Juventus Special Thread

Marotta atangaza rasmi "the value of Pogba is immense and he will continue to be with us for many years".
 
Ngoja nimnyooshe Roma baadae nifukuzie nafasi ya Pili...
Pogba PSG Wakileta mpunga mna uwezo wa kukataa? Morrata anajiamini nini??

walete mara ngapi na bado watu wametoa nje.Mwaka juzi Juve walikataa mabilioni mangapi ya Bayern kwa Vidal tena huku wakiwa hoi kifedha?hujawajua vizuri Juve we endelea kuwafuatilia ili uwajue sera zao!Huwa hawapendi kupelekeshwa hadi waamue wenyewe!muulize Ibra,almanusra ashuke nao daraja 2006!yaani hadi mashabiki wake ni vichwa ngumu kama sie hadi leo tumo pamoja na dhoruba zote.This is Juventus bwana,sio Napoli!ngoja mchezee kichapo leo,ntachekaje!
 
We juve2012, na Mourinho, mbona huu uzi wenu hamwekagi mapicha? Nenda kule chelsik, manure, aseno man site, kote huko kuna mapicha kedekede. Wekeni mapicha bhana, uzi wetu na cc upendeze bhana.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo muda mkuu!huu uzi umejaa watu walio kwenye age ambayo kupata muda wa kutulia na PC ukafanya mambo hayo unayotaka ni vigumu.Tunadandiadandia juu kwa juu tukiwa kwenye daladala,lunch,e.t.c kuna siku nilikuwa nachati na Mourinho usiku saa 7 akaniambia yuko klabu ndio kapata muda wa "kupumzisha akili" huku akichati na kunywa "maji magumu" ha ha ha haa!sasa huyu unamtegemea akuwekee picha humu si anaweza kutupia picha za huko klabu halafu asubuhi akaamka ana ugomvi na mkewe,mods..na wale aliowapiga picha nao wakaamka wana magomvi huko kwao...aisee pweza usitafutie watu matatizo bwana!
 
Yah!saa hizi kichwa chake kizima ndio maana katupia picha zenyewe.ngoja ifike saa 6 halafu umpe hiki kibarua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…