JWTZ yatangaza nafasi za kazi kwa vijana wenye mafunzo ya JKT

JWTZ yatangaza nafasi za kazi kwa vijana wenye mafunzo ya JKT

"Nnacho jua form 6 wameenza kuitwa ikitokea kuitajika kwa 4m4 wataitwa"

Mwisho wa kunukuu
Form 6 au wale wa chuo unaowazungumzia wewe hilo litakuwa ni kundi la 8 maalumu kaka lakini kuna kundi la 43 hilo ni mchanganyiko humo kuna degree takers mpaka wa form four na ndio hao walioomba mwezi March.
 
kwahiyo ina maana wale walioomba march bado wapo kwenye mkakati? au ni siasa tuu za jeshi letu kama kawaida
We acha tu mkuu maana wale wa March bado hawajaitwa hao waliomaliza waliomba mwaka jana na ndio kundi la 42, wale wa mwezi March inabidi liwe kundi la 43 ndio mpaka sasa kozi haijaanza ni siasa juu ya siasa, hivyo kwa aliyeomba mwezi March atulie asikilizie bado hawajaanza kozi.
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi kwa Vijana ambao wametumikia au wamefanya mafunzo ya kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa miaka miwili kisha wakarejeshwa majumbani.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda akiwa Dodoma leo amesema “Vijana hawa walifanya mafunzo JKT na walipotimiza miaka miwili wakapewa vyeti baada ya kukosa fursa aidha kuandikishwa JWTZ au katika Taasisi/Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, walirejeshwa majumbani lakini sasa fursa imepatikana, naishukuru Serikali tumepata nafasi kuandikisha Vijana hawa”

“Kijana anatakiwa awe Raia wa Tanzania wa kuzaliwa umri wa miaka 18-26 kwa Form IV hadi Form VI, kwa wenye elimu ya juu kufikia shahada ya uzamili umri usizidi miaka 27, awe na afya nzuri ya mwili na akili, tabia njema, nidhamu nzuri na awe hajawahi kupatikana na kosa la kijinai au kushtakiwa Mahakamani na kufungwa, vilevile awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya Shule na taaluma na pia awe hajawahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo na awe na cheti cha kuhudumia JKT kwa miaka miwili”

“Maombi kwa mkono yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia hivi sasa ninavyotangaza hadi March 20,2023, yatumwe kwa Mkuu wa Utumishi Makao Makuu ya JWTZ, P.O.BOD 194 Dodoma, Tanzania au pia kupitia ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Zamani ilikuwa inatengenezwa vita halafu nafasi zinatangazwa kwa maelfu.
 
Back
Top Bottom