Jumbe Tambaza: Alimsomea Nyerere dua nyota yake ikang'ara

Jumbe Tambaza: Alimsomea Nyerere dua nyota yake ikang'ara

ACHA NA MIMI NIFUTE WATU TONGOTONGO KIDOGO KISHA MWISHONI NITAZUNGUMZA KUHUSU HIZO DUA AZLIOFANYIWA HAYATI MWL J.K NYERERE

Maisha yamegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
1. Ulimwengu wa roho
apa namaanisha ulimwengu usionekana kwa macho ya kawaida, hapa ndipo tuaminipo ktk Mungu na Ibilisi.
2. Ulimwengu wa nyama
ulimwengu ni katika vitu vyote ambavyo tunaviona kwa macho yetu ya kawaida.
Nianze kusema kuwa, Taifa la Tanzania limefika hapa lilipo kutokana na makosa yaliyofanywa na waasisi wa hili Taifa na wale ambao wapo pia madarakani ila sana sana ni waasisi, kwanini? kwasababu muasisi wa taifa ama waasisi wa taifa ni LANGO la taifa.

Lango ni nini? Katika tafsiri ya kawaida lango ama mlango ni sehemu inayopitisha kitu ili kuingia ndani, kama tunaona katika ulimwengu wa nyama kuwa ipo mipaka ya nchi ambayo mtu, wanyama n.k huingia ndani ya nchi husika, vivyo hivyo ipo milango ama lango katika ulimwengu wa roho ambao unapitisha mambo ya rohoni ndani ya nchi.

NOTE: Chochote ukionacho katika ulimwengu wa macho ya nyama, tambua kimeanzia rohoni. Hata katika uumbaji Mungu alianza kumuumba mwanamke na mwanaume ktk ulimwengu wa roho kisha ikaja kudhihirika ktk ulimwengu wa nyama.

Mnamo mwaka 1961, baada ya Waingereza kuiachia Tanganyika, waasisi wa hili Taifa wakiongozwa na Nyerere walitegemea saana ama niseme ni waamini wa ulimwengu wa roho ktk ufalme wa giza, hivyo walienda kwa wachawi wa nchi ama waganga ili kupata maarifa na akili ya kuiongoza nchi.

Moja ya vitu ambavyo vilitokea kwao ni kutopata tu maarifa na akili bali pia walitakiwa wakubali wachawi mazindiko ndani ya nchi, chama cha siasa TANU ambacho sasa hivi ni CCM kuzindikwa ama kuongozwa na serikali ama tawala za kuzimu Tanzania.

Nisizungumze mengi, nikatishe kwa kusema kuwa Mwl Nyerere kama kiongozi wa nchi ama muasisi wa Taifa hili, ndie alikuwa lango la kupitisha falme za giza ndani ya nchi ya Tanzania ambapo hata yeye mwenyewe hakujua kama haya anapitisha haya mambo ambayo yaliicost Tanzania kipindi kile na hata sasa. Hayati Baba wa Taifa angejua kama kupitia yeye anapitisha haya mambo wala asingekubali na kama angekuwa na nguvu ya kujinasua angefanya hivyo ila kwa bahati mbaya hakuwa nayo.

TURUDI KWEYE MADA
Dua alizosomewa Hayati JK Nyerere ndizo tunazoita ushirikina sana sana katika kusafisha Nyota, kwanini?
Mungu anapomuumba mwanadamu huwa anamuumba kwa jinsi yake nikimaanisha vinasaba, mtazamo, akili, nyota, hekima, maarifa n.k ila viongozi wengi wa nchi huwa wanapewa akili ya ziada na kupandikiziwa nyota ambazo sio za kwao. Wachawi/Waganga wana uwezo wa kutambua nyota ya mtu tangu akiwa mtoto na wana uwezo wa kutoa nyota yako na kumhamishia mtu mwingine, sio nyota tu bali hata nafsi na mengineyo.

Hayati Baba wa Taifa ni moja ya viongozi waliveshwa nyota ambazo hazikuwa ni za kwao, hizo nyota wachawi/waganga wanazimiliki sana huko kuzimu.

Embu jaribu kutafakari, endapo kweli Mwalimu Nyerere alikuwa na vinasaba vya uongozi, je katika watoto wote aliokuwa nao hakuna hata mmoja ambae ana vinasaba vya baba yake? HAKUNA, endapo uongozi wake ile hekima na maarifa na nyota yake alipewa na Mungu katika uongozi basi kati ya watoto wake wote alokuwa nao yupo mmoja walau angekuwa na characters kutoka kwa baba yake.

Watanzania tusiwasifu sana hawa wasomaji dua hususani wanaojiita wazee wa Dar es Salaam, ni washirikina wakubwa mno, maisha tunayoishi leo Watanzania ni matokeo ya maagano ya kuzimu na watawala wetu ndio maana leo hii akili za watanzania zimefungwa kutokana na yale mazindiko. Mtawala anaweza akafanya chochote na watanzania wasichukue hatua, UFISADI, WANYAMAPORI, DEMOKRASIA N.K watanzania tunalalamika kwa muda ila watawala kupitia wachawi wa nchi wanazima akili za watanzania na hawahoji tena wala hawakumbuki.

kwa leo nitaishia hapa ila ipo siku nitaandika kwa mapana mno kuhusu haya mambo, kwa wale msionielewa mnisamehe, sina kipawa cha kufindisha na haya nimeyaandika ghafla ila ipo siku nitayaandika kwa mpangilio mzuri kabisa.
 
nakubaliana na wewe mkuu kwa fact kwamba Waislamu/Wakristo walei wanaweza kujichanganya bila kuulizwa maswali lakini si viongozi (sheikhs, wachungaji, etc). huu ndiyo muktadha wa swali langu kwa sheikh Mo Said.
Ndugu zangu,
Katika hizi dua na matambiko kwanza napenda nikufahamisheni kuwa
Nyerere si wa kwanza kufanyiwa hizi dua.

