Junior Kasanga na raia wa China, wakamatwa wakitorosha dhahabu waliyochimba

Hahahaha! Ulimuuliza kichina? Uskute lugha zilikua zinagongana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaongea kiswahili kizuri kabisa, halafu alikua na jamaa mwingine mchina sijui ni boyfriend wake, nae nikamuuliza unaitwa nani akaniambia anaitwa sajuki, honestly niliangua kicheko mbele yao halafu nikamuita Mr nikamwambia sajuki na esta wanataka kupanga apartment yetu ya sehemu fulani, Mr akaniambia waambie watoe ujinga hapa, nikamwambia yule dalali aliewaleta kwamba hatupangishi wachina
 
Ma nchi kama haya ambayo watu wake kuiba wanaona ni moja ya njia ya kujipatia kipato ni bora kuwa na viongozi madikiteta tu kwa maana democrasia haiwezi kufanya kazi kwa Africa hata siku moja .
heri ya nusu shari kuliko shari kamili, alieitwa dikteta uchwara katuacha ulimi nje!!
 
Wachina ni mbwa niliwahi kuwapelekea pembe za ng’ombe vingunguti wakatokomea na cash yangu hawafai hao
Hahahaha Hahaha
Mkuu arovera nmecheka sana
Yaani napata picha jinsi walivyokuacha sjui ilikuwaje....

Kuna mchina mmoja nlikuwa nafanya naye biashara namuzia majongo bahari alikuwaga
Barabara ya hombos, kuna siku tuko ndani
Mara nkaona mtu amepotea anaruka fence yake
Ahh wengine kuona vile machale faster,yakatujia tulipotea pale kama maninja
Badaye kuulizia kmbe walikuwa watu wa mali asili nk,nkasema mtu unaweza tokea kimzamza kwenye itv habari saa mbili usikušŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚

Hawa jamaa ni full magumashi

Ova
 
Ninachoshangaa mbona wilaya na majimbo yenye Madini kama Dhahabu hakuna Maendeleo wakati Kodi zinazokatwa kwenye Madini hayo ni Kubwa shida ni nini? Au hakuna mgao unaobaki kwenye maeneo husika?
 
Asilimia kubwa ya waTanzania ni wezi ambao hawajapata fursa ya kuiba.....hayo makelele unayoyasikia sio uzalendo ni chuki ya kupitiwa mbali na mgao huo.......
Kama unafikili kuiba ni kitu chepesi hebu jaribu uone,utaishia kushindia mihogo ya kukaanga ya jero.
 
Mfano. Hizo kilo 7 au 8 mtu akiuza anapata zaidi ya 1.2B, sasa Kodi Analipa kiasi gani? Tuchukulie mfano alipe 200M Selikali Kuu ichukue 100M na hizo 100M zibaki halmashauri, sasa Kuna kilo ngapi za Madini zinachimbwa Kila siku? Kwa nini halmashauri hizo Maendeleo ni ya kuunga unga?
 
Hii kazi kweli kweli mwekezaji yaani ruksa kuwekeza kulipia kodi zote za uwekezaji halafu wachimbaji yaani ruksa kuchimba na kulipia Vibali na kodi zote za uchimbaji ila ukipata dhahabu ukieondoka nayo kwenda kutafuta soko hapana ni Mali ya umma wewe ni mwizi unatuibia madini yetu unatorosha madini sasa kwani walipewa vibali vya kuchimba nini ???? Sato ama ???mi sielewi hapa
 
Ninachoshangaa mbona wilaya na majimbo yenye Madini kama Dhahabu hakuna Maendeleo wakati Kodi zinazokatwa kwenye Madini hayo ni Kubwa shida ni nini? Au hakuna mgao unaobaki kwenye maeneo husika?
Mgao ni wa taifa wanafaidika na miradi ya CSR zaidi......

Kumbuka maduhuli yote yanakwenda serikalini
 
Serikali wilayani Ulanga mkoani Morogoro imewakamata watu saba akiwemo mwekezaji mzawa Junior Kasanga na raia wawili wa China kwa tuhuma za kutorosha madini ya dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni 337.5 kutoka katika mgodi uliopo kijiji cha Isyanga wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngolo Malenya, amesema kuwa dhahabu iliyokamatwa ina uzito wa gramu 2,640 sawa na kilogramu 2.64 ambapo amebainisha serikali bado inaendelea kuwafuatilia wawekezaji wengine ambao wamekuwa na tabia ya kutorosha madini na kusababisha kupotea kwa mapato ya serikali.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Migodi wilaya ya Ulanga, Edward Ngulinja, ameeleza awali wawekezaji hao walifika katika ofisi ya madini ya wilaya hiyo kwa ajili ya taratibu za kisheria ndipo walipo watiliashaka kuwa kuna udanganyifu wanafanya na kuvitaarifu vyombo vya ulinzi na usalama.

Chanzo Eatv
 
Ulangw nako kuna dhahabu? Nchi hii yote ina dhahabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…