Juventus Special Thread

Yani nahangaika kweli kutafuta namba ya agneli au Nedved. Mwenye nayo anitumie jamani. Maana mm naumia sana kumwona Bentancur anakaa nje anapewa nafasi kwa shida kweli wakati dogo ni pilau balaa. Huyu dogo atakuja kuwa kama Javi Martinez. Miaka 20 kupewa dimba mjini Turin si mchezo. Dogo ni kipaji ila inabidi ajengwe kujiamini tu.
 
Wadau mnaona balaa la Patrick Schick. Juve tulimnunua huyu baadae tukaleta figisu ooh anaumwa moyo mara sijui nn, mwisho wa siku Roma wamemnunua.
 
Grazie Fiorentina. Safi sana. Napoli shujaa wao aliyetufunga leo kawachoma mapema sana. Ubingwa si kuifunga Juve tu. Bado wiki ijayo anacheza na Sampdoria. Kibaraka wetu Quagliarela lazma awaue tu.
 
Hivi wadau msimu ujao Benatia asimame na nani pale nyuma. Maana yule jamaa kisiki haswa.
 
Naskia kocha kachomoa kwenda arsenal. Bora jamani, maana ile timu ingemzeesha kocha wetu. No 6 hawana, 4 na 5 shida tupu. Mzee angeingizwa cha kike tu.
 
Gigi Buffoni team captain wa Juventus Turin ametangaza kuachana na soka baada ya kuitumikia Juventus kwa miaka mingi. Buffon ambaye alinunuliwa kwa uhamisho uliovunja rekoni kwa makipa akitokea club ya Parma ametangaza uamuzi huo leo mbele ya waandishi wa habari.

Gigi amepata mafanikio mengi katika kipindi chake cha uchezaji. Kapata scudetto mara 7 mfululizo.
 
Juve ndio wameua mpira wa italia haiwezekani kila top player serie A anunuliwe juventus mmeua competition kabisa ligi haina mvuto ni sawa na ligue 1 na Bundesliga.... Huu upumbavu hauwezi kuukuta la liga yaani barca auze mtu madrid ama atletico auze madrid hakuna kitu kama hicho ndio mana bado kuna competition kwenye top 3 ila serie A ligi imekufa ssa higuain alikuwa tishio mkamchukua mkaiua nguvu napoli.... Benadetto cjui pjanic walikua wachezaji muhimu wa timu zao leo wote wako juve mpira hauna maana tena sio kama enzi zile ya AC milan ya kina seedorf ama juve ya kina Camoranesi na Inter ya kina zanetti walikuwa hawana huu upumbavu wa kuibiana wachezaji na ndio maana wakawa competitive mpaka mwisho ila leo hii kila mchezaji serie A anataka juventus kma shortcut ya kubeba champions league

R.I.P Serie A
 
Umesema ukweli mdau. Serie A inapita kwenye wakati mgumu sana. Match fixing nalo ni tatizo kwa soka la Italia. Upangaji wa matokea, hii kashfa imesumbua sana kwenye soka la italia kwa ngazi zote za ligi. A,B, na kule Serie C.
Miaka ile ya 80, 90 na mwanzo wa miaka ya 2000 mchezaji mkubwa alikuwa anapenda kucheza ligi ya italia. Ila kwa sasa wengi ni Laliga na Epl. Ila naona kama kuna mwanga mbele. Kuja kwa Ronaldo juve kutaongeza chachu kwa wachezaji wengine wazuri kutaka kucheza Serie A.
Ilikuwa ni nadra sana kwa mchezaji wa kitaliano kucheza nje ya italia. Ingawa walikuwepo wachache. Vilabu kama Parma, Sampdoria, Venenzia, Vicenzo na hata Bologna vilikuwa vikitoa upinzani mkali kwa kina Milan na Inter Milan. Lazio naRoma. Juventus na Torino.
Naamini kwa mwendo huu wa uwekezaji, serie A itarudia zama zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…