zurima ramadhan
Member
- Oct 26, 2024
- 10
- 0
Mratibu wa Mradi wa Kumuimarisha Mwanamke katika Masuala ya Ungozi SWIL kutoka Jumuiya ya Wanawake Wenye ulemavu Zanzibar JUWAUZA Zakia Shabani Daudi amesema wataendelea kuwahamasisha wanawake katika kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ili kupata viongozi wenye sifa na weledi.
Ameyasema hayo huko Mfenesini katika mkutano uliowakutanisha wananchi wa shehiya ya Mwakaje, Mfenesini, Mbuzini pamoja na waigizaji wenye ujumbe mbali mbali ambazo zinamuimarisha mwanamke kushiriki katika masuala ya uongozi.
Amesema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha wananchi ili kuzungumzia masuala yanamuathiri mwanamke kushiriki katika harakati za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi sambamba na kuwawezesha wanawake hao katika kufikia malengo yao.
Soma Pia: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?
Kwa upande wake muhamasishaji wa jamii Mulhat Ame Haji amesema changamoto kubwa wanayoipata katika uhamasishaji huo ni kuwepo kwa mfumo dume katika baadhi ya jamii katika kuwaona wanawake wanagombea na kutowashirikisha wanwake wenye ulemavu kwenye nafasi hizo.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki katika mkutano huo wamesema baadhi ya wanawake wamekuwa nyuma kushiriki katika nafasi hizo sambamba na kuwataka wanawake kuweka nia ya kugombea katika uchaguziwa mwaka huu ili kujiletea maendeleo katika shehiya zao.