Wakati nafanya utafiti katika kuandika kitabu cha Abdul Sykes kwa
mara ya kwanza nilikutana na dua katika kisa cha ugomvi baina ya
Abdul Sykes na Mzungu aliyekuwa ''boss,'' wake aliyevamia ofisi yake
ya Market Master Kariakoo Market akamkuta Abdul anauza kadi za
TANU na nyingine anazo katika mtoto wa meza.

Wafanya biashara pale sokoni kwa kuhofia kuwa Abdul atafukuzwa
kazi waliamua kufanya dua.

Nimeelezwa kila kitu nini kilifanyika katika dua na katika makubwa
zaidi na nini yalikuwa matokeo yake.

Inatisha.
Hii ilikuwa 1955.

Sikuweza kukiandika kisa kile katika kitabu na siwezi leo kukihadithia
hapa.

Abdul hakufukuzwa kazi ila aliyepata shida ni Mzungu na TANU ikazidi
kuimarika na Abdul kaendelea kuuza kadi zake za TANU sokoni Kariakoo.

Dua nyingine ilikuwa ya Rashid Ali Meli aliyetoa fedha katika sefu yake
kazini akiwa Mtunza Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council akampa
Idd Faiz Mafungo itiwe kwenye mfuko wa safari ya Nyerere UNO 1955.

Wakaguzi walifika siku ya pili kufanya ukaguzi na ikawa hatari Rashid Ali
Meli
atafungwa kwa ''wizi.''

Walipofungua sefu fedha walizikuta zote kamili hakuna hata senti moja
iliyopotea.

Special Branch walikuwa wametoa taarifa zisizo shaka walizopewa na mtu
wao ndani ya TANU tena kiongozi wa juu kabisa.

Dua nyingine 1956 iliyofanywa Lindi na Sheikh Yusuf Badi Nyerere
akiwapo.

Tabu kuamini yaliyotokea usiku ule.
Sijaweza pia kuandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Dua ilifanyika nyumbani kwa Suleiman Masoud Mnonji Mtaa wa Makonde.
Hii ilikuwa 1956

Dua nyingine ni ya Mnyanjani kuhusu Kura Tatu mwaka wa 1958.
Sishangai kuwa leo watu wanatatazika na historia hii.
 
Mohamed Said,
shukurani sheikh Said kwa kutushirikisha historia hii iliyotukuka.

katika ufafanuzi, umeegemea zaidi upande wa dua - upande huu sina matatizo nao kwani siku zote ninaamini kuwa Mungu (Allah) ndiye muweza katika yote.

tatizo langu lipo kwa viongozi wa dini kuchanganya dua kwa Allah na matambiko kwa miungu wakati wakimuombea Mwalimu JKN.
hili bado hujalijibu sheikh.

wasi wasi wangu, genuinely speaking, ni nini?

kwa miaka nenda rudi nchi yetu iliyosheheni neema kubwa ya mali asili imekuwa ikipiga mark time kiuchumi. wasi wasi ni kuwa isijekuwa Mungu (Allah) labda alituachia laana kupitia Mwalimu baada ya viongozi wetu wa dini ku blend ibada za Mwenyezi Mungu na yale matambiko ya miungu.
 
M-mbabe,
M Mbabe,
Wa kujibu hayo si mimi kwani mimi si niliyefanya hayo.

Mimi kama mwanahistoria nimeeleza yale niliyoyakuta
katika historia ya TANU.

Hayo niliyoweka katika kitabu cha Abdul Sykes ni madogo
sana.

Kipande hiki kinatisha na ndiyo sikuweza kuwa na ujasiri
wa kuyaandika yote niliyoelezwa.

Lakini nitakufahamisha kitu hawa wote waliofanya haya
wakiamini kuwa walikuwa sawa.
 
sawa. nimekusoma sheikh.

nirudi kwako wewe binafsi....

ninaamini wewe ni muumini mzuri wa Uislamu.
swali langu kwako - jee, unaona walichofanya ma sheikh wetu kuchanganya ibada (Mungu vs miungu) ni sawa au si sawa from Islam doctrine perspective?
 
Shajara ya Mwana Mzizima
Jumbe Muhammad Tambaza

Alimsomea Dua Nyerere, Nyota Yake Ikang’ara
Na Alhaji Abdallah Tambaza

Jumbe Muhammad Tambaza

JUMBE Muhammad Tambaza, ni mmoja katika wapigania uhuru mashuhuri wa nchi hii ambao, historia inawataja kama ni watu waliotoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kumng’oa Mkoloni Mwingereza, katika ardhi yetu tukufu.

