JWTZ mpaka leo imeshindwa kuajiri wasomi wenye vipaji halisi, sababu hizi hapa...

Naongelea MENTALLY UPSTAIRS wala SIO MANGUVU YA MWILINI. ELEWA MADA KWANZA NDO UCHANGIE SIO KUKURUPUKA TU. Mnajaza seva bure!
 
Kaka elewa maada inazungumzia nini? Elimu bila ubunifu hamtaweza kitu. Najua wengi wenu hapa ni wanajeshi ndo maana mnatetea tu bila hata kuelewa.
 
Mkubwa sihitaji kuajiliwa jeshini nina ajira tayari tena ya kujidai kiafya cozi sina elimu ya kuunga unga ambayo ingenifanya nije jeshini ok! Jadli maada.
 
Huyo mmoja ya waliotimuliwa nini sasa unataalamu gani bana wenyewe wanakuambia kila kizi ina msingi wake hayo mengine baadae ubwana umetimuliwa nini sasa kazi ya maana kwingine unataka nini kazi ya maana umaana kwako tu inatusaidia nini sisi?
 
Acheni ujinga nyie na upuuzi wenu kakosea ni ll,m ,(legum magister)

we mwenyewe umekosea,angekua amesoma asingeshidwa kutofautisha kati ya LL.B na LLM,kwa kukusaidia tu LL.B-Lex Legum Baccalaureate(LL.B,Lex Legum Magister(LL.M)
 
mkuu hukutaka kusulutishwa asietaka kusulutishwa amejiajiri alafu ukubari kuwa jeshi mpaka ulaya na amerika lipo na mfumo wake ndio huo kama unaushauli peleka serikalini na sio JF hajasaidia kitu unazani jeshi kama jeshi unataka kila huduma yao iwe zaidi ya uraiani huku raia wakiishi maisha haya hali ya jeshi inategemea hali ya nchi kiuchumi.
 
Naongelea MENTALLY UPSTAIRS wala SIO MANGUVU YA MWILINI. ELEWA MADA KWANZA NDO UCHANGIE SIO KUKURUPUKA TU. Mnajaza seva bure!

Kama unadhani UPSTAIRS uko safi, then think again. Next time uje na hoja za msingi. Kama unadhani wanajeshi wana hawako safi vichwani mwao umepotoka sana. Na kama unadhani maguvu si sehemu muhimu ya jeshi, then ni heri ukatafute kibarua cha kubofya computer. Jeshini kuna wasomi weeengi sana tena wanafanya vizuri kuliko hata unavyodhani. Sasa watu waliopigika mitaani ndo mnakuja na mada za kupotosha namna hii.

Wakati unajidanganya na kudanganya watu kuhusu upstairs, jeshi lina mfumo wake wa kupima watu waliofit vichwani, tofauti na UDSM. Ndio maana si lazima mwenye 1st class akafaa jeshini. Na pale panapohitajika ujuzi ambao haupatikani jeshini, kuna raia kibao huajiliwa kutokana na nafasi zao. SI KILA ANAYEJIDHANI YUKO FIT UPSTAIRS ATAWEZA KAZI ZA KIJESHI. Acha kupotosha watu hapa, talk sense. Mambo ya kutaka kuwa treated kama special class of soldiers ni kutaka kuleta uraia jeshini. Standards MUST be maintained, thats all mjaza server.
 
Kaka elewa maada inazungumzia nini? Elimu bila ubunifu hamtaweza kitu. Najua wengi wenu hapa ni wanajeshi ndo maana mnatetea tu bila hata kuelewa.

Umepotosha mada, swala hapa ni vipaji maalum jeshini. Labda mtuambie mlikusudia umaalum gani hasa. Na hilo suala la elimu bila ubunifu halina mashiko, why? Nionyeshe bajeti ya ulinzi ya Tanzania. Usinyooshe kidole bila kuelewa tatizo liko wapi, na ndio mwisho wa siku mnabaki kujidanganya eti jeshini hakuna wasomi, what a shame.
 

