Justice for Mbalamwezi wa "The Mafik"

Justice for Mbalamwezi wa "The Mafik"

Huyu dogo amekwenda,
Ni kweli historia yake ya matukio huko nyuma, mfano tukio la wizi, lililoandikwa hapo nyuma, na visa kadhaa kama hizo watu wanasema za skendo za kusepa na wake za watu, zinamfanya aonekane kama ni halali kwa yaliyomkuta.

Ila kila binadamu ana haki ya kuishi, na kama ni kuhukumiwa ahukumiwe kwa misingi ya sheria za jamhuri, na Mwenyezi Mungu mwenyewe,

So naona msiba wa dogo unataka kupita kimnya kimnya, had sasa police wapo kimnya na hakuna update zozote za uchunguzi unaoendelea, Tumeona video na mahojioano ya key people kwenye hii ishu, maelezo mengi yanajikangaja na kuacha maswali mengi.

Tuseme labda jeshi la police lilikuwa busy na ishu ya SADC, sasa imeisha, tunaomba tafadhali, uchunguzi wa kifo cha kijana huyu uanze mapema, na wahusika wote wapelekwe mbele ya haki.
Mentally ya kupigania haki iendelee, Laiti tungeungana na wenzetu kupaza sauti kwenye ukatili walioufanyiwa tungekuwa na sauti kubwa sana saa hii.
 
si waswahili wanadai mauaji yake yametokana na kisa cha kimapenzi?.

kama ni hivyo, kumbaini muuaji wake ni kazi rahisi sana.

nahisi polisi hawajaamua ila wakiamua waanze kutrace mawasiliano yake ya mwisho ya simu.

nina hakika yatawapeleka moja kwa moja kwa mwanamke aliyekuwa ana date naye halafu baada ya hapo wachunguze wanaume wengine ambao mwanamke huyo alikuwa anatokanao kimapenzi.
kazi itakuwa imeisha.
 
Hiv kuna usalama kweli nchi hii

Kamanda sirro, uweledi upo wapi? Kila siku kufuatana fuatana ktk misafara ya Rais na huku majukumu yenu hamfanyi

Hatusemi msiambatane na mkuu wa nchi ila tunataka kuona mnapambana na wahalifu na kutuhakikishia usalama sisi raia

Had leo hii ni takribani siku 60 na kitu, hakuna lolote jamii imesikia juu ya kukamatwa au hata tu kuhusishwa au update yoyote juu ya huyu dogo wa the Mafik, msanii MBalamwezi

Au ndo ukweli kuwa mnajihusisha na kesi zenye kiki zaid ? Kwamba kwa kuwa dogo alikuwa ni msanii anaechipukia, ambae hajapata jina bado ndo maana mnapotezea?

Justice for Mbalamwezi
 
Back
Top Bottom