Hayati Mzee Tambaza, ambaye alifariki mnamo mwaka 1978 hivi, anaingizwa katika kundi moja la watu wa mwanzo kabisa waliompokea kwa furaha na upendo kijana Julius Nyerere kutoka Butiama, alipofika jijini Dar es Salaam kwa kumuunga mkono ‘mia kwa mia’, katika harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika kwenye miaka ya 1950s.

Wanaharakati wengine aliokuwa nao ni pamoja na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi wa Mwananyamala; Mzee John Rupia wa Mission Quarters; Sheikh Suleiman Takadir; Sheikh Haidar Mwinyimvua (Kisutu); Mzee Max Mbwana (Kariakoo); Zubeir Mwinshehe Mtemvu (Gerezani) pamoja na familia ya Mzee Azizi Ali (Mtoni) na ile ya Kleist Sykes (Gerezani), Dar es Salaam.

Ukoo wa Diwan Tambaza Zarara bin Mwinyi-Kitembe, ndio waliokuwa wenyeji wa maeneo ya katikati ya jiji wakati huo, wakihodhi eneo la ardhi yote ya Upanga, iliyosambaa kuanzia Daraja la Selender kuelekea Palm Beach Hotel, hadi Ikulu ya Magogoni kwa upande mmoja; na kwa upande mwengine maeneo yote kutoka Aga Khan Hospital, Ocean Road Hospital, Kivukoni Front (makaburi ya asili ya wanandugu wengine yako pale Wizara ya Utumishi, Magogoni) kwenda Mnara wa Saa pale Uhuru Street na vilivyomo ndani yake.

Habari zinasema kwamba, katika siku za mwanzo tu za kupambana na Mwingereza, wazee mashuhuri wa hapa Dar es Salaam walikutana na kuamua kumfanyia ‘zindiko’ na ‘tambiko’ la kijadi, pamoja na kumwombea dua maalumu kijana mdogo, Julius Nyerere, ili kumkinga na waovu na pia kuifanya nyota yake ing’are juu ya wote wenye nia mbaya naye; wakiwamo watawala wa Kiingereza, hasa Gavana Twinning.

Katika moja ya hotuba zake za kuaga aliyoitoa mnamo Novemba 5, 1985, Nyerere alilikumbumbuka tukio hilo na hapa chini anasimulia:

“…Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania…na mambo makubwa kama haya kama hayana baraka za wazee hayaendi… huwa magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani; tangu awali kabisa.

“Sasa siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (nyumbani kwake) akasema: ‘Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.”

Anahadithia Mwalimu na kuendelea:

“Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika… zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee… za jadi, “…walikuwa na beberu la mbuzi… wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama beberu akachinjwa huku anaambiwa Twinning ‘umekwisha’… nikaambiwa tambuka… nikavuka lile shimo na baada ya hapo nikaambiwa …basi nenda zako kuanzia leo Twinning amekwisha!”

Mwalimu alimaliza kusimulia namna alivyofanyiwa dua na tambiko nyumbani kwa Mzee Tambaza, Upanga jijini.

(Picha ya Baraza la Wazee wa TANU kutoka kitabu cha Saadan Abdu Kandoro, ''Wito wa Uhuru'')

Kutawaliwa na Wazungu kuliwakera na kuwakasirisha watu wengi sana, kutokana na kule kudharauliwa ndani ya nchi yao wenyewe na watu wengine; hasa pale walipominywa katika kupatiwa huduma muhimu kama elimu bora, matibabu na mahala pazuri pa kuishi.

Pamoja na mambo mengi mengine yaliyokuwa mabaya kutokana na kutawaliwa, yamo pia na yale ya kuwekwa kwa madaraja katika utoaji huduma muhimu. Sisi, wana wa nchi hii, hatukuwa na shule za maana hata kidogo; watu wote sisi tukasomee shule moja tu (Mchikichini) mpaka darasa la nne; kwa nini hasa kama siyo dharau?

Nyumba zetu za kukaa zilikuwa za ovyo zilijengwa kwa miti na kukandikwa udongo na juu ni makuti, tena hapa hapa mjini Dar es Salaam, sikwambii vijijini; umeme uko kwenye taa za barabarani na siyo majumbani mwetu. Tukiwasha vibatari na taa za ‘chemli za Aladin’ kwa wenye uwezo kidogo kila siku.

Hospitali ziliishia kutoa kama huduma fulani ya mwanzo tu (First Aid). Haikuwapo hospitali ya Amana, Temeke, Mnazi Mmoja, Mwananyamala wala Mbagala. Tuliponea kibahatibahati tu kwa mizizi na majani ya porini. Ukiwa na homa kali basi chemsha mwarobaini; tumbo la kuendesha chemsha majani ya mpera au mpapai nani akupe ‘antibiotic wewe’.

Hospitali ya Muhimbili, yenye maabara na vipimo pamoja na madaktari bingwa, ilijengwa mwaka 1957 - ni juzi tu - kwa heshima ya Binti Mfalme Margareth II, aliyekuwa na ziara ya kutembelea makoloni ili aje kufungua rasmi hospitali hiyo. Kiwanja kilitolewa kwa hisani ya familia ya Mzee Jumbe Tambaza, ambapo miembe ile mikubwa inayoonekana mpaka leo pale ilikuwa shambani kwa kina Tambaza.

