Kina nani wanaunda kikundi hiki, nani aliwateua au kuwachagua, kina halali gani kikatiba na kisheria, wanafikiri risasi zitaleta amani. Kichunguzwe na malengo yake yachunguzwe.
Hongera Chadema kwa kukataa kujihusisha na hiki kikundi cha kihuni.
=============
Afisa Mnadhimu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna Masaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Obadia Nselu, amesema Chuo hicho hakihusiki na chapicho lililotolewa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa chuo hicho Naibu Kamishna wa Polisi DCP Dkt. Lazaro Mambosasa, amesema, kumekuwa na chapisho linalotumwa kwenye makundi sogozi likieleza kuwa, Chuo hicho kinatarajia kutoa Mafunzo ya Ulinzi, Upigaji wa Shabaha, Intelejensia na Itifaki za Nyanjani (MUSIN) kwa JMAT.
Aidha, SACP Nselu amesema kuwa, chuo hicho kilipokea barua yenye kumb: JMAT/IMFU/MUSN/2026/001 ya Julai 28, 2026 ikiwa na maombi ya JMAT kupatiwa mafunzo hayo, baada ya Chuo hicho kujiridhisha kwa kina maudhui yake, kiliwasiliana na Mkurugenzi wa jumuia hiyo Bwana Ayoub J. Sanga kuwa, yasingeweza kutolewa kwasababu ya kiusalama na kwamba mafunzo hayo yanatolewa kwa vyombo vyenye ithibati ya kijeshi.