Juventus Special Thread

FT: Juventus 1-0 Monaco (Vidal pen 57)
Sio matokeo mabaya kabisa kwetu, clean sheet na goli moja la ushindi. Jumatano itawabidi tu Monaco wafunguke pale dimbani kwao kutafuta ushindi, na hapo ndipo kitawakuta kilichowakuta Dortmund

#ForzaJuve
 
Vp penalt tuliyopewa, Mimi naona kama ilikuwa soft sana. Mzee pirlo VP Leo kacheza kwa kiwango ulichotegemea?...
 
Arturo Vidal alikua nyota wa mchezo leo with 50 passes, 5 tackles won,5 shots (1 goal, 2 on target)
 
Vp penalt tuliyopewa, Mimi naona kama ilikuwa soft sana. Mzee pirlo VP Leo kacheza kwa kiwango ulichotegemea?...

Ilikua soft? How mzee?

Pirlo hakuwa na influence kubwa kwa kiwango chake nadhani ni kutokana na kutokua na match fitness, hata Marchisio hakucheza vizuri kama alivyocheza wakati Pirlo akiwa majeruhi.
 
Ongereni sana wazee wa Juve, naona mnakwenda second-leg mkiwa na pumzi za kutosha.

Ahsante Salamander, hawa watoto wanacheza defensive sana, sasa hiki kimoko kitabadili kabisa approach yao na hapo ndipo watakapokoma na sisi
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Salamander, hawa watoto wanacheza defensive sana, sasa hiki kimoko kitabadili kabisa approach yao na hapo ndipo watakapokoma na sisi

Mpira siku hizi umeharibika kabisa ( huu wa UCL), wachezaji badala ya kucheza wanafanya kazi ya kudefend mwanzo mwisho, utaona forward moja inakabwa na beki nne. Na filimbi nazo nyingi sana, mtu akiguswa tu anapepea kama karatasi.
 
Kwa umakini wa hali ya juu

Chumaa!

Forza Arturo

kibabu kimezidiwa maarifa kikaamua kucheza mieleka
Carlitos

No nonsense
 
Mpira siku hizi umeharibika kabisa ( huu wa UCL), wachezaji badala ya kucheza wanafanya kazi ya kudefend mwanzo mwisho, utaona forward moja inakabwa na beki nne. Na filimbi nazo nyingi sana, mtu akiguswa tu anapepea kama karatasi.

Itakua vizuri sana kama wataondoa ile sheria ya away goal, maana ile imechangia sana kwa baadhi ya team kupark mabasi
 
Itakua vizuri sana kama wataondoa ile sheria ya away goal, maana ile imechangia sana kwa baadhi ya team kupark mabasi

Si umeona game yetu sisi leo, tumecheza vizuri lakini draw ya 0 - 0 inatufanya tuwe hatarini kutolewa. Na ndio hayo hayo niliyosema, watu wamejazana chini tu wanapanda kwa kuvizia matokeo yake hakuna magoli. Mpira wa kipumbavu sana
 
Huyu Pirlo akiamua anaweza kucheza mpaka ana miaka 60. Jamaa anachofanya ni jogging tu, mpira unamfuata na anauamrisha kwenda anapotaka. Huyu jamaa hapewi heshima anayostahili
 
ni kweli pirlo ni MTU wa aina take...namkubali sana...akiwa anakimbia kama masihala
 
Vp penalt tuliyopewa, Mimi naona kama ilikuwa soft sana. Mzee pirlo VP Leo kacheza kwa kiwango ulichotegemea?...

-Ile penati ilikwa ni dhahiri kabisa.
-Hata kwa Real Madrid refa kakosea kutokutoa penat kwa Atletico.
-Torres kapiga chenga ya kwanza, anapiga ya pili huku azidi kumsogelea kipa Ramos anasogea njiani na kumpa mgongo, ilikuwa penalty kabisa ileee.
 
Si umeona game yetu sisi leo, tumecheza vizuri lakini draw ya 0 - 0 inatufanya tuwe hatarini kutolewa. Na ndio hayo hayo niliyosema, watu wamejazana chini tu wanapanda kwa kuvizia matokeo yake hakuna magoli. Mpira wa kipumbavu sana

-Kosa ambalo Real Madrid atakuja kujutia ni First Half, kacheza mpira mzuri na kupoteza nafasi nzuri.
-Kipindi cha pili Atletico wakaja nao wao kucheza mpira, nadhani kipindi cha kwanza hawakuamua kucheza mpira.
-Akiwa Away atakuwa anacheza mpira wa makini sana, Real sio rahisi kujituma akiwa kwao kama alivyojituma jana. Nadhani Diego Simeon ana lake jambo. Tumsubiri tuona atafanyaje. Ila hata yeye anaweza akaondoka tuu.
 
Hongereni sana wazee wa Juve ni mwanzo mzuri natumai marudio mtafanya vizuri na tutawaona semi- final.
 
Hongereni sana wazee wa Juve ni mwanzo mzuri natumai marudio mtafanya vizuri na tutawaona semi- final.

Ahsante everlenk, kile cha nguruwe cha jana kimesafisha road to the semis, mechi ya pili itakua rahisi kwetu kuliko ya jana
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…