JWTZ kuna udhaifu idara ya habari

JWTZ kuna udhaifu idara ya habari

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
697
Reaction score
218
Jeshi letu lina udhaifu mkubwa katika 'information war'. Nina mifano miwili ya haraka haraka:

1. Vijana wetu waliposhambuliwa Darfur hivi karibuni, walijibu mapigo na kuua attackers wengi tu. Lakini hili halijapigiwa debe na JWTZ mbali na udhalili wa kuonekana waliuawa na kujeruhiwa wao tu!! Kwa maoni yangu, tukio lile limetudhalilisha mno kimataifa. Cha kusikitisha ni sio kwamba vijana wetu hawakupambana. Walipambana kishujaa na kuwaua washambulizi wao wengi zaidi ya wale saba wa upande wetu. kilichotokea ni kwamba wale jamaa walikuwa smart walikusanya maiti wao na kukimbia nao kupoteza ushahidi! Ingawa walikuwa under UNAMID lakini JWTZ walitakiwa walipigie debe la mapambano waliyofanya na athari waliyoingiza kwa adui!

2. Waasi wa M23 majuzi walifurushwa Kibati. Hawakujiondosha kama walivyodai baadaye! Walipata kipondo cha nguvu toka kwa JWTZ hadi wakakimbia kila mmoja na njia yake. Lakini waasi hao wamefanikiwa kupenyeza ujumbe katika vyombo vya habari vya kimataifa kwamba wao walijiondosha Kibati kwa hiari yao. Kipondo kile kilitakiwa kipigiwe debe hadi dunia nzima ijue kuwa JWTZ sio ya kuichezea, ingawa baadhi ya majirani zetu wanajua hilo! Nasisitiza kitengo cha Habari cha JWTZ kiimarishwe na kipewe zana za kisasa kabisa za kutendea kazi ili kuhakikisha wako 'sharp & smart' katika information war coz ndio mambo ya kisasa hayo! Information is power!!
 
Mkuu mi ninavyofahamu JWTZ si Jeshi linalopenda kujisifia hapa Afrika. Mfano Chukulia Rwanda, Kenya Uganda. Rwanda walinunua APACHE lakini walijitangaza vibaya, Uganda nae kanunua Sukhoi Sita ambazo Ghali sana matokeo yake zikawa kila siku zinaruka angani ili wajioneshe kuwa wana ndege. Uendeshwaji wa JWTZ umetulia sana, huwa hatupigagi makelele lakini kila tunapoenda huwa hatuharibu. Mkuu acha jeshi liwe hivi hivi kuwa kimya kwenye mambo yake.
 
Wanajeshi wao wanausemi kuwa Jeshi sio shirika la mkonge ambalo inawezekana kila mtu anaweza kutoa taarifa bila kujali hadhira. Wewe umesukumwa na utashi wako bila kutafakari. JWTZ wanamafunzo ya kutosha kuuwawa askari wanaolinda amani haihitaji propaganda huko hawajaenda vitani.
 
Kwanini wautangazia umma? Wako sahihi sana kutosema.
kweli mkuu sasas hivi wamenunua zana kali ila hata ukitafuta kwenye mtandao huzipati tafuta za ug au apl taarifa njenje sasa jwtz wanazo drone lakini kimya
 
nenda soma mitandao ya majuu jwtz haijifagilii inafagiliwa mfano sasa inatajwa kua ni jeshi la 7 kwa ubora africa la pili nyuma ya kenya kwa zana kali la pili nyuma ya ethiopia kwa kua na idadi kubwa mengine siri sio yote waweke hadharani
 
Ni kweli gen parton vitu vingine sio vya kutangaza , mfano unaishi na majirani alafu hujui ni wazuri au wabaya unawatangazia umenunua bastora kama kuna adui yako kati ya hao majiran zako yeye atanunu s.m.g na mabom kabisa ili siku akitaka kukutoa jasho anakua anajua udhaifu wako, hivyo ni vyema wanavyo fanya wanajeshi wetu wa(jwtz) kuliko watu wanavyofikiri.
 
Kama kutangaza ingekuwa inachangia ushindi mbona Taifa star ingeshachukua Kombe la dunia? Unless otherwise uniambie kuna agenda nyingine nyuma ya kutaka hiyo information..
 
Acha liende kimya kimya hivyo hivyo...kazi ya propaganda waachieni m23 na Kagame wao wasiojiamini.!!
 
we jamaa nilisikia ni mnyarwanda hivi umeishabadili uraia???

hapa tunapiga kimya kimya atakayeumia akimblie UN
 
Back
Top Bottom