Juninho Pernambucano: Mpiga freekick bora kuwahi kumtizama

Juninho Pernambucano: Mpiga freekick bora kuwahi kumtizama

makaveli10

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
31,583
Reaction score
92,670
Katika maisha yangu ya kutazama soka, sijawahi kuona mtu anapiga freekicks kama huyu mwamba, najua wapo kina beckham, ronadinho, messi, zidane, fundi pirlo, cr7, shunshuke nakamura na wengine wengi, ila juninho hana mpinzani, jamaa alikuwa hatar, zaidi ya hatari, kwanza hakuwa na eneo maaluum tofauti na hawa wengi ambao kuna sehemu na sehemu, jamaa ilikuwa popote anakuweka..

Inakadiriwa alifunga magoli ya freekicks yapatayo 80 kasoro kidogo katika official matches.. jamaa alikipa sana lyon ile iliyobeba ubingwa mara 7 mfululizo, katika goli 100 alizofunga pale lyon basi 44 ni za faulo..
Na upigaji wake ndio kuna baadhi ya wachezaji wamechukua kwake..

Heshima kwako juninho pernambucano.
 
Mkuu ahsante sana kwa Kumbukumbu mujarabu!

Madrid wamepata tabu sana uefa na Lyon ya huyu jamaa!

Juzi kati nilikuwa naongea na watu wa mpira, nikawa nawaelezea balaa la huyu Mbrazil!

Huyu jamaa namkumbuka vizuri sana. Kuna game ya Lyon, huyu jamaa akaenda kupiga free kick! Akatisha kama anapiga juu, wale wa ukuta wakaruka! Akapiga chini. Wavu! Lyon wakapata tena free kick! Wale wa ukuta wakajua jamaa anapiga chini, this time Juninho akapiga NDIZI! Wavu! Lyon walishinda 3!
 
Zaidi ya free kick he had nothing else to offer.

Huwezi mtegemea mtu ambaye yupo so limited, alikua master wa eneo moja huku akipwaya sana Kwenye position yake Kama mid, ndo maana hujawahi sikia miamba ya Ulaya kama Madrid, Barca, Milan ya miaka ile ikimtaka, na hata Brazil national team hakua na number.

Alikua master of set pieces tu.
 
Sio lazima kila mchezaji nyota acheze hizo timu! Unamkumbuka All time goal scorer wa EPL? Unajua aliwika wapi na alistaafia wapi? Unamfahamu mtu alieitwa DEVOR SUKER? Hao waliwika pasi na kuchezea hizo timu ulizotaja!
 
fe1aab0f-be05-4bee-a022-883cc839bd49-1336x2040.jpeg
 
Bila video wengine ni vigumu kutuaminisha
Mkuu unataka video ama sehemu utakapopata video.. Video zote za juninho tuweke hapa kweli, nenda youtube utamkuta

Na hapa hatuaminishani, tunaongea kitu kilichopo, wapenz halisi ni ngumu kutokumjua huyu kiumbeblabda uniambie mpira umeanza kutizama miaka ya ya hapa karibuni.
 
Mkuu ahsante sana kwa Kumbukumbu mujarabu!

Madrid wamepata tabu sana uefa na Lyon ya huyu jamaa!

Juzi kati nilikuwa naongea na watu wa mpira, nikawa nawaelezea balaa la huyu Mbrazil!

Huyu jamaa namkumbuka vizuri sana. Kuna game ya Lyon, huyu jamaa akaenda kupiga free kick! Akatisha kama anapiga juu, wale wa ukuta wakaruka! Akapiga chini. Wavu! Lyon wakapata tena free kick! Wale wa ukuta wakajua jamaa anapiga chini, this time Juninho akapiga NDIZI! Wavu! Lyon walishinda 3!
Kuna game ilikuwa na ac milan nahis, alichomesha, akaenda kuchukua mpira wavuni mwenyewe, ilipopatikana freekick akafurahia na kweli alitupia mpira kambani.
 
Back
Top Bottom