Kwa hivyo basi, ukiacha labda homa na vidonda, magonjwa mengine yote kwetu ilikuwa ni kifo tu. Umri mkubwa wa kuishi kwa wastani ulikuwa ni miaka 30.

Mzee Jumbe Tambaza, ambaye jina lake linanasibishwa na shule maarufu ya Sekondari ya Tambaza ya jijini - hana uhusiano wowote na shule hiyo - shule ilipewa jina lake kutokana na eneo iliyopo na kwa kuthamini mchango wake katika kupigania uhuru.

Kabla ya hapo, wakati huo wa ubaguzi wa rangi na matabaka, shule hiyo na ile ya msingi iliyo jirani nayo inayoitwa Muhimbili Primary, zilikuwa mahsusi kwa vijana wa Kihindi tu – hasa Ismailia - zikijulikana kama ‘Aga Khan Schools’ na kamwe hawakuwa wakisoma Waswahili na Kiswahili pale.

Shamba la Mzee Jumbe Tambaza pale Upanga, lilianzia mbele kidogo ilipo Shule ya Jangwani Wasichana (ambayo wakati wa ukoloni ilijengwa na serikali wasome watoto wa kike wa Kihindi tu, na ile Shule ya Azania ilikuwa kwa watoto wa Kihindi wa kiume), na kutambaa moja kwa moja mpaka lilipo Daraja la Selender pale baharini.

Eneo la Majengo ya Hospitali ya Muhimbili ilikuwa mali ya Jumbe Tambaza na marehemu nduguze (Msakara, Kudura na Mwamtoro Tambaza). Kutokana na kukosekana kwa hospitali ya maana ya rufaa kwa ajili ya Waafrika (kwa sababu ya ubaguzi tu), hayati Mzee Tambaza alitoa eneo lote lile la Muhimbili ijengwe hospitali ya Waafrika ili kupunguza vifo vilivyotokana na kukosa tiba sahihi.

Kijihospitali kidogo kwa ajili ya watu Weusi kilikuwapo pale jirani na Kituo cha Kati cha Polisi (Central Police Station) jijini, ikiitwa Sewa Haji Hospital, kwa heshima ya mfadhili aliyeijenga kusaidia jamii masikini. Sewa Haji alikuwa mkazi wa Bagamoyo mwenye asili ya Kibulushi kutoka Persia. Baada ya kujengwa hospitali ya Muhimbili, jengo moja katika yale matatu makuu, likaitwa Sewa Haji kama kumbukumbu yake.

Mjini Dar es Salaam wakati huo wa kibaguzibaguzi, serikali ya kikoloni haikutenga sehemu ya kuzikia watu weusi ambao walikuwa daraja la nne. Yale makaburi mashuhuri ya Kisutu, wakati huo yalikuwa ni ya watu wenye asili ya Kiarabu tu! Mwengine yoyote, ilibidi apelekwe kijijini kwao tu nje ya mji – Kunduchi, Mbweni, Msasani, Bagamoyo, Kisarawe, Maneromango na mikoani pia.

Sasa, ili kuondoa adha hiyo na usumbufu, Babu Mzee Tambaza, alitoa bure sehemu kubwa ya eneo lake itumike kwa watu wenye kuwa na shida ya kuzika ndugu zao jijini. Makaburi ya Tambaza siku hizo yalikuwa maarufu sana kuliko yalivyo yale ya Kisutu kwa sasa. Kamwe watu weusi hawakuwa wakizikwa Kisutu, kama ilivyo wakati huu.

Kufuatia hali hiyo, Jumbe Tambaza aliwashawishi binamu zake wawili, Mwinyimkuu Mshindo na Diwan Mwinyi Ndugumbi na wao wakatoa sehemu watu waweze kuzikana kule maeneo ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa na Ndugumbi, Magomeni Makuti; makaburi ambayo mpaka leo yameendelea kutumika kuzikia watu wote.

Neno, ''Tambaza,'' limetokana na neno ''kutambaa,'' au ''kusambaa,'' eneo kubwa. Diwan Tambaza na nduguze walikuwa watawala wa sehemu mbalimbali za hapa Mzizima siku za nyuma kabla Waarabu, Wajerumani wa Wangereza kufika hapa. Nduguze wengine ni Diwan Uweje; Diwan Uzasana; Diwan Mwenye-Kuuchimba na Diwan Mwinyi Ndugumbi.

Majina hayo walijipachika wenyewe kiushindani, kujigamba na kujitukuza kuliko ndugu wengine; hivyo kimafumbo mafumbo, huyu akajiita hivi na yule akamjibu mwenzake vile; mwengine akajiita naye atakavyo, kutokana na uhodari na tawala thabiti walizoziongoza.

Majina hayo pandikizi, hata hivyo yalikuwa na maana yake kila moja; kama vile mtu aseme mimi ‘Mobutu Sese Seku Kuku Mbenju wa Zabanga’, ikiwa na maana ya ushujaa kwa ‘Batu ba Kongo na fasi ya Zairwaa!’

