GE2025 JWTZ nawaomba ili kuleta muafaka wa maandamano ongeeni kwa hekima na hawa

GE2025 JWTZ nawaomba ili kuleta muafaka wa maandamano ongeeni kwa hekima na hawa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Rijali jandoni

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2018
Posts
2,174
Reaction score
2,265
Wakuuu poleni na kazi naomba niende moja kwa moja kutokana na muda, maandamano yanayo endelea nchi nzima ni kutokana na wananchi kutaka mabadiliko (reforms)

Hili jambo ni la wananchi yaani watoto wetu, ndugu zetu na vijana tunao wafahamu tukizubaa tutajaza mitaa ikiwa na miili ya ndugu zetu, tukumbuke hatupigi risasi na kuua magaidi bali ni wananchi wa kawaida wasio amini watu ama mawazo ya walio wapa ridhaa, maadam serikali ni watu na walio barabani ndio watu tutawategemea na ndio tunategemea kodi zao tuishi, basi tufanye jambo kwa ajili yao, kabla na wao hawaja anza kujihami kwa namna yao wenyewe

Ili kutuliza kisha kufanikisha amani, naomba mjitahidi kuwalinda kuanzia sasa, na kwa hekima kukaa nao watu hawa, pamoja na wengine ambao sitoweza kuwataja

1. Mzee Warioba kwanini huyu kwa sasa anaweza sikilizwa na wananchi, kwasababu wananchi wanacho andamana ni kuhusu kupotea kwa kile walicho hisi ni amani ya moyo na uhuru wa kuongea, mzee wetu ameweza kuongea kwa uwazi na watu wakakubaliana, ni kweli changamoto zinatokea watu wakiwa kwenye viti, kwa sasa mleteni au mtafuteni muongee nae kwa hekima hili swala litapungua na kisha kuisha

2. Polepole ni ukweli usio pingika hapa mwishoni ameongea sana na kwa kuongea kwake chuki imejengwa baina ya wananchi wa kawaida, ambao kwa namna moja ama nyingine ni ndugu zenu na hata watoto wenu, kwa namna hiyo naombeni kama bado yupo hai basi wiki hii nzima ama ndani ya siku saba atafutwe, apatiwe matibabu huko alipo, na afikee kwa uma na kueleza watu watulie maana anayo kwa kiasi chake anayo weza kuyasema na watu wakatulia, kwa sasa watu hawataki tena lugha ya siasa ni vitendo tukichelewa ama kusubiri tutamaliza ndugu zetu, watoto na hata jamaa bila kutumia hekima, kama hayupo hai basi ongeeni na hawa wengine

3. Lisu kwa sasa naimani yupo na mzima, huyu akitoka cha kwanza atulizwe na wazee wa pande zote maana jambo limeshakuwa zito, na watu hawawezi kutoka walipo yaliyo anza yameathiri saikolojia vijana wapo tayari kufa zaidi tutazika watoto zetu na hata ndugu wa watoto wetu, Lisu anaweza ongwa kwa nafasi yake na watu wakatulia ila kwa sasa apatiwe ulinzi wakutosha, kuhusu watakayo ongea wapeni uhuru na muda, kikubwa wawasilishe yanayo hitajika na wananchi

4. Gwajima ni kiongozi wa kanisa na ana waumini lakini ukizingati aliongea hapa mwishoni na kuleta fikra na mawazo mengi kwa watu na huenda watu wengi tunao waona barabarani nikutokana na hawa watu wote kuongea, kwa upande wa Askofu Gwajima kaeni nae kisha muone namna nzuri ya kutatua hili swala maana kwa sasa watu wanataka kuona walio jificha wakitoka nnje, ni ngumu kusema ila nadhani muda wa haki na kuijua kweli umefika wakuu

5. Heche huyu amewekwa mahali mnapo fahamu siku kadhaa kwa sasa kama yupo timamu na mzima basi apatiwe mazingira mazuri pamoja na ulinzi ili baada ya siku kadhaa tuwaone wakija hewani sio kwa kuwekewa vizuizi ila wapate uhuru na nafasi ya kuongea ukweli utakao anzisha utendaji wa moja kwa moja juu ya Taifa hili, kwa sasa dunia ina badilika hasa Africa hili ni wimbi la pili la ukombozi kutoka kwenye siasa za utegemezi wa nnje, nasikitika kusema haya ila hatuna budi kukivaa na kukinywa hiki kikombe kwa sasa huu moto upo nyikana, amini utashika kwenye nyasi hizi zote zilizokauka hapa Africa,

hakuna Tiafa lililooweza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa watu na wakatulia baada ya maandamano basi Tanzania ikawe wa kwanza kama ilivyo utamduni na mfano kwa Afrika ukaanze hapa kwetu

6. Viongozi walio pita wenye hekima, busara na wasio na tamaa na huko mwanzoni hawakusikika ila wanajulikana kutokana na nyadhifa walizo shika vipindi vilivyo pita, ni ngumu ila kwa sasa iwepo kampeni ya kuleta haki na tukumbuke haya yakiwa yanaendelea basi kile kitabu kinaweza kuletwa na kikatangazwa,ni mazito ila kulinusuru Taifa hatuna namna

7. Wachungaji, masheikh walio kimbia na kunyamza walipo ongea, watu ama wasanii walio kamatwa kupotea, kama wapo hai basi waombeni waongee na wananchi kwenye hili jambo, ifike wakati sote tuamini vijana wengi tunao waona wapo barabarani wanataka haki wanataka kuona walio nyamaza wakiongea na sio kuongea tuu bali kuwapa uhuru wa fikra, ni swala litakalo weza chukua miezi lakini litaiponya taifa, huu ndio uhalisia.


Note, TUKUMBUKE TAASISI ZA KISISASA HAZITOWEZA KUPOTEA ILA KWA SASA, TUCHAGUE HAWA WANAO AMINIKA NA KWA NAMNA MOJA WAMEPITIA WALIO PITIA, NA UKIANGALIA WAMETOKA VYAMA TOFAUTI, HAPO BAADAE TURUDISHIE TAASISI ZOTE KWENYE MFUMO WA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI WAO UWEPO KWA VITENDO, AINA YA SERIKALI SIJUI ITAKUAJE ILA MTAANGALIA KWENYE HIVYO VIKAO

HII NI HATMA YA WATU MILLION SABINI, IKIJUMUISHA WATOTO ZETU, NDUGU ZETU, WAZAZI WETU, MARAFIKI NA JAMAA ZENU WOTE HAWA WAPO MIKONONI MWENU WAKUU ZETU

ILA KWA SASA MFUMO UNAWEZA BADILIKA HAKUNA NAMNA NDIO TANZANIA MPYA NASIKITIKA KUONGEA HIVI, INAHITAJIKA UWEPO MFUMO NNJE YA TAASISI MOJA, NA HATA CHOMBO KIMOJA CHA ULINZI UTAKAO SIMAMIA MASLAHI YA TAIFA, KIKISHINDA CHAMA AU WATU FULANI BASI WAPEWE DHAMANA LAKINI UWEPO MFUMO WA SIRI WENYE WATU MAHIRI, TIMAMU WENYE UWEZO KUTOKA VYAMA VYETU ZIWE TAASISI ZA KISERIKALI, VYOMBO VYA ULINZI NA WENGINE WATAKAO TOA DIRA NA MALENGO YA NCHI

NAWAOMBA MSILETE MTU TOFAUTI, WATU WALIOMSIKIA AMEFANYA JAMBO FULANI HII ITAWEZA LETA HASIRA ZAIDI

Poleni wakuu wote, niwatakie kazi njema Maafande

TUIPENDE TANZANIA KAMA TUNAVYOPENDA MAMA ZETU, TANZANIA NI MTOTO KWENYE AMANI TUMLINDE, NA KWENYE GADHABU ATAKUWA NI MAMA WA KUTUFICHIA AIBU YETU

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Huu ni moto wa kuangamiza nchi yetu pendwa, ikiwezekana kuutuliza kisha kuzima basi tufanye hilo, hawa vijana wakipata ushawishi na maagizo tofauti kutoka kwa watu, tutazika watoto na ndugu zetu wengi
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%

Lakini kabla ya haya kufanyika, cha kwanza kabisa kinachopaswa kufanyika immediately sasa na sio kesho ni kupata KIONGOZI WA SERIKALI YA MPITO WA MUDA na kama ni Jeshi basi ni vyema zaidi....

Na baada ya hapo, funga mipaka yote kwa muda (hakuna mtu kutoka wala kuingia), funga Airports zote (No flight in, No flight out). Na mwisho kamata wote waliokuwa wakijiita "serikali", detain wote waliosababisha maafa haya kuanzia na:

1. Samia Suluhu Hassan na genge lake lote wanaojiita "serikali"

2. Viongozi wote wa Tume ya Uchaguzi

3. IGP Wambura, RPC wa kanda maalumu ya DSM Muliro na ZCO wake Faustine Mafwele na RC na RPC wa Mbeya na wengine wengi kwa kadiri inavyofaa..
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%

Lakini kabla ya haya kufanyika, cha kwanza kabisa kinachopaswa kufanyika immediately sasa na sio kesho ni kupata KIONGOZI WA SERIKALI YA MPITO WA MUDA na kama ni Jeshi basi ni vyema zaidi....

