Kolola,
Yawezekana kuwa ilikuwa haijaundwa.
Vipi kuhusu hizo taarifa nyingine?
Sheikh Mohamed,
Naomba nami nikusaidie kidogo katika hili
Wakati huo hata kama TCU ilikuwepo lakini hapakua na utaratibu wa Central Admission unaofanywa sasa hivi na TCU ambapo unaweza ukachagua course fulani chuo fulani ukajikuta umepelekwa pengine
Wanafunzi walikua wakifanya applications zao moja kwa moja vyuoni, na vyuo ndio vikifanya admission kulingana na requirements na criteria zao
Na kwa taarifa tu ni kwamba tukio hilo la UDOM liliogunduliwa na VC wao ni miongoni mwa sababu zilizotumika kujenda hoja ili Chuo Kikuu Cha Waislam Morogoro (MUM) kikubaliwe kutoingizwa katika mfumo wa udahili wa TCU!
MUM ndio chuo pekee cha elimu ya juu kinachoruhusiwa kufanya udahili wake bila kupitia TCU(I stand to be corrected)
Baada ya kadhia ile ya Admission ya UDOM, ambayo hakika haikusikika kwa jinsi ilivyokua “systematically down played” na ulipoanzishwa mfumo wa central admission ikapelekwa hoja TCU na Serikalini kuomba MUM iwe exempeted na utaratibu huo
Hoja ikawa kwamba; Kwenye vyuo vya Umma (Serikali) uwiano wa wanaodahiliwa kati ya Waislamu na Wakristo ni 20:80
Vyuo Vya Elimu ya Juu vya Binafsi na Vya Mashirika ya Dini zaidi ya asilimia 90 vinamilikiwa na Taasisi za Kikristo, ambapo uwiano wa udahili wa wanafunzi kati ya Waislamu na Wakristo ni 15:85
Sasa kwa kuruhusu MUM nayo iingie kwenye udahili wa wanafunzi kupitia TCU kunaweza kuendeleza sura hiyo ya kuwanyima nafasi wanafunzi wa kiislamu kama huko kwengine. Ikahofiwa kupangwa wanafunzi kwa uwiano uleule unaokalamikiwa siku zote
Pia malengo ya IDF(Islamic Development Foundtion) ya kuanzisha MUM ili kuondoa upogo(kutokua na usawa) uliopo wa vijana wa Kiislamu kupata fursa sawa za elimu ya juu yasingetimia kama hili likiruhusiwa
TCU inatoa vigezo tu vya requirements za admission kwenye courses za certificate, diploma, undergraduate degrees, Masters etc.
Hakika hapakua na hoja kinzani maana takwimu zote zipo hadharani tena takwimu rasmi kabisaa!! Likapitishwa kwa haraka sana katika ile Waswahili wanasama “Funika kombe…….”
Surprisingly, Muslim University of Morogoro (MUM) kinapata applications za wanafunzi wengi sana wenye sifa za kusoma Higher Learning Institution yoyote duniani ambao hawaonekani katika vyuo vingine hasa vya Umma!!!!!!?
Jambo hili la kunyima watu fursa kwa hila katika nchi yao ingekua ni kinyume chake kwamba hao wanaosemwa kudhulumu haki na fursa za wengine ndio wanaofanyiwa mbona pangewaka moto!