Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
JUVENAL HABYARIMANA: MKOMBOZI ALIYEGEUKA KUWA DIKTETA UCHWARA, KIFO CHAKE CHANZO CHA MAUAJI YA HALAIKI (GENOCIDE) NCHINI RWANDA.
Na. Comred Mbwana Allyamtu
Wednesday- 18/7/2018
Mbinu za kiintelijensia zilizosukwa kwa ustadi mkubwa zilitumika kuifanya Rwanda kuwa uwanja wa damu mapema mwaka 1994. Ustadi huu ulisukwa mapema mwaka 1988 kule Ethiopia na kumalizika pale Enttebe Uganda lengo likuwa ni kuingia Kongo DRC kwenda kujinyakulia Mali bila vizingiti vyovyote. Hawakujua kuwa mpango ule unge leta madhara makubwa vile kama ilivyokuja kutokea usiku wa tarehe 6/4/1994 mpaka 15/5/1994 kwa kutapakaa kwa maiti nchi nzima. Mpango mkakati ulikuwa ni kumuondoa Idd Amini kule Uganda na kuweka kibaraka wao mpango ambao ulitimia tarehe 26/10/1986 kwa kupachikwa Museveni kupitia usaidizi uliofanywa na Tanzania kwa karibu kabisa.
Mpango mpya ni tutaingiaje Rwanda? Mkakati huu ulikuwa wa Kufurumisha utawala wa mtoto wa ubatizo wa Mobutu Seseseko aliye fahamika Kama Juvenal Habyrimana. Mwanzoni mwa mwaka wa 1990 kuliundwa chama cha RPF chini ya kiongozi wake Major General Fredy Gisa Rwigema aliyejalibu kuivamia Rwanda mwaka huo huo bila mafaniko Kwani aliambulia kipigo kikali kutoka vikosi vya askali wa Rwanda wakisaidiwa na vikosi vya ZDF kutoka Zaire ya Mobutu. Baada ya kukwama kwa njia hii mpango mkakati ulipanuliwa zaidi kwa Kagame aliyekuwa masomoni huko Marekani kurejeshwa kwa minajiri ya kuongoza kikosi cha wanamgambo wa RPF lengo ni kutekeleza operation ya siri (iliyofichika sana mpaka leo) kwa kuzishilikisha nchi kadhaa ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya na Ethiopia. Ambapo kupitia mkakati huu ilifanikisha Kagame kujinyakulia utawala kwa wepesi.
Wakati wa utekelezaji ulio ratibiwa na mataifa ya magharibi yakiingozwa na Marekani na Uingereza pamoja na washilika wao kutia ndani Ufaransa na Uberigiji mkakati huo unabaki kuwa nyakati isiyo saulika Kamwe nchini Rwanda Kwani maiti zisizo na hatia za makabila ya kitusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuwawa na maiti zao kutapakaa kwenye mitaa huko Rwanda na zingine kutupwa Kwenye mto Ruvuvu unaepeleka Maji yake kwenye mto kagera.
Habyimana ndio chanzo cha machafuko hayo yote ya kimbali huko Rwanda na hii ni baada ya ndege iliyokuwa imembeba kutunguliwa na watu wasiojulikana (bado kuna vuta ni kuvute ya nani hasa alihusika) wapo wana mtuhumu Kagame na kikosi chake cha RPF kuhusika jambo ambalo Kagame mwenyewe hukanusha japo dulu za ndani zikithibitisha RPF ndio ilihusika wakati Habyimana akitunguliwa.
Ilikuwa saa 2:20 usiku wa tarehe 6 Aprili 1994, ndege ya shirika la Ubelgiji C-130 Hercules, iliyokuwa ikipaa kila wiki, ikiwa imebeba kikosi cha askari wa umoja wa Mataifa cha UNAMIR, ilisubirishwa angani ili ndege ya Rais iweze kutua kwanza katika uwanja wa ndege wa mjini Kigali.
