Mkuu
Mwita Maranya nikuhakikishie tu kuwa duniani kote hakuna kozi za wasomi na wasiosoma. Mafunzo ya kijeshi yako standard no matter what. Ukiwa katika uwanja wa medani bahati mbaya masters yako haitokusaidia kama hujaiva kimbinu. Ndo maana hata corporal ambaye ni competent anaweza kuitikisa nchi. (Nadhani unamkumbuka Iddi Amini). Tena ukihudhuria vyuo vya nje huwezi amini, ni balaa zaidi. Wanakuambia kwamba technology fails, that is why we don't use it in training. Kule kila kitu ni manual tofauti uongo wanaopeana watu. Technology utafundishwa kwenye unit yako sio chuoni. Tatizo wabongo wanafikiri digitali ina affect basic soldiering, no way.Wale wanaotamani kuonda maisha wavumilie kupitia katika kikaango kwanza, ndo wakakae maofisini na bachelors na masters za mambo ya utawala.
Na pale mnaposema vipaji maalum I can't understand what you are driving at? Jeshini vipaji maalum hupelekwa Commando, PT na sehemu nyingine zinazohitaji outstanding performance. Sasa hivi vipaji maalum sijajua ni nini. Nadhani mnamfahamu Balati. He was the greatet leader of all time katika commando, na huyo ni mmoja tu. Alipata bachelor na masters akiwa karibu kabisa na kustaafu. Kumbe basi jeshini kuna askari wengi sana wenye military knowledge ya hali ya juu kuliko most of graduates. Siwapondi hawa, isipokuwa tu kuna notion fulani imejengeka kwamba wasomi wanachukiwa jeshini, lakini ukweli ni kwamba wanaojiita wasomi wengi wao hawapendi kupitia rigorous training. Wanataka watambuliwe usomi wao wakati wa mafunzo kwamba mimi ni daktari, mhasibu, mchimi, n.k. Wakati wa training haya mambo hayana maana yoyote, na ndipo competent corporal ukimtishia elimu yako atakuwa willing kukudhihirishia kuwa katika kile ulichofuata pale, yeye ni zaidi yako. Guys, it is the matter of self discipline, that's all it takes. Otherwise mtabaki ku-lament kila siku kama hamtaki kutambua kuwa military knowledge is a profession in itself.
Daktari akifuzu mafunzo atatakiwa kutibu majeruhi mstari wa mbele, bunduki begani.
Mhasibu atatumia bachelor yake kulipa mishahara mstari wa mbele (vitani mishahara hulipwa kama kawaida).
Logistician atafanya kazi kupeleka logistics frontline (tena hawa huwindwa sana vitani).
N.k. Sasa usipokuwa trained utaperform vipi majukumu hayo? Tusilewe na kazi za jeshi wakati wa amani, kikinuka watu huvua kombati na kujificha, don't be one of them! Just do your part and everything should be fine.
MILITARY TEACHES YOU HOW NOT TO DIE!!!!!!!!!!