Mourinho
JF-Expert Member
- Jul 24, 2012
- 4,619
- 2,327
unazungumziaje mechi ya leo mkuu!unaonaje nusu fainali tutapita kweli?
Mkuu kwa kweli nilikua naangalia highlights za Sevilla Vs Porto, kwa kweli wamenitisha kidogo kwa namna walivyokua wanashambulia kama mbwa mwitu toka dk ya 1
Kama tutakutana na Sevilla au Valencia/Basel (nadhani game bado inaendelea) nina uhakika wa kufika fainali,
Benfica ndio team ngumu sana, iko stable kwa muda mrefu, ina msimu mzuri domestically na wana uzoefu na kombe hili, halafu wanacheza mpira ambao huwa unatupa shida sana Juventus, wanajaa sana nyuma, ukuta mgumu, wanashambulia kwa kushtukiza na wana mawinga wanakimbia kama kicheche. Itabidi tuwe kwenye kiwango cha juu kuwafunga hawa.
Ndio maana naomba kukutana nao kwenye fainali, kwa sababu tutakua na extra motivation ya kushinda match