Jumuiya ya madola (common wealth) yatoa msimamo kuhusu Tanzania

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Katika taarifa yake ya kikao chao cha Septemba 20, 2026 CMAG imesisitiza yafuatayo:

1. Kuendeleza mchakato Unaojumuisha pande zote, unaoaminika na unaowezeshwa kupitia ushirikiano kati ya vyama vya siasa.

2. Kulinda Uhuru wa kiraia, Uhuru wa kisiasa na Uhuru wa vyombo vya habari.

3. Kuhakikisha taratibu za kisheria katika kesi ambazo bado hazijamalizika zinafanyika kwa haki, kwa wakati na kwa uwazi.

4. Kuweka mifumo inayoaminika ya kuhakikisha Uwajibikaji, kutoa Haki kwa walioathirika (Hapa wanazungumzia mauaji ya Oktoba 29) na kulipa fidia stahiki

Tanzania itaendelea kubaki kwenye ajenda rasmi ya CMAG, huku Jumuiya hiyo ikiitaka Serikali kuweka tarehe ya mapema ya ziara ya Katibu Mkuu kwa ajili ya mazungumzo na Nduli Idd Amin Mama na wadau wengine.

NB. Serikali haram kupitia Mahmoud Kombo alipeleka taarifa ya uwongo wakadhan wajumbe wa CMAG watafanya maamuzi kwa kuzingatia kale kareport walikowasilisha wao wakadhan jambo limeisha yani hii ngoma bado mbichi halafu Katibu Mkuu wa Common Wealth kila akiwambia anataka kuja Tanzania wanampiga chenga maana hawataki aje, sasa Mara hii hadi kikao kimeadhimia, sijui watajitetea na nini?😂

Mungu awabariki wote ambao mlitenga muda wenu kuandika emails na kuwatumia wajumbe wa CMAG, tuendelee kupeleka moto mpaka wateme ndoano.
 
Umeisoma na kuilewa hiyo taarifa?
 
Lisu huyooo anafutiwa kesi
 
Unamuuliza Mshana Jr hilo swali, hebu jiangalie Kijana.
Unajua Mshana ni mwandishi mkongwe , ama upo filed ya chuo cha kati na WiFi ya ofisini unahoji tu?
Mwandishi mkongwe kwa kumlinganisha na nani?
Unamjua Titus Philipo,Juma Nkamia,Ben kiko,Ahmed Jongo n.k?
 
Mkuu mahakama zetu zimekuwa kama bunge la JMT, hakuna pa kukimbilia.
 
Katika taarifa yake ya kikao chao cha Septemba 20, 2026 CMAG imesisitiza yafuatayo:
1. Kuendeleza mchakato Unaojumuisha pande zote, unaoaminika na unaowezeshwa kupitia ushirikiano kati ya vyama vya siasa.
Unaojumuisha pande zote! Hapa kuna pande mbili tu, zile pande nyingine zipo upande ule
Unaoaminika! Hadi juzi walikuwa na taarifa ya Tume inayoendelea. Kauli ya unaoaminika inaeleza kutoaminika
Unaowezeshwa kupitia ushirikiano kati ya vyama vya siasa! Kwamba lazima pande zikubaliane na mchakato
2. Kulinda Uhuru wa kiraia, Uhuru wa kisiasa na Uhuru wa vyombo vya habari.
Uhuru wa kiraia ni uhuru chini ya sheria kufanya ya kiraia kwa mfano kukusanyika
Uhuru wa kisiasa, kwamba, kusiwe na kufungia shughuli za siasa
Uhuru wa habari, kwamba, media zitoe taarifa bila kufungiwa
3. Kuhakikisha taratibu za kisheria katika kesi ambazo bado hazijamalizika zinafanyika kwa haki, kwa wakati na kwa uwazi.
Hii ipo kama ilivyo!
4. Kuweka mifumo inayoaminika ya kuhakikisha Uwajibikaji, kutoa Haki kwa walioathirika na kulipa fidia stahiki
Kwamba wawepo watakaowajibika, waathirika wapewe haki na fidia

JokaKuu
 
Uhuru wa Kiraia (Civil Liberties): Haya ni malinda ya kisheria yanayomzuia mtawala au serikali kuingilia maisha binafsi ya mwananchi.

Mfano uliotoa wa uhuru wa kukusanyika, pamoja na uhuru wa kuabudu na uhuru wa kwenda kokote, ni mifano halisi.

Uhuru wa Kisiasa (Political Freedom):
Hii inahakikisha kuwa wananchi wana haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi yao.
Inajumuisha haki ya kuanzisha au kujiunga na vyama vya siasa, kugombea nafasi za uongozi, na kupiga kura bila woga, vitisho, au vikwazo vya kiutawala.

Uhuru wa Habari (Freedom of the Press/Information):
Huu ni muhimili mkuu wa uwazi. Vyombo vya habari (media) vinapaswa kuwa na uwezo wa kufanya uchunguzi, kuripoti matukio, na kutoa taarifa kwa umma bila hofu ya kufungiwa, kudhibitiwa (censorship), au kushitakiwa bila sababu za kisheria.

Vipengele hivi vitatu kwa pamoja ndivyo vinavyojenga jamii huru na yenye haki
 
ok.
 
Mwandishi mkongwe kwa kumlinganisha na nani?
Unamjua Titus Philipo,Juma Nkamia,Ben kiko,Ahmed Jongo n.k?
Kwani ukongwe wa mtu unapimwa kwa kulinganisha na mtu/ watu ? Au experience & tenure?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…