Ni kweli kabisa jumba hilo lilikuwa la benki ya Ushirika. Vile vile tuongezee kwamba hapo ndipo Chuo Kikuu cha DSM kilipoanzia mwaka 1961 kikiwa na Kitivo kimoja tu cha Sheria. Watu kama Prof. Shivji na Prof. Kanywanyi ndipo walipoanzia kusomea. Ujenzi wa Chuo ulipokamilika huko Ubungo (Mlimani) ndipo Chuo Kikuu kikahamia huko. Baada ya Chuo Kikuu kuhama, jumba hilo lilitumika pia kwa elimu ya watu wazima. Nawafahamu watu kadhaa ambao hawakufika Darasa la 12 katika shule za kawaida. Watu kama hao walikuwa wakienda kujiendeleza hapo hadi kufanya mtihani wa Darasa la 12.

Nadhani hapa umechaganya mambo!! Hilo jumba la ghorofa la ushirika sio mahala Faculty of Law ya UDSM ilipoanzia!! Jengo lilpoanzia Faculty of Law ni hilo jengo ambapo baadae lilikuja kutumiwa na SUKITA mtaa huo huo wa Lumumba!!
Sio Sahihi Kuwa Prof. Shivji alisoma pale; cohort ya shivji ni wakina Prof. Fimbo , marehemu Majaji Mwalusanya , Nsekela.etc wao walianzia masomo yao main campus! Walionza pale Lumumba ni Julie Manning, Kileo Arnold, Marehemu Bakilana na wengine.