Juventus Special Thread

pirlo atafika miaka 50 bado ana ubora wake ..kazi yake kubwa nikuzunguka ile duara pale na akishika mpira anauamuru uende anakotaka....


Kwanini Gatuso yeye alichoka mapema? Au Clarence Seedof? Maana hawa ndio walikua viungo hatari Wa Milan na mbele kidogo alikuwepo mdogo wao Ricardo Kaka!
 
Kwanini Gatuso yeye alichoka mapema? Au Clarence Seedof? Maana hawa ndio walikua viungo hatari Wa Milan na mbele kidogo alikuwepo mdogo wao Ricardo Kaka!


Gattuso ilikuwa ni lazima achoke mapema mno...kama ulikuwa makini kuangalia kilomita anazokimbia uwanjani plus vikumbo na mitama anayowabetua wenzie utajuwa wazi ilikuwa lazima achoke akifika miaka 35 tu...

kuhusu Seedorf jamaa alianza kucheza kitambo mno na still alikuwa anaubwenga mpk pale uongozi wa Milan ulivyomfuata ili aje awe Kocha
 
Tunaenda semi, tumecheza mpira mbovu na kama Monaco wangekuwa makini wangepata ushindi. Kuna kazi kubwa sana mbele yetu. Barca, Bayern, na Real madrid, Hii ni miamba hapo ulaya.


huwa siamini ktk imani...
nina hakika Juve wataingia Final kwa kumdunda yeyote yule ajae mbele yake.
ktk haya mashindano najuwa wazi Juve wanaelewa thamani ya hatua ya Nusu Final...
 
Kila la kheri.. Mungu asaidie Juve azame kwa pep.. hahahah.. hongera Juve
 
Wajukuu
kutoka moyoni, nawatakia kila la kheri. Kama hamtakutana na sisi, basi mshinde mechi zenu zote, japo ni mlima kwenu.
Forza Juve.
 
Heri yako kijana, una moyo wa chuma.
Mtazamo wangu, juve wanakalishwa tena goli za kutosha ambazo zitafanya hata round ya pili isiwe na msisimko
 
Wajukuu
Mwisho wenu umefika, ila tutabaki kuwa ndugu, na sitashangilia kwa heshima niliyonayo kwenu. Kila la kheri.
Forza Juve next season.
 
Wajukuu
Mwisho wenu umefika, ila tutabaki kuwa ndugu, na sitashangilia kwa heshima niliyonayo kwenu. Kila la kheri.
Forza Juve next season.

Uefa wanajitahidi kuhakikisha fainali inakua kati ya Madrid Vs Bayern, hawajui sisi tuna mipango tofauti na hiyo
 
Uefa wanajitahidi kuhakikisha fainali inakua kati ya Madrid Vs Bayern, hawajui sisi tuna mipango tofauti na hiyo

Hahaha kama kuna ukweli vile. Ila kutoka moyoni, tusipobeba sisi, bora m'bebe nyie katika timu zilizobaki. Japo Trezeguet aliniliza, ila sijawahi kuwachukia kamwe.
 
Juve mmepata mpinzani mwepesi kwenye semi final,Allegri akipanga karata zake vizuri ubingwa ni wenu
 
Nilitamani sana tupangiwe hawa RM. Nikaomba game ya kwanza tucheze pale Turin. Yote yametokea kweli. Kazi imebaki kwa Alegri na kikosi chake, kuweka mikakati na kuwavua ubingwa hawa jamaa.

Naiona Juve ikielekea Berlin kwa fainali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…