Juu ya kaburi la baba mdogo kuna nyumba imejengwa. Je, nifanye nini?

superbug, Kwani ukiacha hivyo hivyo na kuendelea na maisha utapungukiwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uchungu wa ndugu unaujua hapa tunatofautiana aisee mbaya zaidi unajua mwili wa ndugu yako uko pale umekaliwa kibabe au kitapeli maana nimeenda kuomba kwa unyenyekevu kufukua wamekataa kununua nyumba wamekataa what else mkuu?
 
Nao Naomba ufafanue mkuu hii sheria imenishangaza kidogo
 
Nao
Naomba ufafanue mkuu hii sheria imenishangaza kidogo
Ipo sheria inasema hivyo. Miaka 50 baada y mtu wa mwisho kuzikwa, eneo hilo ni public area na linaweza kutumika kwa chochote. Si makuburi tena.
 
Ipo sheria inasema hivyo. Miaka 50 baada y mtu wa mwisho kuzikwa, eneo hilo ni public area na linaweza kutumika kwa chochote. Si makuburi tena.
Ok ila mnapewa nafasi ya kutoa miili? Na je makaburi Kama Yale ya bibititi karibu na frimason mtu anaweza akanunua Lile eneo akajenga au Yale makaburi yanalindwa na sheria Fulani za malikale?
 
Kazi ipo...sasa ukichimba ukakuta wakati wa kuchimba msingi mafundi walikutana na mifupa, wakatupilia mbali, utajisikiaje??

Watoto wa bamdogo wapo, kesi kanunua mtoto wa bamkubwa...

Mleta mada lazima kuna kitu cha mambo ya mizimu ndiyo kinakusukuma, kutaka kufukua kaburi..

Maadam mnajua hiyo nyumba ni kaburi inatosha...mfanyie matambiko hapo hapo...marehemu tunaposema wapumzike kwa amani...tumaanishe kweli...

Everyday is Saturday....................... 😎
 
Unawaambia nini ndugu zetu wachaga wanaozika kwenye makazi yao ?
Hata wahaya ukienda kwao kila familia pembeni kuna makaburi. Kama ni makaburi ya ukoo au familia haina shida kama wewe ni mwanafamilia au ukoo! Lakini kwa mtu baki unauziwa kiwanja na makaburi?? Mbaya Iseee! Ujue wenye makaburi yao watakuwa wanakuja kukutembelea kufanya mambo yao! Ona Jacqueline Mengi anavyogombana na ukoo kisa kusalimia kaburi la mmewe Mengi! Makaburi ni sehemu yakuhabudia kwa makabila Mengi! Kama umejenga nyumba juu ya kuburi fahamu kwamba jina lake aliyelala kwenye kabuli likitajwa na ndugu zake lazima akushughulikie uliyejenga juu yake kama sio mwanaukoo
 
Huyo sio mwanaukoo kabisa ni mtu alikuja na pesa zake akawarubuni walioachiwa mji mwaka 1988 .
 
Matatizo mengine yanatokana na namna tunavyofikiri.

Fikira zetu zina uwezo wa kutengeneza matatizo ambayo hayapo
 
Hii dunia sehemu nyingi ni makaburi chief kama ulikuwa haufahamu, ni kujua ndio tatizo ila makaburi ya zamani mengi hayajulikani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ushirikina wewe, ndio maana Afrika hatuendelei kwa upuuzi wa watu kama nyinyi.
 
Achana na hizo habari mkuu, mtu akifa amekufa, mwili ni mzoga tu, utaoza utapotea maisha yataendelea.
 
Ok ila mnapewa nafasi ya kutoa miili? Na je makaburi Kama Yale ya bibititi karibu na frimason mtu anaweza akanunua Lile eneo akajenga au Yale makaburi yanalindwa na shria Fulani za malikale?
Just imagine ndugu waliokuwepo miaka 50 iliyopita wakati wa kuzika watakuwa na umri gani? Nani atafuatilia?

Na hapo ni wale wachache waliozika siku za mwisho mwisho.
 
Just imagine ndugu waliokuwepo miaka 50 iliyopita wakati wa kuzika watakuwa na umri gani? Nani atafuatilia?

Na hapo ni wale wachache waliozika siku za mwisho mwisho.
Sasa naelewa kwanini eneo la Msamvu stand karibu na uhamiaji na kwa Kimario kwenye kitimoto Hilo eneo lote la magesti na maloji ni makaburi na watu wamejenga Sana na hakuna anaelalamika.
 
Km umeelewa hivyo,fanya ishu za msingi achana na mishe za mifupa mkuu..
Sasa
Sasa naelewa kwanini eneo la msamvu stand karibu na uhamiaji na kwa kimario kwenye kitimoto Hilo eneo lote la magesti na maloji ni makaburi na watu wamejenga Sana na hakuna anaelalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kijiji nilichokulia shamba walilokatiwa na wakoloni kina babu na bibi, yalikuwa makaburi matatu...ila wakaishi badae yakafutika tukaanza lima kwa juu...maisha yakendelea, ila tukawa tunaambiwa ni yalikuwa hapa..

Ishu ni mtu akishakufa, hamna la ziada mkuu au unafikiri mifupa yake inaumia unayoililia? Maeneo mengi ni makaburi, usisahau hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli wa kihistoria lakini je ana uhakika kuwa kaburi lipo pale? Jambo la muhimu huyu bwana ni kwanza asome sheria ya kuhamisha makaburi No 9 ya 1969 ( an Act to provide for removal of Graves from land required for public purposes) na akipendezewa apate wakili mzuri wa sheria za ardhi nina imani atapata mifupa ya baba yake na kwenda kuiweka mahala salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…