Justice for Mbalamwezi wa "The Mafik"

Justice for Mbalamwezi wa "The Mafik"

pinno

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,213
Reaction score
1,229
Huyu dogo amekwenda,
Ni kweli historia yake ya matukio huko nyuma, mfano tukio la wizi, lililoandikwa hapo nyuma, na visa kadhaa kama hizo watu wanasema za skendo za kusepa na wake za watu, zinamfanya aonekane kama ni halali kwa yaliyomkuta.

Ila kila binadamu ana haki ya kuishi, na kama ni kuhukumiwa ahukumiwe kwa misingi ya sheria za jamhuri, na Mwenyezi Mungu mwenyewe,

So naona msiba wa dogo unataka kupita kimnya kimnya, had sasa police wapo kimnya na hakuna update zozote za uchunguzi unaoendelea, Tumeona video na mahojioano ya key people kwenye hii ishu, maelezo mengi yanajikangaja na kuacha maswali mengi.

Tuseme labda jeshi la police lilikuwa busy na ishu ya SADC, sasa imeisha, tunaomba tafadhali, uchunguzi wa kifo cha kijana huyu uanze mapema, na wahusika wote wapelekwe mbele ya haki.
 
Polisi wakiamua kufanya kazi mbona dakika 0 tu, ila sasa wana mengi je na hilo ni priority? hapo ndo gogoro inakuja. Mambo sasa vipi dogo kaondoka na harufu ya kutolewa uhai fanya uchunguzi toa taarifa kwa umma. Hongera kwa sadc umefanya kazi njema ingawa bodaboda pasua kichwa walikuwa wanakatisha mjini baadhi ya mitaa!! ila umejitahidi. sasa bado hili kamanda mwenye sifa kuliko ma rpc woote nchini kama ulivosema mwenyewe pale cloud - tuthibitishie ondoa haka kawingu! ahsante
 
Intelijensia yangu inanambia mtoa mada unajua baadhi ya hints za kifo cha huyu jamaa sema ndio hivyo humu ni JF
 
Kama una clue kuhusu chanzo cha kifo unaweza kuwajuza polisi utakuwa umesaidia.
 
ingekuwa hili tukio limetokea USA au nchi za wenzetu huko majuu mtuhumiwa angekuwa ameshapatikana.
Ila Bongo sasa tunakwama wapi?
 
ingekuwa hili tukio limetokea USA au nchi za wenzetu huko majuu mtuhumiwa angekuwa ameshapatikana.
Ila Bongo sasa tunakwama wapi?
Some things should stay unsaid. Kama wata deal na wahusika kimya kimya ni poa zaidi kuliko kuvuta attention!

Najua wanafanya kazi ila sio lazima watangaze.. Labda mpaka hatua za mwisho!!

Kwa ufupi tu, modus operandi ya polisi sio ya kutangaza tangaza. Ikitokea wametangaza basi ni final level kabisa au ni nyavu wanatupa kukamata samaki.

Nina amini, kama lipo la kusikia na kujua tutajuzwa tu. Otherwise, let karma work - Si malipo yote ni hapa hapa!
 
Kupata kubaya sana tangu dahari kunamaliza roho zetu tuendako ndio kunatisha sana,jamaa alikua na kipaji sana ndio maana hakua muongeaji kama wenzie.
 
Back
Top Bottom