Kwanza inawezekana sana.
Kama hamna aliye attracted na mwenzake kuwa marafiki hakutobadilisha hilo. Mtapendana, mtaelewana, mtajaliana ila kila mmoja atapenda kwingine kimapenzi. Na hii ni kwasababu unaweza kumpenda mtu (fikra/mawazo/tabia yake/ushawishi wake) bila kuvutiwa nae kimapenzi.
Pili Kama mmoja anavutiwa na mwenzake hata wasingekua marafiki bado upo uwezekano mkubwa tu kwamba angevutiwa nae, na kama uwezekano wa kuwa nae nao ungekuwepo basi wangekua pamoja. Sasa bora kipi. . . kufall inlove with your (best) friend, mtu ambae mnafahamiana zaidi ya watu wengine wavyofahamiana au mtu tu anaeibuka out of nowhere?
Alafu kama hujagundua jaribu kuchunguza msichana na mvulana ambao ni marafiki wazuri/wa karibu sana huku wakiwa wana wapenzi wao. Utagundua kwamba kwa kiasi kikubwa wale wapenzi na bestfriend ni tofauti kabisa. Kama rafiki ni mchangamfu/mchokozi chokozi sana utakuta mpenzi ni mpole, kama mpenzi sio mtu wa movie/music kwa sana utakuta rafiki anapendelea. Kwa maana nyingine watu(sio wote) hua wanakua na marafiki wenye yale wasiyonayo wapenzi wao/yanayowavutia kua mpenzi na mtu ni tofauti na yanayowavutia kwenye urafiki. That way anatengeneza balance. . . akichoka kukaa nyumbani na kuboreka na mpenzi anamtafuta rafiki yake achangamke kidogo, akichoka na maneno mengi kwa mpenzi anamtafuta rafiki yake akili itulie kidogo.
So ndio inawezekana kuliko ambavyo watu wanapenda kukubali.