JWTZ hawapaswi kuwa na uhalali wowote wa kuchukua silaha dhidi ya wananachi

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Katika jeshi nilijifunza jambo moja, kwamba kuna amri halali na isiyo halali. Kwa mfano, huwezi ukaamriwa kumpiga risasi askari mwenzio na kutii kwa sababu tuu umeamriwa na kamanda wako.

Sasa je, Amiri Jeshi Mkuu anaweza kutoa amri ambayo sio halali kwa jeshi, JWTZ kwa sababu tu yeye ni Amiri Jeshi Mkuu? Tukumbuke Amiri Jeshi mkuu ni mwanadamu kama wanadamu wengine, inawezekana kabisa akatoa amri kwa JWTZ ambayo si halali, na JWTZ watapaswa kuwa na uhalali wa kutoitii!

Basi nini lifanyike ikiwa hilo litatokea? Na tunapoongelea amri isiyo halali inayoweza kutolewa na Amiri Jeshi Mkuu wa JWTZ, ni amri kama zipi?

Kujibu swali kama hilo ni vizuri kuelewa kazi za JWTZ ni zipi - na huenda tunajua ni kulinda usalama na kupambana na maadui wa Tanzania, ambao wanaweza kuwa ndani au nje ya mipaka ya Tanzania.

Adui wa nje ya mipaka ya Tanzania ambaye atafanya Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania kutoa amri kwa JWTZ wapambane nae - hilo ni rahisi kueleweka. Lakini vipi adui wa ndani, na nani anaweza kuwa adui wa ndani ambae uadui wake kwa taifa utalazimu JWTZ watumike?

Labda tuanze na kanuni, kwamba katika mazingira yeyote yale, iwe marufuku na hata laana kabisa, kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuchukua silaha dhidi ya Wananchi wa Tanzania (WTZ) ambao hawana silaha mikononi, ndani ya mipaka ya Tanzania. Tuanzie na hapo.

Ikitokea kwamba JWTZ wamechukua silaha dhidi ya WTZ, basi itamaanisha JWTZ limekoma kuwa jeshi la wananchi, WTZ! Raia wa Tanzania "mwenye fujo" bado ni raia ya Tanzania na JWTZ ni la kwake.

Sasa vipi ikiwa wananchi wamebeba silaha, ndani ya mipaka ya Tanzania, ili kufanya vurugu? Bado hiyo haihalalishi JWTZ kuwa deployed kukabiliana na wananchi (WTZ) ndani ya mipaka ya Tanzania. JWTZ wanapaswa kuelewa kwamba, kazi ya kupambana na wananchi wa Tanzania ndani ya Tanzania, wawe na silaha au wasiwe na silaha, ni kazi ya jeshi la Polisi, sio yao. Hata kama JWTZ wataingilia kati basi iwe kama "neutral force", kwa ajili ya kwenda kurudisha amani na usalama, au kuleta suluhu kati ya raia na Polisi.

Kwa msingi huo, JWTZ hawapaswi kuwa na uhalali wowote wa kuchukua silaha dhidi ya wananachi, WTZ, ndani ya mipaka ya Tanzania, iwe wana silaha au hawana silaha!

Lakini lazima tukubali kwamba JWTZ wanaweza kuchukua silaha dhidi ya wananchi ikiwa tu wananchi hao watawashambulia wanajeshi wakiwa ndani au nje ya kambi za jeshi, kwa minajili ya kujilinda (self defence), pale ambapo raia hao wameonyesha bila shaka kwamba lengo lao ni kuwashambulia na kuwaangamiza askari wa JWTZ au kushambulia vituo vya kijeshi.

Hivyo basi, vitu kama maandamano ya raia, vurugu siku ya uchaguzi nk, hata siku moja visiwe sababu ya kuhalalisha JWTZ kuchukua silaha dhidi ya wananchi, WTZ. Hayo ni mambo ambayo yabaki kuwa chini ya jeshi la Polisi.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=nD7XdXDN6mo

Jambo hili halipaswi kukubalika hata kidogo. Hii ni kazi ya Polisi, na hakuna mahali Polisi wamesema wanadhani watashindwa kutunza amani nchini wakati wa uchaguzi.

Hongera kwa kupita huko, lakin tupo wengi mpaka waliotumikia kabisa kwa kipindi kirefu. Kwanza amri kutoka juu kama hiyo jeshini huwa inakuwa documented, jeshi wana utaratibu mzuri sana tofauti na (polis) ambao wao wakiambiwa kwa mdomo wanaruka

Jeshin wana document, ili yakitokea maafa, alietoa order na walio tekeleza wasipate pa kuruka. Is why wanasiasa wangi wanashindwa ku access tpdf maana wana utaratibu serious sana
 
Hapana, sio amri zote za kijeshi zinaambatana na documentation. La sivyo kungekuwa na urasimu sana
 
Hao viongozi wa jeshi wanakuwa machawa wanataka teuzi za ubalozi na ukuu wa mkoa baada ya kustaafu
 
CCM wanajitahidi sana kuwarubuni JWTZ kwa muda mrefu sana. Natumaini JWTZ hatakubali kurubuniwa kirahisi kiasi hicho na wataendelea kuwa JWTZ, sio JCCM
 
Hapana, sio amri zote za kijeshi zinaambatana na documentation. La sivyo kungekuwa na urasimu sana
ni kweli si zote, nasemea zile major, zinazotoka COS or ngazi za juu zaidi kwa rais. Huwa ziko documented , just incase. How do i know, i was there.
Zaidi ya hapo ni kunyemeleana
 
Katika jeshi nilijifunza jambo moja, kwamba kuna amri halali na isiyo halali. Kwa mfano, huwezi ukaamriwa kumpiga risasi askari mwenzio na kutii kwa sababu tuu umeamriwa na kamanda wako.

Sasa je, Amiri Jeshi Mkuu anaweza kutoa amri ambayo sio halali kwa jeshi, JWTZ kwa sababu tu yeye ni Amiri Jeshi Mkuu? Tukumbuke Amiri Jeshi mkuu ni mwanadamu kama wanadamu wengine, inawezekana kabisa akatoa amri kwa JWTZ ambayo si halali, na JWTZ watapaswa kuwa na uhalali wa kutoitii!

Basi nini lifanyike ikiwa hilo litatokea? Na tunapoongelea amri isiyo halali inayoweza kutolewa na Amiri Jeshi Mkuu wa JWTZ, ni amri kama zipi?

Kujibu swali kama hilo ni vizuri kuelewa kazi za JWTZ ni zipi - na huenda tunajua ni kulinda usalama na kupambana na maadui wa Tanzania, ambao wanaweza kuwa ndani au nje ya mipaka ya Tanzania.

Adui wa nje ya mipaka ya Tanzania ambaye atafanya Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania kutoa amri kwa JWTZ wapambane nae - hilo ni rahisi kueleweka. Lakini vipi adui wa ndani, na nani anaweza kuwa adui wa ndani ambae uadui wake kwa taifa utalazimu JWTZ watumike?

Labda tuanze na kanuni, kwamba katika mazingira yeyote yale, iwe marufuku na hata laana kabisa, kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuchukua silaha dhidi ya Wananchi wa Tanzania (WTZ) ambao hawana silaha mikononi, ndani ya mipaka ya Tanzania. Tuanzie na hapo.

Ikitokea kwamba JWTZ wamechukua silaha dhidi ya WTZ, basi itamaanisha JWTZ limekoma kuwa jeshi la wananchi, WTZ! Raia wa Tanzania "mwenye fujo" bado ni raia ya Tanzania na JWTZ ni la kwake.

Sasa vipi ikiwa wananchi wamebeba silaha, ndani ya mipaka ya Tanzania, ili kufanya vurugu? Bado hiyo haihalalishi JWTZ kuwa deployed kukabiliana na wananchi (WTZ) ndani ya mipaka ya Tanzania. JWTZ wanapaswa kuelewa kwamba, kazi ya kupambana na wananchi wa Tanzania ndani ya Tanzania, wawe na silaha au wasiwe na silaha, ni kazi ya jeshi la Polisi, sio yao. Hata kama JWTZ wataingilia kati basi iwe kama "neutral force", kwa ajili ya kwenda kurudisha amani na usalama, au kuleta suluhu kati ya raia na Polisi.

Kwa msingi huo, JWTZ hawapaswi kuwa na uhalali wowote wa kuchukua silaha dhidi ya wananachi, WTZ, ndani ya mipaka ya Tanzania, iwe wana silaha au hawana silaha!

Lakini lazima tukubali kwamba JWTZ wanaweza kuchukua silaha dhidi ya wananchi ikiwa tu wananchi hao watawashambulia wanajeshi wakiwa ndani au nje ya kambi za jeshi, kwa minajili ya kujilinda (self defence), pale ambapo raia hao wameonyesha bila shaka kwamba lengo lao ni kuwashambulia na kuwaangamiza askari wa JWTZ au kushambulia vituo vya kijeshi.

Hivyo basi, vitu kama maandamano ya raia, vurugu siku ya uchaguzi nk, hata siku moja visiwe sababu ya kuhalalisha JWTZ kuchukua silaha dhidi ya wananchi, WTZ. Hayo ni mambo ambayo yabaki kuwa chini ya jeshi la Polisi.
Unawapangia wewe kama nani? Unajua miongozo yao kiutendaji? Unajua mipaka yao kiutendaji?
 
Polisi wameshindwa kazi, hadi wapewe hawa baka baka? Mbona hatarii hii, Lol
 
didn't your mom tell you ?
ⓘ 𝘠𝘰𝘶 𝘤𝘢𝘯'𝘵 𝘴𝘦𝘦 𝘵𝘩𝘪𝘴 𝘮𝘦𝘴𝘴𝘢𝘨𝘦 𝘣𝘦𝘤𝘢𝘶𝘴𝘦 𝘺𝘰𝘶 𝘢𝘳𝘦 𝘶𝘴𝘪𝘯𝘨 𝘢 𝘤𝘩𝘦𝘢𝘱 𝘮𝘰𝘣𝘪𝘭𝘦 𝘱𝘩𝘰𝘯𝘦
 
Back
Top Bottom