Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,609
Agosti ya mwaka 1991 Jemedari na kiongozi shupavu wa iliyokuwa USSR Mikhail Gorbachev alishuhudia zama za mwisho za umoja ule, katika yale majaribio ya mapinduzi dhidi yake yalimpa dalili mbaya na ishara ya mwisho wa zama za USSR, ndiyo, kila kucha ndefu ilianza kuonekana pale, kila mwiba ulianza kuchoma kila mguu kuashiria hakuna nyendo tena katika umoja ule.
2023 mwamba wa kijerumani Jurgen Norbert Klopp anapangusa miwani na kushuhudia zama za mwisho za liverpool yake pale merseyside jijini Liverpool, ni ukweli mchungu usiotakiwa na mwana liverpool yeyote yule, ukweli ambao kifikra unaumiza na kuchoma mithiri ya uji wa moto kwenye ngozi ya mwanadamu, kushuhudia mwanzo wa mwisho wa zile zama zilizofanya liverpool iogopeke ulaya nzima, kuishuhudia mwisho wa hatari zote zilizokuwa zinatokea Anfield inaumiza sana.
Kwasasa sura ya Klopp inaonyesha utamati wa akili yake katika Liverpool, haamini tena mawazo yake, haamini tena leo yake huku matumaini juu ya kesho yake yakiwa hafifu mno.
Mwanafalsafa maarufu sana Afrika mashariki na kati, mwana majumuyi toka jamhuri ya watu wa Kenya Patrick Loch Otieno Lumumba aliwahi kusema, "haijalishi wewe ni mjuzi wakucheza au kuimba kiasi gani lazima ujue ni muda gani wa kuondoka katika jukwaa" akimaanisha tu watu watachoka tu, hata wewe muhusika unaweza choka na kukosa tena ubunifu nakujikuta unakuwa mtumwa wa matendo yako pasipo kujua, kwa ubora na historia nzuri ya Jurgen ni bora kukubali maamuzi ya nyakati na kukubali kukaa pembeni, kwenye soka wanafalsafa wanaamini hata uwe bora kiasi gani kuna nyakati yanahitaji mawazo mapya katika office uliyoizoea na ni vyema kukaa pembeni na kuruhusu wengine.
Kwasasa kamba iliyoshika tamaa pale Anfield ilishakatwa, funguo za matumaini hazifungui kitasa chochote kile, hata lile jukwaa la the kop end imani imetoweka, pale kwa Bill shanky napo sura zinapoteza bashasha kila iitwayo leo, subira haivuti heri tena ndani ya liverpool.
Liverpool imepoteza matumaini kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mpaka uwanjani, imepoteza nguvu ugenini mpaka nyumbani pale palipokuwa machinjio ya wengi, alipokufa barca, city na vigogo wengine kwasasa anashinda brighton, forest, newcastle nk, sio hatari tena, ule msitu utishao sasa unafuga ndege wa mapambo tu, hakuna anayetishika nako tena.
Nyakati zimemsaliti Klopp, nyakati zinaihukumu sana Liverpool, mateso wanayopitia sio yale walioyataraji wala kuyafikiria, maisha yamekuwa machungu kwao mithiri ya wahalifu kule el salvador.
Ni wakati sahihi wa Jurgen kuangalia kioo na kumuona adui yake, wana falsafa wanasema adui mkubwa wa maisha yako ni wewe mwenyewe, utakaposhindwa kuyabadilisha yaliyokuwepo hunabudi kubadilika wewe, ni muda sasa wa Jurgen kuumaliza mwendo ndani ya Anfield.
Kila lenye mwanzo lina mwisho Jurgen
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app