Juu wanazidi kukipromoti kiswahili, huku chini walimu sasa wanapewa barua za vitisho za kuhakikisha kiingereza kinazungumzwa mashuleni; imekuwa shida!

Juu wanazidi kukipromoti kiswahili, huku chini walimu sasa wanapewa barua za vitisho za kuhakikisha kiingereza kinazungumzwa mashuleni; imekuwa shida!

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Ilianza rasmi kipindi cha mh. jpm (r.i.p) ambapo kiswahili kilitamalaki kufikia kutumika kisawasawa afrika.
Juzi hapa tena mh. Mwigulu alipokuwa anasoma bajeti, alikipromoti tena kwa kusema usaili fulani (nimesahau eneo rasmi alilolitaja) utakuwa unafanyika kwa kiswahili sasa na si kiingereza tena.

Ifahamike kuwa, kwa sasa, shule nyingi hususani hizi zetu za kata, somo la kiingereza limekuwa somo gumu kwa wanafunzi kama ilivyo hesabu. Na mbaya zaidi, sasa hivi kuna uhaba wa walimu wa kiingereza humu mashuleni kuliko somo jingine lolote.

Hamasa hizi za kutumia na kukitukuza kiswahili zinawapa amani na morali sana wanafunzi kwani wanachukia haswa habari za kulazimishwa kuzungumza kiingereza; jitihada ya kujifunza inapotelea mbali huko na jitihada za walimu za kuwalazimisha madenti wazungumze hicho kiingereza nazo pia zinadidimia. Habari za kuveshana mabango 'I will never speak kiswahili again' yamepotea kwa kasi.

Wakati hayo yanaendelea huko kama hivyo, huku mashuleni nasikia kunatembea vitisho kwa waimu kuwa wakishindwa kuwazungumzisha wanafunzi wao kiingereza basi wajitathimini katika nafasi zao.

Lishikwe lipi haswaa?!!!!
 
Kwanza kabisa kama kiswahili kikuamua kitumike kitumike kingereza kiwe ni hiyari ya mtu mwenyewe kuwe na kozi kwaajili ya kingereza kwa wale wanaotaka kuajiriwa ulaya
 
Back
Top Bottom