Jumla ya Simba kufungwafungwa.

Mchokoo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
1,181
Reaction score
1,579
1) Magumashi katika usajiri wao. Tizama Baleke, Kapama, Okra, Banda, Okwa, Kibu, Watara.
Hawa ukiwachanganya na Boko utafungwa mpaka ucheke!

2) Wachezaji wanamwomba Mungu, hapohapo timu inaroga.
Mungu na ushirikina wapi na wapi? Yaani timu imewekeza sana kwenye matunguri kuliko viwango vya wachezaji.

3) Tuwe wakweli, mwekezaji wa Simba hana hela. Kama anazo basi ni bahiri hadi kapitiliza kipimo.

4) Simba ina mgogoro wa chini kwa chini.
Kuna mgawanyiko wa kuona jambo fulani haliko sawa.
Rejea, kuna waliojiuzuru nafasi zote za uongozi. Babra, Azim Dewji.

5) Kwa sasa timu ina viongozi mamruki, wasio na kauli yoyote ile, ni kama hakuna uongozi pale.

6) Mashabiki wamechelewa sana kujua hali mbaya ya timu yao. Ndiyo maana jana walijaza uwanja wakidhani ni ile simba ya kina Mikisoni.
7) Kuwadharau sana makocha wazawa kwa kuthamini wageni.
Hivi mgunda alikuwa na tatizo gani?
Jamani shida ya simba siyo kocha. Ni viwango duni vya wachezaji.
Ushaurii:
Ukipanda miiba, usitarajie kuvuna maparachichi.
Wanasimba na Mo wao, watakula kule walikopeleka mboga.
 
Uliyoyaandika hapa yanga yote wanafanya
 
Hakuna aliyemlazimisha kuja pale Simba.
Hivi hujui kama si yeye timu angechukuwa Bakhresa. Au kama vipi aiteme uone kama haijachuliwa na mabilionea wa ukweli.
Unataka atumie hela zake zote kukupa furaha wewe, acha ujinga mpira hauko hivyo bro
 
Mtaandika mengi sana lakini kaa ukijua hakuna timu ya Tanzania inayoweza kusajili wachezaji wazuri kushindana na timu kubwa kama Raja. Wachezaji tunaosajili ni kwa ajili kushinda NBC premier League na kushiriki CAF hatua za awali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…