1. a.Je, ni macadet wangapi wenye elimu kubwa waliohitimu na wangapi waliofukuzwa?
b.Je, ni unadhani ni mamlaka gani inayohusika kufukuza cadet?

2. a.Je, jeshi linatengewa bajeti kiasi gani kwa ajili ya tafiti mbali mbali?
b.Je, ni yapi majukumu ya msingi ya jeshi letu? Je jeshi linayatekeleza? Ni yapi majukumu ya ziada?
c.Je, unadhani ratio ya AMO to MD (20:80) ni uwiano mbovu kiasi hicho?
d.Je, jeshi lina vikosi vingapi? Je, kuna vituo vingapi vya afya jeshini? Je unadhani madaktari wote ni vema wawe Lugalo kusubiri migomo?
e.Je, unadhani taifa limewahi kujitosheleza katika nyanja za wataalamu mbalimbali? (mf. madaktari)
f.Je unajua ni mara ngapi kikosi cha mainjinia wamejihusisha katika kuokoa maisha ya watanzania?

3. a.Je unadhani ni wakati muafaka sasa jeshi likaondoa mafunzo magumu yanayowaudhi wasomi wetu na kuweka aina ya mafunzo yatakayovutia wasomi wazuri zaidi jeshini?
b.Je, ungependekeza wakufunzi wa TMA wawe na level gani ya elimu?
c.Je, unaonaje kama jeshi litaachana na strict discipline na kuangalia zaidi elimu ya mtu?

4. Je, unadhani msingi mkuu wa jeshi lolote lile (hata kama ni insurgents) ni nini?

Ni hhayo u.
 
Mimi ninalikubali Jeshi la wananchi kwa operations zao, ila naona wengi hapa badala ya kuongea the real bottom fact wanateteea as if wao ni wasemaji wa jeshi
1.kama wasomi wa kweli wapo jeshini mbona mambo mengi sana wapo kimya tu mfano deni la taifa linazidi kukua siku baada ya siku.huwa wanapataga nafasi ya kuisaidia kuishauri serikali hata kidogo?? au mtasema ni siasa
2.mfano jeshi la marekani au hata S.Africa bajeti yao ipo wazi hapa TZ imekaaje
3.nimegundua mawazo mbadala hayakubaliki kwa Jeshini esp yale ambayo hawajazoea:Technology inahusika sana kubalini kataeni kwa maendeleo mazuri ya jeshi towards hyo Modern army
4.mimi ni raia tuu tena mwema ..haha ila siku jeshi likinihitaji nipo tayari kujitoa kwa ajili ya nchi yangu..
N.B punguzeni mashambulizi kwa mleta mada embu angalieni the other side of coin.
 

1. Kama mawazo yenyewe mnayoyaita real bottom fact ndo haya, basi ni bora mkae kimya. Next utauliza wabunge wanazuiwa kuhoji mambo mazito bungeni na jeshi limekaa kimya tu.

2. Ongea na mbunge wako

3. Mawazo mbadala ya kutaka jeshi lisimamie deni la taifa ni kweli hayajazoeleka jeshini na hayatazoeleka, samahani kwa hilo. Hata hiyo technolojia mnayoling'ang'ania jeshi labda ipo katika idara gani hapa Tz? Mbona mnataka kulifanya jeshi letu lionekane liko kwenye sayari nyingine yenye neema tofauti na Tz? Be realistic, msing'ang'anize mawazo yenu tu.

Na hao mnaowaita WASOMI WA KWELI hebu mnipe mfano wake basi. Ni kama akina nani basi nje ya jeshi? Mtoe na mtazamo wenu kama wakichukuliwa jeshini watalifanyia nini jeshi tofauti na kilichopo hivi sasa? Inaeleweka wengi humu licha ya kutokubali ukweli kuwa ni mambumbumbu wa utendaji wa jeshi, pia hata hawajui kiini cha matatizo ya nchi yetu. Na ndio sababu wanarukia kushambulia kila taasisi kumaliza hasira zao na haziishi.

