Jeshi letu lina udhaifu mkubwa katika 'information war'. Nina mifano miwili ya haraka haraka:
1. Vijana wetu waliposhambuliwa Darfur hivi karibuni, walijibu mapigo na kuua attackers wengi tu. Lakini hili halijapigiwa debe na JWTZ mbali na udhalili wa kuonekana waliuawa na kujeruhiwa wao tu!! Kwa maoni yangu, tukio lile limetudhalilisha mno kimataifa. Cha kusikitisha ni sio kwamba vijana wetu hawakupambana. Walipambana kishujaa na kuwaua washambulizi wao wengi zaidi ya wale saba wa upande wetu. kilichotokea ni kwamba wale jamaa walikuwa smart walikusanya maiti wao na kukimbia nao kupoteza ushahidi! Ingawa walikuwa under UNAMID lakini JWTZ walitakiwa walipigie debe la mapambano waliyofanya na athari waliyoingiza kwa adui!
2. Waasi wa M23 majuzi walifurushwa Kibati. Hawakujiondosha kama walivyodai baadaye! Walipata kipondo cha nguvu toka kwa JWTZ hadi wakakimbia kila mmoja na njia yake. Lakini waasi hao wamefanikiwa kupenyeza ujumbe katika vyombo vya habari vya kimataifa kwamba wao walijiondosha Kibati kwa hiari yao. Kipondo kile kilitakiwa kipigiwe debe hadi dunia nzima ijue kuwa JWTZ sio ya kuichezea, ingawa baadhi ya majirani zetu wanajua hilo! Nasisitiza kitengo cha Habari cha JWTZ kiimarishwe na kipewe zana za kisasa kabisa za kutendea kazi ili kuhakikisha wako 'sharp & smart' katika information war coz ndio mambo ya kisasa hayo! Information is power!!