Jurgen Klopp, kila lenye mwanzo lina mwisho!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Agosti ya mwaka 1991 Jemedari na kiongozi shupavu wa iliyokuwa USSR Mikhail Gorbachev alishuhudia zama za mwisho za umoja ule, katika yale majaribio ya mapinduzi dhidi yake yalimpa dalili mbaya na ishara ya mwisho wa zama za USSR, ndiyo, kila kucha ndefu ilianza kuonekana pale, kila mwiba ulianza kuchoma kila mguu kuashiria hakuna nyendo tena katika umoja ule.

2023 mwamba wa kijerumani Jurgen Norbert Klopp anapangusa miwani na kushuhudia zama za mwisho za liverpool yake pale merseyside jijini Liverpool, ni ukweli mchungu usiotakiwa na mwana liverpool yeyote yule, ukweli ambao kifikra unaumiza na kuchoma mithiri ya uji wa moto kwenye ngozi ya mwanadamu, kushuhudia mwanzo wa mwisho wa zile zama zilizofanya liverpool iogopeke ulaya nzima, kuishuhudia mwisho wa hatari zote zilizokuwa zinatokea Anfield inaumiza sana.

Kwasasa sura ya Klopp inaonyesha utamati wa akili yake katika Liverpool, haamini tena mawazo yake, haamini tena leo yake huku matumaini juu ya kesho yake yakiwa hafifu mno.

Mwanafalsafa maarufu sana Afrika mashariki na kati, mwana majumuyi toka jamhuri ya watu wa Kenya Patrick Loch Otieno Lumumba aliwahi kusema, "haijalishi wewe ni mjuzi wakucheza au kuimba kiasi gani lazima ujue ni muda gani wa kuondoka katika jukwaa" akimaanisha tu watu watachoka tu, hata wewe muhusika unaweza choka na kukosa tena ubunifu nakujikuta unakuwa mtumwa wa matendo yako pasipo kujua, kwa ubora na historia nzuri ya Jurgen ni bora kukubali maamuzi ya nyakati na kukubali kukaa pembeni, kwenye soka wanafalsafa wanaamini hata uwe bora kiasi gani kuna nyakati yanahitaji mawazo mapya katika office uliyoizoea na ni vyema kukaa pembeni na kuruhusu wengine.

Kwasasa kamba iliyoshika tamaa pale Anfield ilishakatwa, funguo za matumaini hazifungui kitasa chochote kile, hata lile jukwaa la the kop end imani imetoweka, pale kwa Bill shanky napo sura zinapoteza bashasha kila iitwayo leo, subira haivuti heri tena ndani ya liverpool.

Liverpool imepoteza matumaini kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mpaka uwanjani, imepoteza nguvu ugenini mpaka nyumbani pale palipokuwa machinjio ya wengi, alipokufa barca, city na vigogo wengine kwasasa anashinda brighton, forest, newcastle nk, sio hatari tena, ule msitu utishao sasa unafuga ndege wa mapambo tu, hakuna anayetishika nako tena.

Nyakati zimemsaliti Klopp, nyakati zinaihukumu sana Liverpool, mateso wanayopitia sio yale walioyataraji wala kuyafikiria, maisha yamekuwa machungu kwao mithiri ya wahalifu kule el salvador.

Ni wakati sahihi wa Jurgen kuangalia kioo na kumuona adui yake, wana falsafa wanasema adui mkubwa wa maisha yako ni wewe mwenyewe, utakaposhindwa kuyabadilisha yaliyokuwepo hunabudi kubadilika wewe, ni muda sasa wa Jurgen kuumaliza mwendo ndani ya Anfield.

Kila lenye mwanzo lina mwisho Jurgen

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ile mechi ya juzi aliyoatandikwa nne na manchester city muda mwingi nilikuwa namfuatilia yeye na benchi lake wanavyopokea reaction ya kufungwa

Umeongea ukweli muda umemtupa mkono Kloop na bahati mbaya miaka zaidi ya tisa kwa timu ile kuchukua EPL moja ni aibu kubwa

Kombe la uefa ndilo linambakisha angeshatimuliwa
 
Uko sahihi kiongozi wangu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Bonge moja la makala kumuhusu huyu mwamba, aachie ngazi kabla hajatolewa kwa kufedheheshwa
 
Ukizungumzia zama unamaanisha kipindi kirefu angalau miaka 10, sasa Liverpool lini walikuwa na zama za mafanikio ya kisoka Ulaya chini ya Klopp?
 