Sasa Diwan Tambaza alipojiita vile, nduguye Diwan Uweje akamjibu na kumwuliza hata ukiwa umesambaa ndio uweje? Mwengine naye akasema, ‘’Ah! Uliza sana wewe uambiwe.’’ Hivyo yeye akajita Diwan Uzasana. Diwan Mwenye-Kuuchimba, yeye alikuwa akitawala maeneo ya Mtoni Kijichi na Mbagala yake, akasema, ‘’Nyie wote mnacheza tu, ‘mimi ndiye mwenye kuuchimba!’’ Kwa maana ya kwamba ndio kiboko ya wote. Ilimradi hali ikawa ndiyo hiyo; na hizo ndio zama zao, kwani husemwa kila zama na kitabu chake.

Mwandishi wa makala haya, jina langu naitwa Abdallah Mohammed Saleh Tambaza. Babu yangu Mzee Saleh bin Abdallah Tambaza wa Zarara, anakuwa binamu wa Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, yaani baba zao walikuwa ndugu.

Shamba la babu yangu mimi pamoja na kaka yake Kidato Tambaza, linasambaa kuanzia Don Bosco, Makao Makuu ya Jeshi, Diamond Jubilee, Msikiti Maamur (kaburi la babu na babake babu yamo ndani ya Msikiti wa Maamur unapoingia mkono wa kulia pale ukutani), kuelekea kwenye Jamat la Wahindi mpaka Mahakamani kule Kisutu.

Miembe, minazi na mizambarau ile ya asili inayoonekana Upanga, ilipandwa na babu yangu kwa ajili ya urithi wa wajukuu zake, itakapofika zamu yao kumiliki maeneo yale.

Kwa bahati mbaya sana, Wazungu Waingereza, wakaona mandhari ile nzuri ya Upanga, hawakustahili watu weusi kuishi pale na wakawaamuru babu zangu wahame wawapishe Wahindi raia daraja pili. Hii ni baada ya wao Wazungu daraja la kwanza kuchukua eneo lote la Oysterbay (sasa Masaki). Maeneo yote hayo mawili yenye upepo mwanana ni karibu kabisa na bahari.

Kitendo cha kumhamisha mtu nyumbani kwake kwa namna ile, halafu kumpa fidia uitakayo wewe, ni dharau, dhuluma na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Wazee wale wastaarabu na wajanja hawakuwa na haja ya kuyauza maeneo yale, kwani ukiyaangalia utaona waliyapangilia ili vizazi na vizazi vya kwao viishi hapo.

Hii haihitaji mjadala wala maelezo marefu, lakini ni ushahidi tosha kwamba inaweza ikawa ndiyo sababu kubwa iliyomfanya Mzee Jumbe Tambaza awe mstari wa mbele kabisa katika kuwachukia watawala wa Kizungu na kumuunga mkono Nyerere kwa nguvu kubwa kama ile.

Mchango wa Mzee Jumbe Tambaza katika ukombozi wa nchi yetu haukutetereka hata kidogo, kwani hata pale rafiki yake mpenzi Sheikh Suleiman Takadir, alipotahadharisha watu kuwa makini na Nyerere maana ameonyesha kwamba siku za usoni angependelea zaidi jamaa zake, Mzee Jumbe hakumuunga mkono na akakubali Sheikh Takadiri atengwe na jamii kwa manufaa ya umoja wa kitaifa.

Jumbe Tambaza pia hakumuunga mkono Zubeir Mtemvu, kwenye suala la Kura Tatu ambalo ilibaki kidogo tu chama cha Tanu kingesambaratika na kuwa vipande viwili; lakini yeye alibaki na Nyerere wake mpaka dakika ya mwisho kule Tabora hadi kukasainiwa waraka wa ‘Uamuzi wa Busara’ ambao uliwapeleka TANU kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu.

Katika picha ya pamoja iliyopigwa baada ya kutangazwa ushindi wa kuingia kwenye Kura Tatu kwa chama cha TANU, anayeonekana nyuma ya Mwalimu Nyerere pale Tabora ni Mzee Jumbe Tambaza. (Rejea kitabu Mohammed Said, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes… uk 275).

Kutokana na uaminifu wao usiotetereka kwa chama chao, Mzee Jumbe Tambaza na mwenziwe Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; wazee wale wawili wa Kimashomvi kutoka Mzizima, kwa muda mrefu wamekuwa wajumbe wa kudumu (permanent seats) kwenye Kamati Kuu ya TANU bila kupigiwa kura; achilia mbali ule uwepo wao kwenye Baraza la Wazee wa TANU.

Mnamo mwanzo wa miaka ya mwanzoni 1950, Mzee Tambaza alitumbukizwa tena kwenye mgogoro mkubwa na serikali pale ilipokuwa inajenga upya Barabara ya Umoja wa Mataifa kutokea Faya kuelekea Daraja la Selander, ilipoamuliwa kwamba sehemu ya eneo la makaburi iondoke kupisha ujenzi huo.

Hayati Mzee Tambaza, alifungua kesi mahakamani dhidi ya serikali, kesi ambayo inatajwa kama moja ya kesi nzito (landmark cases) sana kutokea hapa nchini na Afrika Mashariki iliyogusa imani ya Dini ya Kiislamu; kwamba je, ni halali au si halali kufukua makaburi ya watu waliokufa?

Kesi ya Makaburi, kama ilivyokuja kujulikana, iliunguruma kwa muda mrefu na kujaza kurasa za mbele za magazeti wakati huo, kutokana na mabishano makali ya hoja (cross examinations) mahakamani baina ya mawakili wa pande mbili hasimu.

