Justi bieber ni noma, hivi ndo alivyoamua kulifanya gari lake. Cheki hapa

Justi bieber ni noma, hivi ndo alivyoamua kulifanya gari lake. Cheki hapa

mijitu mingine bana sijui huwa tunatoa maoni kwa kujifanya sisi ni wasafi sana? yaani pesa nitafute mimi matumizi mnipangie nyie?? hii imekaaje?? na zikiisha mtanisaidia tena kuzitafuta? ebu mmpeni break mtoto wa watu atumie anavyotaka zikiisha atatia akili za wapi kuzipata na kuliko kubwabwaja hapa, tunatofautiana hapa duniani, justin anavyotoa hiyo misaada ya watoto yatima huwa habari hizo huwa hamzifuatilii kabisa. kipindi kako 16 tu kalitoa pesa nyingi sana kwenye matatizo ya haiti na hadi akaenda kule leo mnamuona eti ni mtoto hajui kutumia pesa, zenu mmezifanyia nini pamoja na hicho kiduchu mlichonacho??? fanyeni kazi

Asante, watu umbea umewajaa tu.
 
Wewe ndio unaoneakana stupid,kwanini mabilion mliyonunulia ndege ya raisi inayoharibika kila wiki msisaidie yatima,kwanini mabilion mliyonunulia Radar kwa hasara msisaidie yatima,kwanini mabilion mliyoficha uswiswi msisaidie yatima,kwanini mabilion ya safari za raisi kila wiki msisaidie yatima? Hizo milion 300 za mtu alizozitafuta kwa jasho lake akitumia ndio unamuona stupid? fikiria mara mbili acha wivu wa ajabu, matumizi ya hela yanategea ni wapi na ni nani na kwa muda gani.
Mkuu ray05 wewe unazungumza maneno ya kipumbavu kwani mimi ni kiongozi wa Serikali yenu ya Tanzania? mimi na Siasa zenu za kipuuzi wapi na wapi mkuu? Umekwenda shule mpaka darasa la ngapi wewe?
 
1549406653428.png
 
Mkuu Anheuser Ningelikuwa ni mimi Mwenye hizo Pesa ningeliwasaidia watoto yatima duniani wasiokuwa na Baba na Mama Huyu ni Stupid hana akili angelikuwa na akili asingeweza kuipamba gari kesho au kesho kutwa inakula mzinga Heavy. Je wewe Ungelikuwa na hiyo Pesa kama hiyo ungelifanyia kitu gani?
Siyo kazi yake kusaidia wala siyo wito wake. Acha aishi atakavyo
 
Wewe hiyo hela ungefanyia nini cha ki utu uzima, ungejenga visima kijijini kwenu?

Watu walioko dunia tofauti wana mahitaji tofauti.

Wewe unafikiri ningefanyia mtaji, ningejenga nyumba, ningetoa msaada wa kujenga visima... wengine hawana mahitaji hayo!!!
Hahaaaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom