Jux: Nampenda sana Vanessa

Jux: Nampenda sana Vanessa

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

MSANII wa muziki wa RNB nchini, Juma Jux, anayetamba na wimbo wake mpya wa ‘Utaniua’ amefunguka juu ya uhusiano wake na mwanamuziki wa Tanzania, Vanessa Mdee, kuwa kwake kwanza ni familia yake halafu anafuata Vanessa Mdee.

Alipoulizwa na mtandao huu kuhusu uhusiano wake na Vanessa, alisema: ”Nampenda Vanessa kuliko msichana yeyote yule na sitegemei kumuacha, hata familia yangu inajua kuwa nina upendo Mkubwa kwa Vanessa.

“Nikiwaga mbali na Vanessa huwaga asubuhi nikiamka cha kwanza naingiaga Instagram kumuangalia baada ya hapo ndo nampigia simu siwezi, kumpigia simu bila kuangalia picha zake. Kiufupi nampenda sana Vanessa,“ alisema Jux.

Kuhusu kupata mtoto, Jux alifunguka kwamba: “Sa’hivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo kwa sasa wa kujipanga kupata mtoto na mpenzi wangu pia mtoto wangu wa kwanza nataka nimuite jina la Karim na si jina jingine zaidi ya hilo.”


Muungwana
 
Sasa anataka mtoto kwa mwenza mwingine au uyo vanessa sijamuelewa
 
Vanessa mwenyewe nilisikia hatarajii kupata mtoto siku za karibuni
 
Mi simooo..!

[HASHTAG]#Mtu[/HASHTAG] asiyejulikana
 
Vijana wanawaza watoto kabla ya ndoa/familia ndio maana mambo tafrani sana siku hizi.
 
Back
Top Bottom