Ndani ya ndege hiyo ya Rais walikuwamo;
1.Juvénal Habyarimana, Rais wa Rwanda
2.Cyprien Ntaryamira, Rais wa Burundi
3.Bernard Ciza, Waziri wa kazi wa Burundi
4.Cyriaque Simbizi, Waziri wa mawasiliano wa Burundi.
5.Meja Generali Déogratias Nsabimana, Mkuu wa utumishi jeshi la Rwanda.
6.Meja Thaddée Bagaragaza, Mkuu wa kikosi cha "maison militaire" cha Rais wa Rwanda.
7. Kanali Elie Sagatwa, mjumbe wa sekretarieti maalum ya Rais wa Rwanda na mkuu wa baraza la kijeshi la Rais wa Rwanda.
8. Juvénal Renaho, mshauri wa masula ya kigeni wa Rais wa Rwanda
9. Dr. Emmanuel Akingeneye, Daktari binafsi wa Rais wa Rwandan
10.Jacky Héraud, Rubani (raia wa Ufaransa)
11.Jean-Pierre Minaberry, Rubani msaidizi (raia wa Ufaransa)
12.Jean-Michel Perrine (Injinia wa ndege, raia wa Ufaransa)
Wakati ikijiandaa kutua, makombora mawili ya kurushwa kutoka ardhini yalikatisha maisha ya watu hao 12 waliokuwamo ndani ya ndege hiyo aina ya Jet-Dassault Falcon. Kombora la kwanza likipiga ubawa mmoja wa ndege na kombora la pili likapiga mkia, kisha ndege hiyo ikiwa inawaka moto iliangukia kwenye bustani ya ikulu ya Rais.
Tukio hilo likawa mwanzo wa machafuko yaliyopelekea mauaji ya wanyarwanda zaidi ya laki nane (800,000) kwa siku mia moja pekee. Maana yake kila siku walikufa watu 8000.
Wanamgambo wa kihutu, walioitwa "Intarahamwe" wakisaidiwa na wanajeshi wa kihutu walitumia silaha za Jadi kuwaua watu wa kabila la Watutsi. Machafuko haya yaliibuka tu baada ya kuuwawa kwake Hbyarimana, raisi wa pili wa Rwanda wakati huo aliyechukua madalaka mwaka 1973 kwa mapinduzi baridi kutoka kwa Gregory kayibanda aliyekuwa raisi wa kwanza wa Rwanda.
Juvenal Habyimana ambaye ndie atakaye sadifu makala yangu hii ya leo ni rais wa pili wa Rwanda aliyetoka kabila la kihutu, aliingia rasmi madarakani siku ya Tare 5 July mwaka 1973. Kabla ya hapo alikuwa ni Jenerali katika jeshi la Rwanda akishikilia cheo cha Mnadhimu Mkuu wa jeshi kwenye serekali mpya iliyokuwa ikiongozwa na Gregory Kayibanda. Mapinduzi yaliyofanywa na Habyarimana kumuondoa madarakani Rais Gregoire Kayibanda hayakuwa mapinduzi ya kumwaga damu.
Mapinduzi haya yalipokelewa kwa shangwe na vifijo hasa maeneo ya mijini nchini Rwanda. Rais aliyepinduliwa, Bw. Kayibanda ilifika kipindi alianza kuchukiwa mno na wananchi kutokana na kushindwa kabisa kuituliza Rwanda na machafuko ya kikabila yaliyo kuwa yameota mizizi nchi nzima pamoja na kuiletea maendeleo badala yake aliendeleza visasi dhihi ya Watusi. Hii ilisababisha Rwanda kutengwa na majiranio zake, hasa jirani yao muhimu zaidi wa Uganda ambayo ilikuwa na Watusi wengi wanaoishi nchini humo. Hii iliathiri hata maendeleo ya Kiuchumi ya Rwanda.
