Muda mrefu jeshi letu limekuwa likipata heshima kimataifa pamoja na umaskini wa taifa letu kutokana na kushiriki oparetion nyingi kwa mafanikio makubwa eg Kagera war, Comoro, Liberia etc.
Ufanisi huo ulitokana na mafunzo mazuri,nidhamu ya askari pamoja na ushirikiano mzuri kati ya askari hao na viongozi wa juu jeshini etc.
Sasahivi niliyotaja kama baadhi ya sababu ya za ushindi hazipo au zipo kwa kiwango cha chini sana.
Tukianza kwenye mafunzo, hali ni mbaya kwani kujiunga na jeshi sasa inachukuliwa kama ajira nyingine yoyote kitendo kinachofanya watoto wa vigogo wengi kujiunga huku wazazi wao wakiagiza kwamba wasifanye mazoezi 'magumu'. Pia viongozi wakuu hawana ushirikiano mzuri na askari wa chini kwani wamekuwa wakiwaona kama mashine za kufanya kazi bila kujali maslahi yao. Mfano, wakati wa maafa ya kilosa askari walishiriki kuokoa na kurudisha hali ya miundombinu iliyoharibika katika hali nzuri na kuahidiwa kupewa posho lakini mpaka sasa hawajapewa.
Si hivyo tu bali hata mitambo iliyonunuliwa na kitengo cha maafa na kukabidhiwa JWTZ ili isaidie kurahisisha kazi ili cheleweshwa kufika eneo la kazi hivyo askari kuumia bila sababu.
Mbaya zaidi baada ya kazi ile kumalizika, mitambo iliyoletwa ilikubaliwa wapewe wataalam wa jeshi ili iweze kutumika kwa wakati mwingine kama itatokea tatizo kama hilo lakini cha kushangaza, bila taarifa za wazi mitambo hiyo ameichukua kigogo mmoja na kuwakodishia SUMA JKT kwa maslahi binasfi.
Kutokana na wakubwa hao baadhi kutowajali askari na watendaji wengine wa chini imefika hatua ya kuwakata hata pesa zinazo tolewa na UN kwa wale wanaoenda DARFUR ambapo kila mwanajeshe bila sababu za msingi hukatwa 20 percent ya pesa za UN huku pesa yake nyingine aliyokuwa apewe ya chakula hapewi bali kuishia mikononi mwa hao vigogo wachache.
Hali hii imefikia kuwavunja moyo askari na kukosa ile nidhamu ya kazi kwa kujua ukweli kuwa wakuu wao wanawaibia.
Hali hii isiporekebishwa heshma ya jeshi letu itaporomoka sana.