Justice Rutenge: Dira ya Taifa inapaswa itokane na Sauti, Mawazo, Mitazamo na maoni ya Wananchi

Justice Rutenge: Dira ya Taifa inapaswa itokane na Sauti, Mawazo, Mitazamo na maoni ya Wananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Screenshot_20240823-160325.jpg
Washiriki zaidi ya 500 kutoka Asasi za Kiraia (AZAKI), Sekta Binafsi, Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajiwa kushiriki maadhimisho ya Wiki ya AZAKI 2024, itakayofanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 Jijini Arusha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Agosti 23, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, amesema kuwa, wiki hiyo imebebwa na kauli mbiu ya Sauti, Dira na Thamani, ikiendana na wakati uliopo na matukio yanayoendelea nchini, ambayo ni pamoja na uchaguzi wa Serikali za mtaa utakaofanyika Mwaka 2024, Uchaguzi Mkuu wa mwakani na Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Screenshot_20240823-161132-1.jpg
“Tupo kwenye kipindi muhimu sana kwenye demokrasia yetu kama nchi, kwa sababu mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mtaa, wote mnafahamu, pia mwakani tuna Uchaguzi Mkuu.

"Jambo la kipekee sana, mwakani tunatarajia kuzindua Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo ni fursa adimu sana inayokuja mara moja kwa muda mrefu.

"Fursa hii kutokana na umuhimu wake si budi sauti za wananchi zikasika kuchangia maoni yao wenye, kwani dira ya Taifa inapaswa itokane na sauti, mawazo, mitazamo na maoni ya wananchi," amesema Rutenge.

Aidha, Rutenge ameongeza kuwa, wiki hiyo pia itakuwa na mijadala mbalimbali inayohusu shughuli za AZAKi nchini, maendeleo ya jamii na ushirikiano baina ya Asasi za Kiraia, Serikali na sekta binafsi.
Screenshot_20240823-160614.jpg
Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulika kusaidia na kuwezesha watu wenye ulemavu wa macho nchini (CBM), Nesia Mahenge, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya AZAKi 2024, amesema kuwa kuelekea katika wiki hiyo maandalizi yamekamilika, ambapo amewashukuru wadau wote waliojitokeza kudhamini na kuwezesha maadhimisho hayo.

Soma Pia: Prof. Kitila Mkumbo: 81% ya waliotoa maoni kwenye Dira ya Taifa 2050 ni vijana

Aidha, Mahenge ameeleza kuwa, katika wiki hiyo itayaleta pamoja makundi mbalimbali ikiwemo vijana, jamii, makundi maalum na wadau mbalimbali watakaojadiliana kwa pamoja mada zinazohusiana na kaulimbiu ya maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya wiki ya AZAKi 2024 ni ya sita kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018.
 
Huyo binti mwenye koti la light blue, blauzi nyeusi na shanga nyeupe shingini ndio Mahenge??
Anyways.....
Yaani wakati anatoka ndani hakuweza kujiangalia hata kwenye kioo walau apunguze urefu wa wanja..🤣
Na wenzake walivyo na roho mbaya wakamuacha tu bila kumwambia ili khali walitambua picha zitatoka kwenye media..😂
 
Ila kuna wananchi wengine wana maoni/hoja/mawazo ya ajabu.
Fuatilia dira huko mikoani utaona vituko.
Mfano kuna mmoja ali suggest "umri wa kuoa na kuolewa mwisho 35 yO.
Kuna mawazo watu wanatoa hadi mtangazaji au mchukua maoni anacheka na ku skip.
 
Back
Top Bottom