Wakati serikali ikiwatumia masheikh wazawa wa hapa waliosema kwamba inakubalika kufukua makaburi, Jumbe Tambaza aliwatumia masheikh wakubwa kutoka Mombasa na Zanzibar, akiwemo aliyekuwa Kadhi wa Zanzibar Abdallah Saleh Farsy kupinga hoja hizo.

Kwa kishindo kikubwa, Mzee Tambaza alishinda kesi ile na ikabidi barabara ile ipindishwe pale kwenye mteremko wa kutokea Faya na kuyaacha makaburi na vilivyo ndani yake kama yalivyo. Haraka haraka, Hayati Mzee Tambaza akafanya maamuzi ya kujenga msikiti ambao haukuwapo mahala hapo kabla ya tukio hili, kuepusha kujirudia.

Huyo ndiye Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, mwanaharakati wa kupigania uhuru wa taifa hili wa kupigiwa mfano, aliyetetea na kutoa vyake kusaidia wanyonge wenziwe katika jamii yetu katika kipindi cha manyanyaso ya utawala dhalimu wa Malkia wa Uingereza. Alimfanyia madua na matambiko ya jadi Mwalimu Nyerere ili nuru yake ing’are kama mwezi na jua!

Ewe Mola Mghufirie madhambi yake – Ameen.
Historia nzuri sana, inatufundisha kukaa na wazee tupate hekima zao. Je viongozi wa sasa wanaweza kujishusha hivyo na kupata baraka na ushauri wa wazee?
 
Mzee Mohamed Said, umeongelea kuhusu shule ya Azania kujengwa na wahindi, ila nafikiri umetatanisha kidogo, navyofahamu, Tambaza ndiyo ilikuwa Aga Khan Boys na zanaki, Aga Khan girls huku muhimbili primary ikiwa Aga Khan Primary.

Azania ilijengwa na serikali baada ya uhuru (ikiwa ni shule pekee ya sekondari ya kiume jijini huku Jangwani iliyojengwa na wajerumani ikibaki kuwa ya wasichana) kabla ya shule za Agha Khan kutaifishwa. Ndipo waismailia walipojenga shule yao mpya ya Aga Khan Mzizima sec school 1967.
 
Chamoto,
Muandishi wa makala hiyo ni Abdallah Tambaza si mimi.
Mimi nimeleta hapa.
 
sawa. nimekusoma sheikh.

nirudi kwako wewe binafsi....

ninaamini wewe ni muumini mzuri wa Uislamu.
swali langu kwako - jee, unaona walichofanya ma sheikh wetu kuchanganya ibada (Mungu vs miungu) ni sawa au si sawa from Islam doctrine perspective?

M-mbabe,
Mimi si mtaalamu wa dini kuweza kujibu swali hilo.
Mimi ni mwanahistoria.

Shabaha yangu wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ilikuwa
kuwaeleza watu nini Abdul kaifanyia Tanganyika na kumfanyia
Nyerere na TANU.

Hivi ndivyo nilivyokutana na haya yote ya dua za usiku, Dar es Salaam,
Tanga na Lindi na kuwaleta katika historia ya TANU wazalendo hakuna
mtu alipatapo kuwasikia hata kwa mbali.

Niulize maswali katika historia hii.
 
Chamoto,
Muandishi wa makala hiyo ni Abdallah Tambaza si mimi.
Mimi nimeleta hapa.
Halafu wewe unataka sisi tuamini kila kitu wazee wako wa Gerezani walikueleza wakati mmoja kishashikwa ni mwongo na umeshindwa kumtetea na kutuambia wewe si mwandishi.
 
M-mbabe,
Mimi si mtaalamu wa dini kuweza kujibu swali hilo.
Mimi ni mwanahistoria.

Shabaha yangu wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ilikuwa
kuwaeleza watu nini Abdul kaifanyia Tanganyika na kumfanyia
Nyerere na TANU.

Hivi ndivyo nilivyokutana na haya yote ya dua za usiku, Dar es Salaam,
Tanga na Lindi na kuwaleta katika historia ya TANU wazalendo hakuna
mtu alipatapo kuwasikia hata kwa mbali.

Niulize maswali katika historia hii.
Mbase...
Jitulize na soma upya mjadala wangu na Chamoto na zingatia
nini ameniuliza na mimi nimemjibu nini.

Hapajakuwa na suala kuwa yaliyoandikwa si kweli.

Usiandike kwa ghadhabu ingawa historia hii kawaida yake toka
ilipoanza kuandikwa takriban sasa miaka 20 imekuwa ikichoma
nyoyo za wengi kwa bahati mbaya wewe ni mmoja wa hao.

Lakini muhimu ni kuwa mtu hana lazima ya kuamini hii historia
na wala sijakutaka wewe uamini ninayoandika na una uhuru na
haki ya kuona historia hii wala haikuwapo ni utunzi wa hadithi.

Historia ya Mzee Jumbe Tambaza sikuandika mimi kaandika
mjukuu wake Abdallah Tambaza.
 