Hivyo basi kitendo cha Jererali Jevenal Habyarimana kumuondoa madarakani Rais Kayibanda kilipokelekwa kwa furaha na wananchi wengi na Habyarimana alionekana kama shujaa. Japokuwa nimeeleza kuwa mapinduzi yaliyomuingiza madarakani Habyarimana hayakuwa ya umwagaji damu, lakini kati ya mwaka 1974 mpaka mwaka 1977 takribani watu hamsini na sita, hasa wale ambao walikuwa na nyadhifa za juu kwenye serikali iliyopita ya Kayibanda waliuwawa kwa maelekezo ya Habyarimana mwenyewe huku Rais aliyeondolewa madarakani Gregoire Kayibanda akifariki mwaka 1976 akiwa gerezani kwa sababu inayoelezwa ilitokana na kunyimwa chakula kwa muda mrefu (Nikipata wasaa ntawaandalia makala yake hapo siku za usoni).
Baada tu ya kuingia madarakani Habyarimana alivifuta vyama vyote vya siasa nchini humo akieleza kuwa hataki Rwanda iendekeze majibishano ya kisiasa kila siku badala ya “kuchapa kazi” na mara nyingine akituhumu vyama vya siasa kutumika na maadui wa Rwanda ili kuvuruga taifa. Mwanzoni wananchi karibia wote waliunga mkonmo msimamo wake huu. Lakini ajabu ni kwamba mwaka uliofuata baada ya kuingia madarakani, yaani mwaka 1975 Rais Juvenal Habyarimana aliunda chama chake cha siasa ambacho alikiita Mouvement Revolutionnaire National pour le Developpement (MRND) na kutangaza kwamba hicho ndicho kitakuwa chama pekee cha siasa nchin Rwanda.
Mwanzoni Habyarimana alipendwa na watu wa makundi karibia yote, yaani Wahutu na Watusi. Wahutu walimpenda kwa kuwa alikuwa ni Muhutu mwenzao na Watusi walimpenda kwa kuwa mwanzoni mwa uongozi wake baada ya kumpindua Kayibanda, alipiga marufuku sera ambazo mtangulizi wake alizitengeneza kwa ajili ya kuwapendelea Wahutu pekee. Watusi walifurahishwa sana na hatua hii. Kwa upande wa Wahutu wenzake japokuwa suala hili liliwaudhi lakini hapa mwanzoni walimvumilia na kuendelea kumuunga mkono kwa kuwa alikuwa ni mwenzao (Muhutu).
Kwa muda wote huu serikali ilikuwa chini ya jeshi, yaani hakukuwa na serikali ya kiraia. Jeshi ndilo lilikuwa serikali nay eye Habyarimana akiwa kiongozi mkuu wa nchi. Lakini kufika mwaka 1978 kulifanyika mabadiliko mengine ya kikatiba ambayo yalitaka kurejea kwa serikali ya kiraia. Kwa hiyo mwaka huo ukaitishwa “Uchaguzi Mkuu”. Haukuwa uchaguzi mkuu haswa kwa maana ya uchaguzi mkuu kama ambavyo unapaswa kuwa, kwa maana ulikuwa ni kiroja cha kuchekesha ambazo kilitoa taswira kwamba kuna harufu ya shari iliyo mbele. Ni kwamba kwa kuwa vyama vyote vya siasa vilipigwa marufuku nchini humo, hivyo basi MRND, chama cha Juvenal Habyarimana ndicho chama pekee ambacho kilishiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huo 1978 kwa kusimamisha wagombea na katika nafasi ya Urais kulikuwa na mgombea mmoja tu, Juvenal Habyarimana.
Siku ya Desemba 24 mwaka huo 1978 matokeo ya uchaguzi yalitangazwa ambapo Habyarimana alishinda ‘kwa kishindo’ akipata 98.99% ya kura zote na kuapishwa kuwa Rais wa Rwanda kwa muhula wa miaka mitano. Uchaguzi uliofuata miaka mitano baadae, yaani mwaka 1983 kwa mara nyingine tena, MRND kikiwa chama pekee cha siasa killichoshiriki uchaguzi huo na katika nafasi ya Urais Juvenal Habyarimana akiwa mgombea pekee, alipata tena ‘ushindi wa kishindo’ ambapo siku ya Desemba 19 matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa Habyarimana alipata ushindi wa 99.97% ya kura zote zilizopigwa. Kama hiyo haitoshi, miaka mingine mitanao tena baadae, yaani mwaka 1988 siku ya Desemba 19 matokeo yalitangazwa na kumpa tena Habyarimana ushindi wa 99.98% ya kura zote zilizopigwa huku MRND kikiwa chama pekee kilichoshiriki uchaguzi na Habyarimana akiwa mgombea peke wa nafasi ya Urais.
