Jumuiya ya wanafunzi CHADEMA: Ripoti ya CAG, imeonesha madudu yaliyopitishwa na wasomi, waliyakubali bila kuangalia athari

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Jumuiya ya wanafunzi wa Chadema (CHASO) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imewajia juu wasomi nchini kwa kile walichokiita "uchawa wa wasomi," wakidai kuwa hali hiyo inaliangamiza taifa. Akizungumza kwa niaba ya jumuiya hiyo, msemaji wao ameeleza kuwa wasomi wengi wameacha weledi na kugeuka kuwa wasifiaji wa serikali badala ya kuwa wakosoaji, jambo ambalo linafungua mianya ya ufisadi na kupoteza mabilioni ya fedha za umma katika miradi isiyo na tija.

Akisisitiza madhara ya tabia hiyo, msemaji huyo alisema: “Wasomi tunapogeuka kuwa machawa wa mfumo, machawa wa madaraka na tunashindwa kusimamia misingi yetu, tunaliua taifa kimeyakimya. Inabidi tuwe wakosoaji wa serikali na sio wasifiaji.” Aliongeza kuwa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonesha madudu mengi kwenye miradi ambayo wasomi walishiriki kuipitisha na kuishauri serikali bila kuhoji gharama na athari zake kwa jamii.

Aidha, vijana hao walitolea mfano mradi wa maji wa Ruvu Juu, wakidai kuwa wasomi walisimama na kutoa ahadi kuwa kero ya maji ingeisha Dar es Salaam, lakini hadi kufikia mwaka 2026, wananchi wa maeneo kama Ubungo bado wanateseka bila huduma hiyo. Walihitimisha kwa kutoa wito kwa wasomi kurejea kwenye misingi ya taaluma zao na kuisimamia serikali ili kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote badala ya kuishia kwenye sifa zisizo na tija.

Chadema Haina wapumbavu kama kule kwingine
 
bado wanafunzi wasio na maono hao, wapuuze tu 🐒
 
Back
Top Bottom