Elections 2010 JWTZ waanza mazoezi ya machafuko

Hakuna ni mazoezi yao ya kawaida mwaka huu wamerecruit vijana wengi sana katika, kada mbalimbali kwa ajili ya mafunzo na kama umezoea kupita njia hiyo utaona kuwa kunaendeshwa mafunzo ya aina mbalimbali tangu mwezi wa pili kwa hiyo nadhani ni sehemu ya kazi yao ya kawaida
 

Mh!! Watu wanachukulia poa!!
Ngoja tusubiri tuone.
 
Kama askari hawa wako tayari kuwapiga marungu,mabomu na kuwaua Baba zao,shangazi zao,mama zao na ndugu zao walioibiwa kura zao na hawakuridhika, ili kuwafurahisha wachache wenye maslahi binafsi huku wao wenyewe(askari) wakiwa wanabaki kwenye lindi la umasikini na taabu na kutojua hatima yao baada ya kustaafu, basi tuna jeshi ambalo askari wake wanahitaji kuchunguzwa akili.
 
Mh!! Watu wanachukulia poa!!
Ngoja tusubiri tuone.
Kama ningekua na uwezo hii thread ningeiondoa, inazidi kutisha watu ziadi kuliko kutaarifu. Kama watu, tena wanaoweza hata kutumia internet wanaogopa Jeshi, Je mwanakijiji wa Kasyabone ambako hata gazati halifiki atafanya nini? kama sio kutoenda kupiga kura kabisa na kujifungia ndani. Bado natoa rai mambo ya jeshi tuyapuuze tu, ili tusiitishe jamii zaidi. Lengo lao ni kutisha, na tutakapotishika tumekwisha wakuu.
 
Kutumia JWTZ au JKT kwa ulinzi ni kwenda kinyume na matumizi ya majeshi hayo...Hawa hawana weledi wa kutuliza ghasia na kudeal na watu. Wapiganaji wamefundishwa kutumia bunduki kwa ajili ya kuua tu wakati polisi na magereza wao wanafundishwa kukamata na kumlinda muharifu.... Ukitumia jeshi tu jua mauaji yanakaribia. Kwa wale waliokwenda jkt enzi zile watakumbuka hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…