Dah aisee historia kama hizi bora mmezidocument mapema kabla jua lenu kuzama

Mimi naifahamu upanga vizuri sana ule mskiti maamur umepakana na mgahawa mmoja zamani duka linaitwa *chetu wote*
Mle ndani kwa nyuma kuna mzambarau kweli kwenye zile flat za wahindi zamani usalama wa taifa na sasa kuna ofisi za mama Anna mkapa fursa sawa kwa wote

Swali langu ni je hayo makaburi ya wazee wako yako ndani mskitini au kwenye mgahawa wa chetu wote yule mangi kwa nyuma?
 
Ni kweli pia upanga kuna mi zambarau mingi sana kuanzia muhimbili kushuka mpk mitaa ya tunakopesha makao makuu aisee nimependa sana hili bandiko

Pia ilipo baa ya tairo nasikia palikuwa na machine ya kusaga ya kina mama Sophia simba hili nalo ni kweli?
 
ACHA NA MIMI NIFUTE WATU TONGOTONGO KIDOGO KISHA MWISHONI NITAZUNGUMZA KUHUSU HIZO DUA AZLIOFANYIWA HAYATI MWL J.K NYERERE

Maisha yamegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
1. Ulimwengu wa roho
apa namaanisha ulimwengu usionekana kwa macho ya kawaida, hapa ndipo tuaminipo ktk Mungu na Ibilisi.
2. Ulimwengu wa nyama
ulimwengu ni katika vitu vyote ambavyo tunaviona kwa macho yetu ya kawaida.
Nianze kusema kuwa, Taifa la Tanzania limefika hapa lilipo kutokana na makosa yaliyofanywa na waasisi wa hili Taifa na wale ambao wapo pia madarakani ila sana sana ni waasisi, kwanini? kwasababu muasisi wa taifa ama waasisi wa taifa ni LANGO la taifa.

Lango ni nini? Katika tafsiri ya kawaida lango ama mlango ni sehemu inayopitisha kitu ili kuingia ndani, kama tunaona katika ulimwengu wa nyama kuwa ipo mipaka ya nchi ambayo mtu, wanyama n.k huingia ndani ya nchi husika, vivyo hivyo ipo milango ama lango katika ulimwengu wa roho ambao unapitisha mambo ya rohoni ndani ya nchi.

NOTE:
Chochote ukionacho katika ulimwengu wa macho ya nyama, tambua kimeanzia rohoni. Hata katika uumbaji Mungu alianza kumuumba mwanamke na mwanaume ktk ulimwengu wa roho kisha ikaja kudhihirika ktk ulimwengu wa nyama.

Mnamo mwaka 1961, baada ya Waingereza kuiachia Tanganyika, waasisi wa hili Taifa wakiongozwa na Nyerere walitegemea saana ama niseme ni waamini wa ulimwengu wa roho ktk ufalme wa giza, hivyo walienda kwa wachawi wa nchi ama waganga ili kupata maarifa na akili ya kuiongoza nchi.
Moja ya vitu ambavyo vilitokea kwao ni kutopata tu maarifa na akili bali pia walitakiwa wakubali wachawi mazindiko ndani ya nchi, chama cha siasa TANU ambacho sasa hivi ni CCM kuzindikwa ama kuongozwa na serikali ama tawala za kuzimu Tanzania.
Nisizungumze mengi, nikatishe kwa kusema kuwa Mwl Nyerere kama kiongozi wa nchi ama muasisi wa Taifa hili, ndie alikuwa lango la kupitisha falme za giza ndani ya nchi ya Tanzania ambapo hata yeye mwenyewe hakujua kama haya anapitisha haya mambo ambayo yaliicost Tanzania kipindi kile na hata sasa. Hayati Baba wa Taifa angejua kama kupitia yeye anapitisha haya mambo wala asingekubali na kama angekuwa na nguvu ya kujinasua angefanya hivyo ila kwa bahati mbaya hakuwa nayo.

TURUDI KWEYE MADA
Dua alizosomewa Hayati JK Nyerere ndizo tunazoita ushirikina sana sana katika kusafisha Nyota, kwanini?
Mungu anapomuumba mwanadamu huwa anamuumba kwa jinsi yake nikimaanisha vinasaba, mtazamo, akili, nyota, hekima, maarifa n.k ila viongozi wengi wa nchi huwa wanapewa akili ya ziada na kupandikiziwa nyota ambazo sio za kwao. Wachawi/Waganga wana uwezo wa kutambua nyota ya mtu tangu akiwa mtoto na wana uwezo wa kutoa nyota yako na kumhamishia mtu mwingine, sio nyota tu bali hata nafsi na mengineyo.
Hayati Baba wa Taifa ni moja ya viongozi waliveshwa nyota ambazo hazikuwa ni za kwao, hizo nyota wachawi/waganga wanazimiliki sana huko kuzimu.

Embu jaribu kutafakari, endapo kweli Mwalimu Nyerere alikuwa na vinasaba vya uongozi, je katika watoto wote aliokuwa nao hakuna hata mmoja ambae ana vinasaba vya baba yake? HAKUNA, endapo uongozi wake ile hekima na maarifa na nyota yake alipewa na Mungu katika uongozi basi kati ya watoto wake wote alokuwa nao yupo mmoja walau angekuwa na characters kutoka kwa baba yake.

