LGE2024 Jussa: Chama cha upinzani chenye muelekeo ni ACT- WAZALENDO

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amewaomba wananchi wa Mtaa wa Komesho, Kata ya Msambweni, Jimbo la Tanga Mjini na vijiji vya jirani kuwaamini wagombea wa chama hicho kwa kuwapigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Komesho, Jussa amewahakikishia wananchi kwamba wagombea wa ACT Wazalendo wameandaliwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi na wataongozwa na dira ya ilani ya chama hicho iliyotengenezwa maalumu kwa uchaguzi huu.

Soma pia: Lema: CCM wanakaa vikao na ACT Wazalendo ili kukifanya kuwa Chama Kikuu cha Upinzani nchini na kuondoa hadhi yetu

Jussa amesisitiza kuwa chama chake kimejipanga kulinda kura za wananchi ili kuhakikisha matokeo halali. Pia aliongeza kuwa viongozi wa ACT Wazalendo watawajibika kwa wananchi na kwamba mwenyekiti yeyote atakayeshindwa kutimiza majukumu yake, chama kitamwondoa kabla ya hatua za wananchi.

Chanzo: Jambo TV
 
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amewaomba wananchi wa Mtaa wa Komesho, Kata ya Msambweni, Jimbo la Tanga Mjini na vijiji vya jirani...​
Uwanja wa michezo ya kisiasa ungekuwa huru, haki na nia ya dhati haya maneno yangekuwa ya kweli. Vinginevyo ni mwamba ngozi huvutia kwake.
 
Wakuu,

Back
Top Bottom