GE2025 Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDASA) watoa tamko kali hali ya kiusalama nchini wagusia Utekaji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Andiko lenu lina madhaifu mengi sana. Kama tuna wahadhiri wa kiwango hiki, bila shaka tumekwisha. Kunahitajika reform kubwa sana ya kujenga kundi la wahadhiri linalojiambua na tayari kuipeleka Tanzania kwenye kutimiza vision 2050.

1. Wasomi wameshindwa kutofautisha baina ya kukosoa na kutukana.
2. Baadhi ya vifungu vya Katiba vinapaswa kusomwa au kurejewa kwa uangalifu pamoja na ufafanuzi wake ili kutoleta taharuki. Kwa kifupi makosa ni mengi na UDASA mmetuangusha saaaana kuja na andiko biased kama hili.
 
Tunafika pazuri taratibu, wasomi wakipunguza uchawa hata kama hawataumaliza kabisa, heshima ya nchi itaanza kurudi! Japo wachache sana against population
 
Wananchi tunaangalia na tunaenda na wanaosimama na haki, hayo makosa madogo madogo ya kiuandishi hayana uzito wowote na hayaathiri lolote hoja yao ya msingi.
 
Mwendo uwe ni waraka kwa wote wazalendo na wanaochukizwa na uhuni unaoendelea katika taifa letu,nitafanya dua ili wote waguswe kutiririsha waraka za ukombozi wa taifa hilikuelekea 29 Oct.Mungu awaongoze na kuwalinda dhidi ya madhila yote na mwongezewe Uzalando dhidi ya Taifa letu.
 
Uyu mama kwa kung’ang’ania uku, ni wazi kuna mambo ya ajabu makubwa mno ameyafanya na mengine wanampango wa kuyafanya…kwake hii ni life and death, hawezi achia kwa amani
Huu ndio ukweli wenyewe.
Hawezi kuachia madaraka bila ya kulazimishwa kufanya hivyo.
 
Asante Udasa, may you live longer. Wamenikumbusha enzi za malegendary Prof. Seith Chachage, Haroub Othman, Mwesigwa Baregu, Issa Shivji etc. Hongereni sana kutuunga mkono watanzania.💪🙏🙏🙏
Imebidi nisome jina mara tatu, kuhakikisha ujumbe huu unatoka kwa mtu mwenye jina hilo.
Nimefarijika sana na msimamo wako huu.
 
Inatosha tu kwa sasa, kukariri jina lako, nisilisahau: "Zed"

Ninajishangaa sijawahi kukusoma hadi hii leo!
 
Hizi Taasisi ifike mahala ziache Upumbavu sasa ziendane na karne tuliyopo ya Kuwa Huru kama Taasisi na Kuzungumza Ukweli uliopo bila Woga na Uzandiki + Uchawa ndani yake.
 
Baada ya salamu nina haya tu;

1. Mbona hamjatoa mfano wa maandamano ya Kenya ambayo Yana unasaba mkubwa mno na sisi kutokana na muingiliano wa kitamaduni, kijiografia na kijamii na badala yake tumeshangaa kuona mmetolea mifano miwili tu ya Nepal na Madagascar?!!! Mnataka tufikiri kuwa mna lebu jambo na upande?!!! Do you real want to make us nervous?!! Are you brave enough to calm our nerves?!! Kenya walitaka Ruto aondoke madarakani; nawakumbusha tu UDASA. Vipi, haifanani na haya mnayoyaaka nyie...oops sorry, kumbe nyie mnasema hamhamasishi maandamano (mpo neutral 🤣🤣🤣). Nilimaanisha vipi, hayafanani na haya wanayoyataka hapa?! Kulikuwa na ubaya gani kuyatolea mfano. Mbona mnatushangaza wasomi nyie nyie 'mlioelimika' na 'msioendeshwa' na watu?!!!😄😄😄

2. Mbona mifano yenu ya waliotekwa imejikita kwenye ile ile tu inayosemwa na maria sarungi, mange na wenzao kina lissu na heche?!! Kwenye idadi kubwa yote hiyo "mliothibitisha" kuwa kweli wametekwa mmeona mje na majina Yale Yale tu ya mange kweli?!!! Kama 'wasomi wabobezi', hamuoni kuwa wasiosoma wanaweza kuhusi kuwa kuna connection kati yenu.....yaani mmeshikiwa kiakili?!! Kushikiwa akili ni aibu sana kwa wasomi wabobezi'!

3. Hiyo report ya amnesty inayosema 2020 walitekwa watu wanne (4) tu mnaweza kuwapelekea wake zenu na kuwasomea Huku mkiwaangalia usoni?!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…