Watanzania tusiwasifu sana hawa wasomaji dua hususani wanaojiita wazee wa Dar es Salaam, ni washirikina wakubwa mno, maisha tunayoishi leo Watanzania ni matokeo ya maagano ya kuzimu na watawala wetu ndio maana leo hii akili za watanzania zimefungwa kutokana na yale mazindiko. Mtawala anaweza akafanya chochote na watanzania wasichukue hatua, UFISADI, WANYAMAPORI, DEMOKRASIA N.K watanzania tunalalamika kwa muda ila watawala kupitia wachawi wa nchi wanazima akili za watanzania na hawahoji tena wala hawakumbuki.
kwa leo nitaishia hapa ila ipo siku nitaandika kwa mapana mnooooooo kuhusu haya mambo, kwa wale msionielewa mnisamehe, sina kipawa cha kufindisha na haya nimeyaandika ghafla ila ipo siku nitayaandika kwa mpangilio mzuri kabisa.
Dah...Sijaelewa...nimekusamehe...ila nawe naomba uniwie radhi[emoji13]
 
Ukipata jibu nitag please

sheikh Said naomba unisaidie ilimu kidogo kuhusu Uislamu. nimenukuu hiko kifungu kidogo hapo juu kwenye bandiko lako kwa ajili ya rejea.

inaonekana dhahiri kuwa ma sheikh uliowataja hapo juu walifanya ibada kwa Allah na baada ya kumaliza wakafanya pia ibada ya matambiko ya "miungu".

swali langu..... jee, kwenye dini ya Kiislamu - ibada (Allah) na matambiko (miungu) huchangamana?
 
Ndugu zangu,
Katika hizi dua na matambiko kwanza napenda nikufahamisheni kuwa
Nyerere si wa kwanza kufanyiwa hizi dua.

Wakati nafanya utafiti katika kuandika kitabu cha Abdul Sykes kwa
mara ya kwanza nilikutana na dua katika kisa cha ugomvi baina ya
Abdul Sykes na Mzungu aliyekuwa ''boss,'' wake aliyevamia ofisi yake
ya Market Master Kariakoo Market akamkuta Abdul anauza kadi za
TANU na nyingine anazo katika mtoto wa meza.

Wafanya biashara pale sokoni kwa kuhofia kuwa Abdul atafukuzwa
kazi waliamua kufanya dua.

Nimeelezwa kila kitu nini kilifanyika katika dua na katika makubwa
zaidi na nini yalikuwa matokeo yake.

Inatisha.
Hii ilikuwa 1955.

Sikuweza kukiandika kisa kile katika kitabu na siwezi leo kukihadithia
hapa.

Abdul hakufukuzwa kazi ila aliyepata shida ni Mzungu na TANU ikazidi
kuimarika na Abdul kaendelea kuuza kadi zake za TANU sokoni Kariakoo.

Dua nyingine ilikuwa ya Rashid Ali Meli aliyetoa fedha katika sefu yake
kazini akiwa Mtunza Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council akampa
Idd Faiz Mafungo itiwe kwenye mfuko wa safari ya Nyerere UNO 1955.

Wakaguzi walifika siku ya pili kufanya ukaguzi na ikawa hatari Rashid Ali
Meli
atafungwa kwa ''wizi.''

Walipofungua sefu fedha walizikuta zote kamili hakuna hata senti moja
iliyopotea.

Special Branch walikuwa wametoa taarifa zisizo shaka walizopewa na mtu
wao ndani ya TANU tena kiongozi wa juu kabisa.

Dua nyingine 1956 iliyofanywa Lindi na Sheikh Yusuf Badi Nyerere
akiwapo.

Tabu kuamini yaliyotokea usiku ule.
Sijaweza pia kuandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Dua ilifanyika nyumbani kwa Suleiman Masoud Mnonji Mtaa wa Makonde.
Hii ilikuwa 1956

Dua nyingine ni ya Mnyanjani kuhusu Kura Tatu mwaka wa 1958.
Sishangai kuwa leo watu wanatatazika na historia hii.
Huu ni ushirikina.
 
M-mbabe,
Mimi si mtaalamu wa dini kuweza kujibu swali hilo.
Mimi ni mwanahistoria.

Shabaha yangu wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ilikuwa
kuwaeleza watu nini Abdul kaifanyia Tanganyika na kumfanyia
Nyerere na TANU.

Hivi ndivyo nilivyokutana na haya yote ya dua za usiku, Dar es Salaam,
Tanga na Lindi na kuwaleta katika historia ya TANU wazalendo hakuna
mtu alipatapo kuwasikia hata kwa mbali.

Niulize maswali katika historia hii.
Hapa cha uongo ilikuwa lazima uruke kiunzi ukikamatwa km kawaida yako.
 
Dah aisee historia kama hizi bora mmezidocument mapema kabla jua lenu kuzama

Mimi naifahamu upanga vizuri sana ule mskiti maamur umepakana na mgahawa mmoja zamani duka linaitwa *chetu wote*
Mle ndani kwa nyuma kuna mzambarau kweli kwenye zile flat za wahindi zamani usalama wa taifa na sasa kuna ofisi za mama Anna mkapa fursa sawa kwa wote

Swali langu ni je hayo makaburi ya wazee wako yako ndani mskitini au kwenye mgahawa wa chetu wote yule mangi kwa nyuma?
Uliyejinasibu kuwa upanga unaifshamu vizuri sana unaliuliza tena.wabongo ni nani aliyewaroga?
 
Back
Top Bottom