Juu ya ajali mbaya ya maskini_jeuri

MJ,

POle sana.. ni kweli kwamba una wakati mgumu sana lakini cha maana ni wewe kuvaa ujasiri, kuface kila kilicho mbele yako na kuomba nguvu za mungu.. saidia familia ya merehemu na saidia jamhuri, ila cha maana kuliko vyote.... weka karibu familia yako

Tuko pamoja na nadhani utapata msaada zaidi (hali na mali) kutoka JF kwani sisi ni familia
 

maombi yetu yako pamoja na wewe hili lipite kwa salama
 
ooooo pole sana MJ maisha ndivyo yalivyo naamini kila kitu kitakwenda sawa pia usimwache Mungu atakutetea kwani yeye ni Hakimu wa haki.

RIP aliyetutangulia
 
Guys sio pole nyingi zinatolewa hapa,yeah nakubali kutoa pole kwa marehemu na pia hata bwana M_J ila pia mwishoni ni kuangalia njia gani ya kuweza kumsaidia bwana M_J kwa ushauri au hata kwa lolote lile ambapo ataweza kufanikiwa huko mahakamani maana mahakamani sio sehemu ya kuchezea isitoshe imetokea ajali na mtu kafa so tujaribu kuangalia kama kuna njia yoyote ya haraka haraka ya kumsaidia jamaa.Hapa sasa ndio ubinadamu unapoonekana sio kwenye raha tu kusifiana bila mpango wowote........Nawakilisha!!
 

asante sana kwa mawazo yako tukianza na wewe unatoa mchango gani kimawazo ?
 

ukiona mdau kaishia kutoa pole tu ujue huo ndio mchango wake na
angekuwa na la zaidi angeandika hapa jukwaani au angetuma
pm.

poles sana mj Mwenyezi Mungu akulinde na akuongoze katika kutatua
hili tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…