Na baada ya hapo, funga mipaka yote kwa muda (hakuna mtu kutoka wala kuingia), funga Airports zote (No flight in, No flight out). Na mwisho kamata wote waliokuwa wakijiita "serikali", detain wote waliosababisha maafa haya kuanzia na:

1. Samia Suluhu Hassan na genge lake lote wanaojiita "serikali"

2. Viongozi wote wa Tume ya Uchaguzi

3. IGP Wambura, RPC wa kanda maalumu ya DSM Muliro na ZCO wake Faustine Mafwele na RC na RPC wa Mbeya na wengine wengi kwa kadiri inavyofaa..

Ndugu, kupata kiongozi wa serikali ya mpito ni swala lenye nafasi yake huenda wana hatua nalo, maana uongozi mpya ni kuunda washirika wapya, na mambo yaende kama kawaida na zaidi, tuombe Mungu

Kuhusu hili la viongozi wa Serikali na baadhi ya taasisi kusomewa mashitaka ni zito na baadhi sheria haziruhusu kwa watu fulani, hekima itumike, ndio maana hawa watu wana hitajika na wengine ndani ya vyombo waje watulize hali

Wakuu na viongozi wengine wakumbuke hili jambo la sasa ni la wananchi wenyewe hakuna kiongozi wa siasa alie mstari wa mbele, ni very sensitive
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%

Lakini kabla ya haya kufanyika, cha kwanza kabisa kinachopaswa kufanyika immediately sasa na sio kesho ni kupata KIONGOZI WA SERIKALI YA MPITO WA MUDA na kama ni Jeshi basi ni vyema zaidi....

Na baada ya hapo, funga mipaka yote kwa muda (hakuna mtu kutoka wala kuingia), funga Airports zote (No flight in, No flight out). Na mwisho kamata wote waliokuwa wakijiita "serikali", detain wote waliosababisha maafa haya kuanzia na:

1. Samia Suluhu Hassan na genge lake lote wanaojiita "serikali"

2. Viongozi wote wa Tume ya Uchaguzi

3. IGP Wambura, RPC wa kanda maalumu ya DSM Muliro na ZCO wake Faustine Mafwele na RC na RPC wa Mbeya na wengine wengi kwa kadiri inavyofaa..

Tulipata wasaha wa kubadilishana mawazo hapa ndani, andiko langu liligusia umuhimu wa wananchi kupewa elimu ya amani maana wenye nia ovu wanaweza wahadaa ila hili la sasa sina mamlaka ya kuliita ovu lakini muafaka usipo fikiwa wananchi wanaweza shawishika kwa namna nyingine

Hii hali inaweza sambaa Afrika nzima, kikubwa tuombe Mungu ipite haraka ni gharama na sadaka nzito ya mabadiliko kwa karne hii ya sasa, na ikiwezekana tuoneshe mfano wa umoja tena ila wenye maendeleo kwa miaka 50 na mia ijayo

Tanzania ni paa la Afrika mabadiliko mengi yenye hekima na mvuto huanza Tanzania

Hili litapita, tuombe Mungu tuwe chachu ya kuigwa kwenye safari na wimbi hili la mabadiliko barani Afrika

Mungu Ibariki Tanzania
 
Pamoja na ajenda hizo zote, hawa waliopiga risasi ndugu zetu wakajeruhi na kuua ni LAZIMA wasakwe na wapate adhabu stahiki
 
Umeongea mengi zaidi Ila mwisho ... Samia na genge lake aachie nchi .. Hili ndio la msingi zaidi

Kwa wakati huu watu wanaweza fikiria haya kutokana na taharuki ya ghafla ilio tokea, kikubwa tuombe Mungu hekima na huruma ijae ama kuletwa juu ya fikra za viongozi wa nafasi zote, mkuu hekima itumike hekima hili jambo ni zito sana sana

Tukikimbilia huku kwa sasa kila mmoja ana jilinda hali itaenda kuwa mbaya zaidi hapa Tanzania
 
Pamoja na ajenda hizo zote, hawa waliopiga risasi ndugu zetu wakajeruhi na kuua ni LAZIMA wasakwe na wapate adhabu stahiki

Tuzidi kuomba Mungu, maana utakuwa wakati wa kuwindana, a transition that majority are demanding needs to be soft, huko juu wasipo weza kuelewana sparks might result to a disaster
 
Back
Top Bottom