Jux naye aisoma namba, duka lake lakumbwa na bomoabomoa ya kushtukiza

Jux naye aisoma namba, duka lake lakumbwa na bomoabomoa ya kushtukiza

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Msanii Jux ambaye ni mmiliki wa duka linalo uza nguo za 'brand' yake ya 'African Boy', ametoa sababu iliyofanywa duka hilo lipitiwe na bomoa bomoa, katika eneo la Sinza jijini Dar es salaam

GpxQVOlP.jpg

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Jux amesema duka hilo limevunjwa kwa sababu mwenye nyumba alikuwa na mgogoro na Mahakama kuhusu kiwanja hicho ndipo Mahakama ilipoamuru nyumba hiyo ivunjwe japo hawakupewa taarifa ya aina yoyote na mwenye nyumba huyo.

Nimepata hasara kubwa kwa kuvunjwa kwa jengo hilo kwa kuwa kuna baadhi ya vitu vimepotea pamoja na pesa taslimu shilingi Milioni moja imeibiwa na mpaka sasa, baba mwenye nyumba wangu hapatikani na sijui yupo wapi ?", alisema Jux

Chanzo: EATV
 
Vipi kwenye kampeni zilizopita alikuwa team push up?
 
Dada yake Jux aitwaye Fatma ajirekodi video akionyesha duka lake lililobomolewa bila taarifa yoyote ile. inasemekana wamiliki wa duka hilo ni Jux na dada yake huyu aitwaye Fatma.

kipindi hiki bado jux anatesa na wimbo wake mpya uitwao Utaniua
 
No. inasomeka vzr sana,ikitoka hapo isomeke kwa kina Jb,Rich,Aunt ezekiel,Thea,Steve Nyerere... maana hao ndio frontline..

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Hilo eneo lilikuwa na mgogoro na case ilikuwa mahakamani na kilichotokea mwenye jengo hilo kashindwa case hivyo jengo hilo limeamuliwa livunjwa....... inawezekana mwenye jengo hakuwambia kama kulikuwa na case mahakamani na hukumu ilikuwa inatolewa jana.
 
No. inasomeka vzr sana,ikitoka hapo isomeke kwa kina Jb,Rich,Aunt ezekiel,Thea,Steve Nyerere... maana hao ndio frontline..

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
Tatizo lako unafikiri kila jambo ni siasa.....
 
Tatizo lako unafikiri kila jambo ni siasa.....
Sehemu gani nimetaja siasa.Katika hao niliowataja nani ni mwanasiasa hapo?

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Dada yake Jux aitwaye Fatma ajirekodi video akionyesha duka lake lililobomolewa bila taarifa yoyote ile. inasemekana wamiliki wa duka hilo ni Jux na dada yake huyu aitwaye Fatma.

kipindi hiki bado jux anatesa na wimbo wake mpya uitwao Utaniua

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji134] [emoji134]
Daaah we Mkuu
Ni Mkali Wa Kuunga
Matukio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
August 29, 2017

bomoabomoa imepita kwenye duka la dada wa mwimbaji wa Bongofleva Juma Jux ambalo lilikuwa linauza bidhaa zake za mavazi ya African Boy.

Fatma ambae ni dada wa Jux alichukua video na kusema “Hii ndio hali niliyoikuta baada ya kufika dukani kwangu leo asubuhi, tumebomolewa bila kupewa taarifa yoyote…. vitu nilivyoweza kuvitoa ni hivi, kila kitu changu kimebomoka”

“Ni mgogoro uliokua kwa wenye nyumba wenyewe, nachukua hii video si kama nina nguvu ila najikaza… Wateja wangu mniwie radhi tutaendelea kuwasiliana kwa simu” –Fatma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magu

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
dogo akipeleka poda trip moja tu China anakuja kufungua lingine kubwa zaidi ya hili.....namkubali sana jux
 
Back
Top Bottom