Watu wenye hekima na wanao ona mbali walianza kuhisi joto ambalo lilikuwa na dalili ya kurudi tena ndani ya Rwanda . Habyarimana hakuishia hapo tu, bali pia wafuasi wake wallianzisha utaratibu wa kufundisha raia mitaani kwa lazima nyimbo na tungo zilizotungwa kwa ajili ya kumsifu Rais Habyarimana pamoja na staili za kucheza nyimbo hizo. Katika mikutano yake ya siasa raia wa Rwanda walitakiwa kuimba nyimbo hizi za kumsifu na kucheza kwa staili ya kufanana kama ambavyo walikuwa wamefundishwa.
Kwa kifupi Rais Juvenal Habyarimana aligeuka kutoka kuwa ‘malaika wa ukombozi’ ambaye Warwanda walihisi ameshushwa labda kutoka juu na bila kupindisha maneno Habyariamana sasa alikuwa ni Dikteta.
Udikteta wake ulikuwa ni udikteta haswa… sio udikteta uchwara! Ilikuwa ni ngumu kuchora mstari kati ya chama chake cha MRND na pia nghumu zaidi kuchora mstari wa ukubwa wa madaraka yake ndani ya chama tawala cha MRND. MRND ndio ilikuwa serikali na Habyarimana ndiye alikuwa MRND. Kwa hiyo yeye ndiye alilkuwa serikali na yeye ndiye alikuwa chama tawala. Ofisi zote za serikali pia zilifanya kazi kama ofisi za MRND. Katika serikali za mitaa, ‘Maafisa Watendaji’ wa kata au vijiji au mitaa pia ndio walifanya kazi kama makatibu wa chama.
Kadiri ambavyo Habyarimana alikuwa anajivika utukufu na kukoleza makali yake ya udikteta ndivyo ambavyo hata watu wa kabila lake, Wahutu walianza kumchukia. Kama dikteta mwingine yeyote yule duniani, naye akaanza kufanya makosa ya kipuuzi kabisa ya kimkakati. Ati ili kuwafurahisha watu wa kabila lake, Habyarimana taratibu akaanza kurejesha sera za mtangulizi wake ambazo zilikuwa zinawabagua Watusi. Kwa mfano kwenye udahili wa vyuo vikuu au ajira za serikali, walirejesha vipengele ambavyo moja kwa moja vilikuwa vinamnyima fursa Mtusi.
Hili lilikuwa ni kosa kubwa kwake kwani watu wa kabila lake tayari walikuwa ‘watembukiwa nyongo’, wengi walikuwa hawamtaki na hata Watusi ambao walikuwa wanamuunga mkono nao wakamchukia kutokana na kurejesha sera za kibaguzi. Kwa kifupi alikuwa anaenda kinyume na misingi na sababu ambazo alizitumia kuhalalisha mapinduzi yake mwaka 1973 na vitu ambavyo vilifanya Wahutu na Watusi kwa pamoja kumpenda.
Tofauti na ambavyo nchii ilitulia mara baada ya Habyarimana kumpindua Kayibanda, lakini kutokana na udikteta wake na kutokubalika tena kwa wananchi, ‘order’ ilianza kupotea mitaani na taratibu chuki za kikabila ambazo zilikuwa zinawafurukuta watu zikaanza kumea tena upya. Na kuzuka upya kwa vuguvugu la ukombozi kutoka kabila la watusi yaliyokuja kuibua machafuko Ya kimbali ya mwaka 1994 yaliyoteketeza maelfu ya watu.
[emoji117][emoji420]Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
[emoji2400]Wako Mjoli wa Historia ya ulimwengu na diplomasia ya dunia......
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
[emoji2398] Copy rights of this article reserved
[emoji2400]written by Comred Mbwana Allyamtu
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com