.

Haiwi kejeli, kebehi na matusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…