Unaongea kirahisi mnoo,,,bora hiyo mara moja kwa miaka tisa,,umeshasahau walikuwa na ukame nalo kwa miaka 30,,,acha uchambuzi na ujuaji uchwara kaka!!!
 
Bonge moja la makala kumuhusu huyu mwamba, aachie ngazi kabla hajatolewa kwa kufedheheshwa
Wewe,
Ninachokifahamu mimi ijapo sijafuatilia mkataba wake utaisha lini,Klop hawezi vunja mkataba,wavunje Liverpool wenyewe.

Labda km ni moja ya masharti ya mkataba wake sawa.

Pesa ni tamu.
 
Bonge moja la makala kumuhusu huyu mwamba, aachie ngazi kabla hajatolewa kwa kufedheheshwa
Pesa haijawahi kujaa mkuu, Hawa watu Wana pesa nyingi lakini lini umeskia kocha anajiuzulu mwenyewe kulinda heshima???

Hawa hata wakiona kazi hawawezi wanasubiri kutupiwa virago walipwe rundo la fedha zilizobaki kwenye mikataba yao
 
Pesa haijawahi kujaa mkuu, Hawa watu Wana pesa nyingi lakini lini umeskia kocha anajiuzulu mwenyewe kulinda heshima???

Hawa hata wakiona kazi hawawezi wanasubiri kutupiwa virago walipwe rundo la fedha zilizobaki kwenye mikataba yao
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ndugu yangu huwa sina ujuaji labda univunjie heshima tu

Nimesema miaka tisa kwa kikosi kile cha liverpool kuchukua EPL mara moja ilikuwa ni aibu kubwa sana

Lazima tukiri kloop ni mtu wa kuchukulia mambo poa ndio kilichomkost

Hasimu wake aliyemtesa Pep,hana ujinga huo ukikifanya makosa ya kijinga utakaa nje atatafuta mbadala mwingne

Angalia wachezaji aliowasajili kloop na anaewaongezea mkataba na anaowaruhusu waondoke hata shabiki wa kawaida tu anaona kocha anakosea

Kloop amefikia pick na lazima atashuka zaidi ya hapa asipoondoka mashabiki watamchoka
Unaongea kirahisi mnoo,,,bora hiyo mara moja kwa miaka tisa,,umeshasahau walikuwa na ukame nalo kwa miaka 30,,,acha uchambuzi na ujuaji uchwara kaka!!!
 
Umenena vizuri sana kiongozi Klopp hayuko serious kwenye management yake klabuni

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Narudia tena acha kuchukulia mambo kirahisi Kaka!!!Shida ya watanzani kila mtu mjuaji,, kila mtu mchambuzi kwamba wewe unajua sana kuliko huyo klopp na menejimenti ya livapuli??
 
Mimi inawezekana sijui ili matokeo ya team management yanaonekana wazi nje na ndani ya uwanja

Kiukweli kloop katika hilo amefeli! Kocha makini angejifunza kutokana na makosa lkn yeye aliendeleza business as usual

Unazidiwa ubingwa kwa point moja unarudia tena msimu mwingne unazidiwa ubingwa kwa point moja hapo utasema kocha yupo serious?

Unamsajili Ox ameshindwa kuimprove hata msimu mmoja kwanini usimtoe ununue mchezaji mwingne?

Huo ujinga hauwezi kufanywa na makocha elite wengine

Kloop anajificha kwenye bajeti ndogo ya usajili je hao wachezaji aliowasajili km
OX
Keita
Thiago
Timikas
Na wengine wameisadiaje timu kabla ya kulalamika bajeti ndogo

Kloop bila shaka ni mtu mzuri katika kuishi vizuri na wachezaji ila kwenye group management anapata shida


Narudia tena acha kuchukulia mambo kirahisi Kaka!!!Shida ya watanzani kila mtu mjuaji,, kila mtu mchambuzi kwamba wewe unajua sana kuliko huyo klopp na menejimenti ya livapuli??
 
Mara ya mwisho,usipende kuuchambua mpira kwa mawazo mepesi kiasi hicho!!
 
Sahihi kabisa kama alivocheza kagame wale Woote alioanza nao KAZI kawapunguza na kuwapangia majukumu mengine ,ofisini kwake na Chama chake kajaza vijana ilisasa wamwambie mambo Sasa ...... Clop atafute njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…