Ndo hao hao utawasikia wakishangilia eti mwanajeshi kafa kwa ajali, " ooh ndo wakome, wanajidai sana hao, wanajiona wako juu ya sheria...." upuuzi mtupu. Wanadhani mtu anapokuwa mwanajeshi anakuwa saint, kwamba isolated incidents haziwezi kutokea. Kisha wanakuja hapa kujiita wasomi wa ukweli wenye mawazo mbadala. Ukiwauliza ni mawazo yapi hayo, watakwambia hatutaki jeshi la kutumia maguvu, tunataka jeshi la kisomi. Watakao pigana wakiwa mtandaoni. Hawajui hata core soldiering ni nini. WASOMI WA UKWELI. Eti jeshini hakuna wasomi wa ukweli. I hate this word.
 
Ukiwa jeshini inabidi uwe mtii na kupokea amri bila kuuliza wasomi siku zote ni wadadisi kabla ya kutii amri watajiuliza kama hiyo amri ni sahihi au la pia wasomi wasingefumbia macho ufisadi unaoendelea hapa nchini kama kuuza rasilimali za nchi na hayo wamejifunza toka jeshi la Nigeria ambalo lilikuwa likiajili wasomi matokeo yake kila mara nchi ikawa inapinduliwa
 

wasomi wa kweli hawapo kule jeshini ila huku uraini wapo sasa kipi kinachofanywa na wasomi wetu hawa wa kiraia huku uraiani mbona na wenyewe wamekaa kulalamika tu bila kusaidi chochote kama jeshi aliwajiri utaalam wenu peleka urain tunataka inchi ya viwanda magari ya undwe hapa si kukosoa tu.
 

Kwa hiyo duniani jeshi la wasomi ni Nigeria tu? Poor logic, do your home work. Hujui unachokiongelea na huo usomi wako haujakusaidia. You are a problem.
 

Mkuu hawa wala si wasomi bali ni opportunists. Ukiwapa nafasi wanawazia kupiga hela tu. Hakuna hoja ya kisomi hapa zaidi ya kwamba wengi humu ni mbumbumbu wa mfumo wa majeshi. Eti wasomi wanaogopwa kwamba watahoji ufisadi na madeni makubwa. Msomi wa kweli angeangalia mumo wa serikali na vyombo vyake vya ulinzi halafu akaja na logical deductions wala si hoja za kitoto namna hii. WASOMI WA UKWELI? Aibu kubwa.
 
Kwa hiyo duniani jeshi la wasomi ni Nigeria tu? Poor logic, do your home work. Hujui unachokiongelea na huo usomi wako haujakusaidia. You are a problem.
wewe ndio unatakiwa ufanye homework kumbuka hapa tunaongelea jeshi la jwtz ndio maana nimechukulia mfano wa Nigeria ambao majeshi yao yamejaa wasomi ila kuna majeshi kama ya USA,CHINA,ISRAEL hata SOUTH AFRICA ambayo yamejaza wasomi na hata kiteknologia wako mbali usiwe unakurupuka soma uelewe
 

Kweli mkuu umenena vema.
 

Haya nyie makanjanja mmelifanyia nini taifa? Au mpaka mpatb nafasi jeshini. Acheni upuuzi wenu, jeshi linao wasomi wengi tu. Habari za kuwaza mapinduzi ni akili zilizo choka. Wakati Foday Sanko anapindua aliongoza wasomi wangapi? Vipi kuhusu Samwel Doe? Mnadhani jeshini kila mmoja lazima awe na digrii? Mmeshindwa kushindana kwenye soko la ajira EA mmegeukia jeshi ambako hamkidhi vigezo, kisha mnaleta hoja za kutaka jeshi liendeshwe kiraia? Wacheni huo uzandiki. Kama kweli mnawazia mapinduzi, basi mmechoka vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…